Wednesday 27 April 2016

Tahadhari ya Mvua kubwa na Upepo mkali f kuanzia tarehe 26-04-2016 Hadi 29-04- 2016

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha uwepo wa mvua kubwa na upepo mkali unaozidi kasi ya kilomita 40 kwa saa iliyotarajiwa kuanza jana hadi keshokutwa.

Sambamba na upepo huo, taarifa hiyo ya TMA imesema mvua za zaidi ya milimita 50 zinatarajiwa kunyesha huku bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 

Taarifa hiyo imeelezwa kuwa hali hiyo imesababishwa na mgandamizo mdogo wa hewa katika Pwani ya Tanzania unaotakana na kimbunga cha Fantala.

Maeneo yaliyotajwa na TMA kwamba yataathiriwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara, Unguja na Pemba na kwamba mvua hizo pia zinatarajiwa kusambaa hadi katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro na Mashariki mwa Manyara.

Ofisa Habari wa TMA, Monica Mutoni aliwataka wakazi wa maeneo hayo na watumiaji wa bahari kuchukua hatua stahiki ili kuepuka uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kujitokeza.

“Mvua hizi ni kama zile zilizonyesha wiki iliyopita. Wajibu wetu ni kutoa taarifa pale tunapoona kiwango cha juu cha mvua na upepo ili watu wachukue tahadhari. Kwa watumiaji wa bahari umakini uzidi kuongezeka kwani mawimbi yatakuwa makubwa na upepo wa bahari utakuwa kilomita 30 kwa saa,” alisema Mutoni.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger