Friday 14 November 2014

BREAKING NEWZ:WALIOCHAGULIWA UDOM SPECIAL PROGRAMME KUSOMESHWA BURE HATA KAMA HUKUJAZA FORM ,UNATAKIWA KUWAHI CHUO MAPEMA ILI UJAZE FORM YA MKOPO

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOYslide5
TANGAZO MUHIMU KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STASHAHADA MAALUM YA ELIMU KWA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI CHUO KIKUU CHA DODOMA
Chuo Kikuu cha Dodoma kinawatangazia wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Stashahada Maalum ya Elimu kwa masomo ya Sayansi na Hisabati kuwa usajili umeanza tangu tarehe 8/11/2014 na wanatakiwa kuzingatia  yafuatayo;
1.    Wanafunzi wote waliochaguliwa wanafursa ya kupata mkopo wa kugharamia masomo yao kwa asilimia mia moja (100%)

2.    Wanafunzi ambao hawakupata nafasi ya kuomba mikopo watapewa fursa ya kujaza fomu za maombi mara baada ya kufika Chuoni na kukamilisha usajili
3.    Wanafunzi walioomba na wanaotarajia kuomba mkopo toka bodi ya mikopo wataruhusiwa kujisajili kabla ya kulipa ada na gharama mbalimbali za masomo hapa Chuoni
4.    Usajili utafungwa rasmi baada ya wiki moja kuanzia tarahe 12/11/2014

Imetolewa na:
Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Taaluma, Utafiti na Ushauri
Chuo Kikuu cha Dodoma
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger