Wednesday 4 November 2015

Tume ya taifa ya uchaguzi yaombwa kutoa tarehe ya kupiga kura jimbo la Lulindi.

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Tume ya taifa ya uchaguzi imeombwa kuweka wazi mapema iwezekanavyo tarehe ya kupiga kura ya ubunge jimbo la Lulindi vinginevyo ucheleweshaji huo unaathari kwa wapiga kura na vyama vyenye wagombea.
Tume ya taifa ya uchaguzi ililazimika kusitisha upigaji kura ya ubunge katika jimbo la Lulindi baada ya jina la mgombea wa chama cha wananchi CUF Amina Thomas Msham kukosewa katika karatasi za kupigiwa kura na kusomeka Msham Thomas Mcham.
 
Akizungumzia hilo mdhamini wa chama cha NLD ambaye pia ni mgombea wa jimbo la Lulindi Modesta Makaidi na uongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mtwara wameonyesha wasiwasi wao na kuzungumza haya.
 
Akizungumza kwa njia ya simu msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo Beatres Maiko amesema analitambua hilo na kwa sasa yuko jijini Dar es Salaam kufuatilia suala hilo.
 
Jimbo la Lulindi limefanikiwa kufanya uchaguzi wa rais na madiwani, wagombea ubunge wanaotarajiwa kupigiwa kura ni Jerome Bwanausi wa CCM, Modesta Makaidi wa NLD na Amina Thomas Msham wa CUF, jimbo lingine linalotarajiwa kufanyiwa uchaguzi mkoani Mtwara ni la Masasi mjini kutokana na mgombea wake Emmanuel Makaidi kufariki dunia.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger