Monday 16 November 2015

TAARIFA KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA ZA UALIMU ELIMUMSINGI NA ELIMU YA SEKONDARI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
  TAARIFA KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA ZA UALIMU ELIMUMSINGI NA ELIMU YA SEKONDARI KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwataarifu wote waliochaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) baada ya Mfumo wa CAS kuonyesha kuwa umechaguliwa kwenda Chuo Kikuu cha Dodoma, utaratibu ni kusubiri UDOM na vyombo vyake vya ndani kuthibitisha majina hayo. Waliodahiliwa wanatakiwa kwenda chuoni baada ya kupata joining instructions na wito kutoka Chuo husika.

Kumekuwapo na wanafunzi waliosafiri kwenda kuripoti chuoni kabla ya taratibu hizi kukamilika na hivyo kusababisha usumbufu kwao wenyewe na kwa taasisi za NACTE na UDOM. Majina ya wanaotakiwa kwenda kuripoti na tarehe za kuripoti mara zote hutolewa na chuo husika. Kwa kuwa majina yamekwenda vyuoni kwa makundi (batches) sio makundi yote yamepitishwa na katika mchakato wa ndani ya vyuo.
Baraza (NACTE) hutoa uchaguzi wake ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi kuangalia tovuti za vyuo mbalimbali kusaka majina yao. Iwapo kwa sababu zozote UDOM itashindwa kuwapokea baadhi ya waliochaguliwa, Baraza litawapa nafasi katika vyuo vingine. Ikumbukwe kuwa kuna vyuo vingi ambavyo havijapata wanafunzi wa kutosha.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
15 Novemba 2015
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger