Wednesday 22 February 2017

TCU: ORODHA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU 2016/2017

...

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
Image result for tcu tz
TAARIFA KWA UMMA
WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la uhakiki wa sifa za wanafunzi wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kwa mwaka 2016/2017 limekamilika katika baadhi ya vyuo. Katika kutekeleza zoezi hilo Tume imebaini kuwa kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa.
Orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika. Hivyo, wanafunzi wote wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya Juu nchini wanaweza kutazama matokeo ya uhakiki wao kupitia kiunganisho (link) (Bonyeza Uhakiki wa Sifa za Udahili).
Tume inawaarifu wanafunzi wote ambao majina yao yameorodheshwa wawasiliane na vyuo vyao ili kuthibitisha sifa zao kabla ya tarehe 28 Februari 2017. Wanafunzi ambao hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na Tume na hivyo kukosa sifa za uanafunzi.
TCU inatoa rai kwa wanafunzi wote kutembelea tovuti ya Tume (www.tcu.go.tz) mara kwa mara ili kupata taarifa mpya kuhusu uhakiki wa sifa za wanafunzi.
Imetolewa na
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

20/02/2017
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger