Sunday, 8 May 2016

JKT:TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USAILI WA VIJANA WATAALAMU WA TASNIA YA HABARI

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Kujenga Taifa linakanusha taarifa zinazosambazwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu za kiganjani na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa “Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ametoa nafasi maalum kwa wahitimu wa taaluma ya Uandishi wa Habari wenye elimu ya stashahada na shahada wanaopenda kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea”.

Habari hizo siyo sahihi kwani mchakato wa nafasi zote za vijana wanaotaka kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Kujitolea zimepelekwa kwenye mamlaka za Serikali za mikoa yote, ambapo kwa sasa zoezi hilo linaendelea katika ngazi za wilaya.

Aidha Makao Makuu ya JKT yanaendelea kusisitiza kuwa hayapokei na wala hayatapokea maombi yoyote ya kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2016.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 02 Mei 2016
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger