Monday, 16 May 2016

Mbarawa ‘Kuvaa Viatu’ vya Magufuli Kesho Bungeni

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wiki hii anatarajiwa kuanza kuvaa viatu vya Rais John Magufuli bungeni.

Kesho Profesa Mbarawa anatarajiwa kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Mbunge huyo wa kuteuliwa atakuwa na jukumu kubwa la kuwasilisha bajeti hiyo ambayo kwa takriban miaka 10 ilikuwa jukumu la Dk Magufuli.

Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi kwa miaka mingi kabla ya kujitosa kuwania urais kupitia CCM ambako aliteuliwa na kushinda Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka jana.

Sekta tatu alizopewa Profesa Mbarawa ni nyeti na ngumu, hivyo Watanzania wanasubiri kuona atakavyoanza bajeti yake ya kwanza kesho tangu kuteuliwa na Dk Magufuli kushika nafasi hiyo.

Ujenzi bado ni sekta inayotegemewa na Taifa katika kuingiza mapato na pia kusaidia huduma za jamii. Masuala ya ujenzi wa barabara, madaraja, mawasiliano na uchukuzi vyote ni muhimu kwa uchumi. Hayo yanatiwa nguvu na jitihada za Rais Magufuli za kukusanya mapato tangu aingie madarakani.

Suala la bandari ni eneo mojawapo litakalogusa bajeti ya Profesa Mbarawa. Kuliibuka masuala mengi ya ufisadi katika bandari ya Dar es Salaam, mambo yanayotegemewa kuligusa Bunge.

Mbali ya hayo, masuala ya mawasiliano yatakuwa pia na nafasi katika bajeti ya Profesa Mbarawa.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger