Sunday 22 November 2015

Magufuli ataka mitazamo tofauti kuhusu albino

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Image result for magufuli
RAIS John Magufuli amesema nchi bado inakabiliwa na tatizo la imani za kishirikina dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kufanyiwa vitendo kinyume na haki za binadamu, ikiwemo kuuawa na kueleza kuwa kinachotakiwa ni kubadilisha mitazamo ya watanzania kuhusu albino.

Aidha, kukosekana kwa taarifa, ushahidi pamoja na ushahidi wa kimahakama wa matukio wanaofanyiwa albino ni changamoto nyingine kutokana na kufanyika kwa siri nyakati za usiku na wakati mwingine kushirikisha ndugu.

Dk Magufuli alisema hayo wakati wa mkutano wa siku mbili wa viongozi wa vyama na mashirika ya watu wenye ulemavu wa ngozi kutoka nchi zaidi ya 29 za Afrika huku nchi 12 na Ulaya kukiwa na wataalamu wa kutoa elimu kuhusu changamoto zinazowakabili albino.

Alisema bila kuwa na taarifa za kutosha ni vigumu kwa polisi kufungulia kesi wahusika wa vitendo hivyo na kuwataka washiriki wa mkutano huo kujadili kwa undani kuhusu suala hilo kwa lengo la kuangalia kisheria.

Dk Magufuli aliyewakilishwa katika mkutano huo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk Donan Mbando alielezwa kuwa pia nchi inakabiliwa na upungufu wa taarifa sahihi kuhusu albino inasababisha kuendeleza imani potofu kuhusu watu hao.

Alisema imani hizo zina mara nyingi zinazosambazwa na waganga wa kienyeji inasababishwa na kutoelewa usahihi wa watu hao kuzaliwa wakiwa albino.

Dk Magufuli alisema serikali imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanapunguza vitendo hivyo vya kikatili, ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo mbalimbali kwa ajili ya kuhudumia watu hao katika mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Shinyanga,Tabora na Tanga.

Mkurugenzi wa shirika la Under the Same Sun nchini, Vicky Ntetema alisema mkutano huo una washiriki karibu 200 kupewa mafunzo jinsi ya kulinda haki zao na kuhusiana na kesi kupeleka mahakamani kwani nchi nyingi wanafanyiwa ukatili lakini kesi hazifiki mahakamani.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger