Wednesday 26 November 2014

MPYA:TAARIFA KUHUSU WANAFUNZI WALIODAHILIWA IMTU,2014-15

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
Image result for tcu tanzania





 Taarifa Rasmi kwa Umma kuhusu Programu ya Pre-Entry ya Kutoka IMTU

Itakumbukwa kuwa Tume ya Vyuo Vikuu katika kikao chake cha 52 cha tarehe 18 Machi 2011 iliamua kuwa kuanzia mwaka wa masomo 2011 / 2012 hakutakuwa tena na Programu za Pre-Entry na vyuo vyote viliagizwa kusitisha ufundishaji wa programu hizo. Vyuo vikuu vyote vilijulishwa kuhusu maamuzi hayo kwenye kikao maalum cha saba cha kamati ya pamoja ya udahili (Joint Admission Committee) tarehe 9 Februari 2012. Kwa maamuzi hayo vyuo vyote viliagizwa kuandaa na kuwasilisha programu za aina hiyo kwa kutumia mfumo mpya wa Tuzo za Vyuo Vikuu (University Qualifications Framework – Level 6).


Hata hivyo hivi karibuni ilibainika kuwa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU) kilikuwa kikiendelea kufundisha programu hiyo na wanafunzi 111 walihitimu katika programu hiyo. Kwa kuwa programu hiyo ilikuwa haitambuliwi na Tume, wahitimu hao walikata rufaa kwa Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mujibu wa sheria ya vyuo vikuu Sura ya 346 ya sheria za Tanzania. Baada ya kupitia rufaa yao, Mheshimiwa Waziri kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 5(2)(b) aliagiza kwamba wahitimu hao 111 wa programu ya Pre-entry ya IMTU waruhusiwe kusoma programu ya MBBS ya IMTU kwa

1


kuwa ndivyo ilivyokusudiwa wakati wa kuanzisha programu hiyo.

Kutokana na maagizo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, tunapenda kuujulisha umma ya kwamba, kwa kuwa IMTU imesitishwa kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2014 / 2015 wahitimu hawa wanaweza kudahiliwa chuo kingine chochote kilicho tayari kuwapokea kufuatana na taratibu za udahili zilizopo.

Aidha, Tume inasisitiza kuwa programu za Pre-entry zilishasitishwa na kuwa programu zote za masomo lazima zifanyiwe tathmini na kupata ithibati ya Tume kabla hazijaanzishwa na kudahili wanafunzi. Kwa taarifa hii tunawataka vyuo kuwasilisha programu zao ili kupatiwa ithibati kabla ya kuanza kudahili wanafunzi ili kuepusha usumbufu wa namna hii.


Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
























2

 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger