Friday, 20 May 2016

Elimu ya juu waanza kulipa mikopo

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Robert Kibona Mkurungezi wa urejeshaji mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa wa elimu ya juu (HESLB) (Kushoto)
JUMLA ya wadaiwa wapya 21,721 wa mikopo ya elimu ya juu wamejitokeza kwa lengo la kuanza kulipa madeni yao kufuatia agizo la siku 60 lililotolewa na Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu (HESLB).



Robert Kibona Mkurungezi wa urejeshaji mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa wa elimu ya juu(HESLB) ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu tathmini ya agizo la machi 14 lililotolewa na bodi hiyo kwa wanufaika wa mikopo na waajiri ili kutimiza wajibu wao kisheria .

Amesema jumla ya shilingi 151.5 Bilioni, zinatarajiwa kurejeshwa na wadaiwa hao ambao walikopeshwa ili kuwawezesha kupata elimu yao ya juu katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi kuanzia mwaka 1994.

Kibona amesema lengo la agizo hilo lilikuwa ni kuhakikisha madeni yote yaliyoiva yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi na agizo hilo limeshafikia kikomo Mei 13 mwaka huu.

Amesema kati ya wadaiwa waliopatikana, wadaiwa 19,528 walipatikana baada ya Bodi kuchambua taarifa za waajiriwa zilizowasilishwa na waajiri na wadaiwa wengine wapatao 2,007 walijitokeza kwa hiari.

“Waajiriwa wana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao, baadhi yao walifanya hivyo katika siku hizo sitini na tukawabaini wadaiwa hao,tunawapongeza waajiri kwa ushirikiano walioutoa na wanufaika wote waliojitokeza kwa hiari”alisema Kibona.

Aidha kibona aliongeza kuwa Bodi imeongeza siku 30 za ziada kuanzia Mei 20 mwaka huu kwa wadaiwa waliobaki kujitokeza na uamuzi huo umetokana na tathimini iliyoonyesha kuwa kuna idadi kubwa ya waajiri na wanufaika wanaoendelea kujitokeza.

Kwa upande wake Cosmas Mwaisobwa, Mkurungenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo amesema kuwa kiwango cha ukusanyaji wa madeni hivi sasa umefikia shilingi 8 bilioni ifikapo Juni mwaka huu.

Katika kipindi cha mwaka 1994/1995 hadi sasa, kiasi cha shilingi 2.44 Trilioni kimetolewa kwa wanufaika 378,504 wakiwemo wanafunzi wanaoendelea na masomo yao hivi sasa ambao kwa sasa hawana wajibu wa kulipa hadi pale watakapomaliza au kusitisha masomo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger