Monday 16 November 2015

MALKIA ELIZABETH II WA UINGEREZA ATUMA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS JOHN POMBE JOSEF MAGUFULI

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAMU ZA PONGEZI
     RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

     Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa  “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako, nakutakia kheri pamoja na wananchi wa Tanzania”  amesema malkia katika salamu zake.

     Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza Mhe.  Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati,  mafanikio na furaha kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.

     Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu  ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz ambaye amemtakia kheri  Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina  imani kuwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya uongozi wako kuelekea katika kupata maendeleo  na mafanikio zaidi”.

  Amesema; na pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa kidemokrasia ulioendeshwa katika mazingira ya kistaarabu chini ya usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye kanda, bara na kimataifa na hivyo kuliletea sifa bara la Afrika.

     Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa salamu zake na zile za wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa ushindi wa kiti cha Urais.

     “Pia napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza kuwa  “Kwa hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM  Mamlaka ya kuipeleka mbele Tanzania  kuelekea kwenye mafanikio zaidi”.  Ameongeza.

      Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amesema Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya demokrasia barani Afrika.

     Naye Rais wa Jamhuri  ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck amemtakia Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio  katika kuendeleza Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na:
Premi Kibanga, 
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Novemba, 2015.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger