Wednesday, 10 August 2022

RC CHALAMILA AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KWA MAENDELEO YA MKOA WA KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila amewataka watumishi kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na vyombo vya habari katika kikao kikao cha Mkuu wa Mkoa na watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa tarehe 9 Agosti 2022, amewataka watumishi na viongozi wote kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha Mkoa unapata maendeleo kupitia umoja wao.

"Viongozi mnapotofautiana na mmoja wapo kumchongea maneno ya uzushi mwingine kwa mkubwa wao ujue yeye ndiye mwenye tatizo maana zipo ajenda nyingi za kuzungumza kama shule, afya, maji na barabara na si kumsema mwenzako. Kaeni kwa pamoja na zungumzeni kwa pamoja ili muwe na malengo ya pamoja" ,amesema Mh. Chalamila.

Ameongeza kuwa yote hayo ni kuepusha migogoro maana hakuna migogoro yenye visababishi viwili, siku zote migogoro mingi kisababishi ni kimoja lazima kuna mmoja ndiye sababu ya mgogoro.

"Na mimi Mkuu wa Mkoa sipendi kusikia hivyo napenda kusikia Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani na Mameya mko pamoja na kama kuna jambo linashindikana tunalirekebisha kwa njia za kitumishi zinazoeleweka", amesema Mh. Chalamila.


Share:

MCHUANO MKALI RUTO NA ODINGA UCHAGUZI MKUU KENYA

 

Hadi sasa bado mgombea Urais William Ruto, ameendelea kuongoza kwa asilimia 51.65, akifuatiwa na Raila Odinga mwenye asilimia 47.71.

– William Ruto (UDA) anaongoza kwa kura 1,377,854 (49.74%)

– Raila Odinga (AZIMIO) anafuatia akiwa na kura 1,356,726 (48.98%)

ZOEZI la kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu wa rais uliofanyika jana nchini Kenya, limeendelea usiku kucha wa kuamkia Jumatano huku Wakenya wakisubiri kwa hamu matokeo rasmi.

Ushindani mkubwa katika kinyang’anyiro cha urais ni baina ya wagombea wawili, naibu wa rais William Ruto na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC inakabiliwa na shinikizo la kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki. IEBC imekiri kwamba takribani vifaa 200 vya kielektroniki vya kuwatambua wapiga kura vilishindwa kufanya kazi kati ya vifaa 46,000.



Wananchi wengi wa Kenya wana matumaini na kura ya mwaka huu kuwa italeta mabadiliko katika maisha ya kila siku wakati wakikabiliwa na kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei.
Share:

JINSI NILIVYOIMARISHA NGUVU ZA KIUME ZA MUME WANGU



Kila mwanamke hufurahia furaha katika ndoa yake kila wakati. Mapenzi mazuri kwenye ndoa ama kwa hakika huandamana na vitu vingi kila mara. Mapenzi bila ya tendo la ndoa kwenye ndoa nyingi huleta wapenzi kukosana kila wakati.

 Kwa jina ni Patricia kutoka kwenye kaunti ya Nairobi. Tulikuwa kwenye ndoa na mume wangu Karimi kwa muda wa miaka miwili sasa. Hali ilikuwa shwari kabisa kwani alikuwa mtu mwenye bidiii na mapnzi jambo lilinipelekea mimi kumpenda kwa kila hali. Sikuwa na mwingine niliyepanga kumpenda zadi yake kwani ama kwa hakika alikuwa amenizuzua ajabu.

Baada ya siku kusonga nilipata udhaifu fulani wa mume wangu. Kila wakati tulipokuwa tukishiriki ngono alikuwa analegea na kila mara alilalamika kwamba alikuwa mchovu. Ama kwa hakika hakuna lolote alilokuwa akifanya kunipa raha kingono.

 Swala hili lilinikwaza sana. Wakati mwingine hata nilikuwa nikimvalia vijisketi vidogo vya kumzuzua lakini hakuna chochote alichokuwa akiona. Hata nilipokuwa namguza uume wake alibaki kutabasamu tu kwani hakuna chochote kilichokuwa kikifanyika. Hapo nilijua bayana kwamba alikuwa na uhaba wa nguvu za kiume. Swala hili liliniwekea kiu cha kushiriki ngono kwani nilikuwa na mazoea ya kufanya tendo lile kila siku. Sasa mume wangu alikuwa bwege sikuwa na mtu wakunizuzua kingono.

Kila mara alipojaribu alifanya kwa muda wa dakika tano kama jogoo na kisha kulala hoii. Jambo lile lilikuwa linanivunja moyo kila mara. Hii ilipelekea kwake kuyatumia madwa ya kuzuzua nguvu za kiume. Kila alipotumia dawa hizi tulishiriki ngono kwa muda mrefu na hapo alinitimizia kiu changu cha kushiriki ngono. 

Baada ya siku kadhaa niliona kwamba dawa zile zingekuja kumharibikia siku moja na hapo nikaanza kumtafutia suluhisho la kudumu. Niliwatembelea madaktari wengi wa miti shamba kwa ajili ya usaidizi lakini hakuna aliyekuwa akinipa suluhisho kamaili la kupata suluhisho la kuongeza nguvu za kiume.

Kupitia ujumbe kutoka kwa kipindi fulani redioni, niliweza kumsikiza daktari Kiwanga ambapo watu wengi walikuwa wakimpigia simu kumpongeza kwa ajili ya kuwasaidia waume wao kupata nafuu kutokana na kuwa na nguzu hasi za kiume. Hapo nilimpigia simu na akanipa mwaliko kwenye afisi zake mjini Nakuru. Baada ya wiki moja nilifung safari hadi mjini Nakuru kwani nilikuwa sna hamu ya kumsaidia mume wangu. Daktari Kiwanga alinipa mizizi ya kiasilia aliyonishauri niwe nikiipikia kwenye chakula cha mume wangu. Nilirejea nyumbani na ama kwa hakika nilizingatia yote aliyonishauri.

Baada ya siku mbili tuliposhiriki ngono na mume wangu, hali ilikuwa toifauti kweli. Alikuwa mchangamfu kwani alikuwa akifanya tendo lile kama mfungwa aliyefunguliwa kutoka kwenye gereza. Kila mara mimi ndiye nilikuwa nikimwambia “tosha gari” ama kwa hakika furaha ilikuwa katika ndoa yetu kwa uwezo wa daktari Kiwanga.

Daktari Kiwanga hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa na magonjwa mengineyo. Husuluhisha shida za kifamilia kama kutokouwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba wako wa maisha, shida za ndoa, kuwa na bahati katika maisha haswa katika michezo ya kamari na mengineyo. Ama kwa hakika daktri Kiwanga ni mtu wa kutegemewa katika jamii kwa ajili ya kusuluhisha mambo yanayowakosesha watu mbalimbali usingizi ama maisha bora yenye matamanio. 

 Kwa mahojiano na daktari Kiwanga kwa ajili ya kusuluhisha shida zako, piga simu kwa nambari +254769404965/barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama tembelea wavuti wwww.kiwangadoctors.com kwa mengi zaidi.
Share:

IJA YATOA MAFUNZO KWA MAKATIBU MUHTASI

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo akisisitiza jambo alipokuwa anafungua mafunzo ya siku tano kwa Makatibu Muhtasi 56 yaliyoanza kufanyika.
Sehemu ya Makatibu Muhtasi wanaoshiriki katika mafunzo ikifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mkuu wa Chuo.
Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo (katikati) ikiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote wa mafunzo.

*******************

Na Rosena Suka, Lushoto

Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto leo tarehe 9 Agosti, 2022 amefungua mafunzo ya siku tano kwa Makatibu Mahsusi wapatao 56 wa Mahakama ya Tanzania yanayohusu Namna Bora ya Uendeshaji wa Ofisi.

 Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 09 Agosti ,2022 mpaka 13 Agosti, 2022 katika ukumbi wa Mafunzo uliopo Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Akifungua mafunzo hayo Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo amewataka Makatibu Muhtasi kutoa
huduma bora zinazoendana na uwekezaji katika majengo ya Mahakama nchini. 

 Aliendelea kwa kusema kuwa, Mahakama ya Tanzania iko katika maboresho ambayo yanagusa maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya majengo na raslimali watu hivyo mafunzo haya yanalengo la kuwaandaa watumishi hao ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea.

“Hivyo lengo la mafunzo yanayotolewa ni kujaribu kuwajengea uwezo na kubadilisha
fikra za watumishi wa Mahakama ili huduma wanazozitoa mahakamani ziendane na
ubora wa majengo ambayo yanaendelea kuboreshwa,” amesema.

Mhe. Dkt. Kihwelo aliwasihi watumishi hao kuwa waadilifu na wachapakazi ili kuipa
sifa nzuri Mahakama ya Tanzania kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kuichafua
Mahakama kama matumizi ya lugha mbaya. Pia aliwaomba watumishi hao
watakaporudi kwenye vituo vyao vya kazi ni wajibu kushirikiana na kuonyesha
waliochojifunza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya
Tanzania, Bi. Beatrice Patrick amewaambia washiriki hao kuwa Mahakama
imejipanga kuwajengea uwezo watumishi wake katika kada mbalimbali ili kuendana
na maboresho yanayoendelea.

Bi. Beatrice Patrick amesema kundi hilo la washiriki wa mafunzo linajumuisha
Makatibu Muhtasi 56, ambapo 50 wametoka katika Mahakama mbalimbali za
Mwanzo, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Hakimu Mkazi, washiriki sita
wakiwa ni waajiriwa wapya.

Amesema kuwa watumishi hao wanapewa mafunzo hayo kwa lengo la
kuwakumbusha majukumu yao ya kazi za Ukatibu Muhtasi, utunzaji wa

kumbukumbu, usimamizi wa ofisi na mawasiliano ya kiofisi, uzalendo na protokali,
mipango ya Mahakama na uboreshaji, huduma kwa mteja, masuala ya saikolojia na
ushauri, mwelekeo wa Mahakama kwa sasa katika mapinduzi ya viwanda kuelekea
Mahakama Mtandao na matumizi ya TEHAMA.
Share:

Tuesday, 9 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 10,2022

Magazetini leo Jumatano August 10 2022




























Share:

AFARIKI KWA KUTUMBUKIA KWENYE SUFURIA YA UJI



Picha za CCTV zimeonesha rejeo la tukio

MWANAUME mmoja nchini India aliyefahamika kwa jina la Muthukumar amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye sufuria kubwa lililokuwa limejaa uji wa moto uliokuwa ukiendelea kuchemka jikoni.


Muthukumar alionekana akiwa mmoja wa wapishi wanaolinda masufuria hayo tayari kwa uji huo kunywewa katika tamasha huko Tamil Nadu Madurai nchini India, Julai 29, 2022.



Video ya CCTV iliyorekodi tukio zima, imeonyesha kusambaa ikimuonesha jamaa huyo akiwa amekaa ndani ya sufuria na watu wakimkimbilia kwenda kumuokoa.


Muthukumar alipelekwa hospitali ya Rajaji akiwa na majeruhi asilimia 65 ya mwili wake hali iliyosababisha kifo chake Jumanne, Agosti 2, 2022.


Tamasha la ‘Aadi Velli’ ni tamasha kubwa na muhimu kwa jamii ya Tamil Nadu ambapo uji hupikwa na kugawiwa kwa watu wanaoheshimika wakipewa jina la Goddess Amman.


Haijajulikana mara moja ni nini kilimfanya atumbukie kwenye sufuria hilo, lakini mke wake anasema mume wake alikuwa na kifafa na huenda ndicho kilichosababisha akaangukia kwenye uji huo
Share:

TBS YAKUTANA NA WAZALISHAJI, WAINGIZAJI WA VILAINISHI VYA MAGARI HAPA NCHINI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema (katikati) akiwa kwenye kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema akizungumza kwenye kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema akifungua kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi udhibiti Ubora, Dkt. Candida Shirima akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini wakiwa kwenye kikao na wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam. Waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini wakiwa kwenye kikao na wataalamu kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kikao hicho kimefanyika leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), inawajibika kikamilifu kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini na zile ambazo zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na biddhaa za vilainishi vya magari zinakidhi matakwa ya viwango ili kukuza uchumi wa nchi.

Ameyasema hayo leo Agosti 9,2022 Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu (TBS), Bw.David Ndibalema wakati akifungua kikao cha waingizaji na wazalishaji wa vilainishi vya magari hapa nchini

Amesema kuwa wameandaa mkutano huo mahususi kwa lengo la kukuza uelewa ili kukidhi matakwa ya viwango kwa bidhaa za vilainishi vya magari hususan oili za injini za magari.

"Ni vyema kutambua kuwa ubora wa vilainishi vya magari ni muhimu katika kutunza vyombo hivyo, ikumbukwe kuwa endapo mtumiaji atanunua vilainishi visivyokidhi vigezo vya ubora huweza kusababisha uharibifu wa gari na kutopata thamani ya fedha zilizotumika". Amesema.

Amesema TBS itaendelea kutilia mkazo suala la usimamizi wa viwango na kudhibiti usalama na ubora wa bidhaa ili kuhakikisha zinakidhi vigezo vya usalama na ubora.

Share:

RAIS SAMIA : VETA ITAFUNGUA FURSA KWA WANAMBARALI

Rais Samia Hassan Suluhu akiweka jiwe la Msingi katika Chuo cha VETA Mbarali

Rais Samia Hassan Suluhu akiweka jiwe la Msingi katika Chuo cha VETA Mbarali

Baadhi ya Mawaziri walioko katika Msafara wa Rais Samia Hassan Suluhu.

Wananchi wa Mbarali wakimsikiliza Rais Samia Hassan Suluhu hayupo pichani mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha VETA Mbarali.

***************************

Rais Samia Hassan Suluhu amesema Chuo cha VETA Mbarali kitafungua fursa kwa wanambarali kupata mafunzo ya ufundi Stadi na kwenda kutoa huduma kwa wananchi.

Hayo ameyasema wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mbarali kilichojengwa katika Kijiji cha Mwaganga wilayani humo mkoani Mbeya.

Rais Samia Hassan Suluhu amesema mafundi umeme watapatikana hapo washonaji , mafundi uchomeleaji , watu wa urembo nao watapatikana ni fursa kwa vijana kwenda kusoma chuo hicho.

Amesema Rais Samia Kozi fupi zitaanza septemba na kozi ndefu mwakani ambapo baada ya kukamilika atazindus mwenyewe na kupata muda wa kuongea na wanambarali.

Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya 25 wanufaika wa mradi wa ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi vya Wilaya ulioanza kutekelezwa mwaka wa fedha 2019/2020. Ujenzi wa vyuo hivi ulianza kupitia mradi wa ambapo Serikali ilitenga Shilingi za Kitanzania Bilioni 40, sawa na Shilingi Bilioni 1.6 kwa kila Chuo kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi.

Profesa Mkenda amesema kupitia Mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 Serikali ilitenga tena jumla ya Shilingi bilioni 28.76 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyuo hivyo pamoja na gharama za kutengeneza samani.

Amesema vyuo vya vinajengwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambapo ujenzi wa chuo cha Mbarali unatekelezwa na kusimaiwa kupitia Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma cha Mkoa wa Mbeya (VETA Mbeya).

Aidha, Chuo cha VETA Mbeya pia kinatengeneza samani kwa ajili ya chuo hiki na Chuo cha Ufundi Stadi cha wilaya ya Chunya huku

Amesema chuo hicho kinatarajiwa kuhudumia wakazi wote wa Wilaya hii na maeneo ya jirani na mradi ujenzi wa chuo hicho una jumla ya majengo kumi na saba (17) ambayo ni Jengo la utawala, Karakana 4, Jengo la madarasa, Mabweni mawili Bwalo la chakula, Majengo tatu ya Maliwato, Nyumba ya Mkuu wa Chuo, Nyumba ya familia mbili za watumishi, Jengo la mitambo ya umeme, Jengo la stoo na Jengo la ofisi ya walinzi.

Profesa Mkenda amesema chuo cha mbarali kikikamilika kinatarajiwa kuanza na fani tisa za muda mrefu na mfupi ambapo jumla ya wanafunzi 240 wanatarajiwa kudahiliwa kwa mwaka kati yao wanafunzi 144 watakuwa wa bweni na 96 watakuwa wa kutwa pia Chuo kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wapatao 500 wa kozi za muda mfupi kwa mwaka, hivyo kufanya idadi ya jumla ya wanafunzi wanaodahiliwa kuwa 740 kwa mwaka.

Amesema Fani za muda mrefu na mfupi zitakazotolewa kwa awamu ya kwanza ni Uhazili na Kompyuta, Ubunifu wa Mitindo,Ushonaji na teknolojia na nguo, Uashi Umeme wa Majumbani na viwandani, Ufundi wa Magari,Ufundi wa zana za Kilimo, Uchomeleaji na Uungaji Vyuma, Mafunzo ya Udereva, Ufundi wa kutengeneza pikipiki na pawatila.

Profesa Mkenda amesema mradi ulianza kutekelezwa tarehe 8 Machi, 2020 hadi sasa utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 95 ambapo majengo yote 17 yamekamilika na kubakiwa na kazi za usambazaji wa umeme, maji, barabara na ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua. Ni matarajio ya Mamlaka kuanza kufanya taratibu za usajili wa wanafunzi ifikapo mwezi Septemba, 2022 kwa lengo la kuanza kutoa mafunzo ifikapo Januari, 2023. Aidha, utoaji wa mafunzo ya kozi za muda mfupi zisizohitaji mitambo mikubwa na vifaa yataanza kutolewa mwezi Septemba 2022 kulingana na mahitaji ya Wilaya hii pamoja na shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika eneo hilo.

Amesemaa gharama za ujenzi wa mradi huo awamu ya kwanza Kiasi cha Shilingi 1,600,000,000 (Bilioni moja na milioni mia sita) kilitolewa na Serikali kupitia mradi wa kwa ajili ya kuanza ujenzi na awamu ya pili Serikali ilitoa kiasi cha Shilingi 631,527,204 kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa ajili ya kumalizia ujenzi, na hivyo kufanya Kiasi cha Shilingi 2,231,527,204.00 kuwa kimetolowa na kutumika katika mradi huu.

Utengenezaji wa Samani Samani kwa vyuo vyote 25 zinatengenezwa kwa jumla ya Shilingi Bilioni 8.76 ikiwa ni sehemu ya Shilingi Bilioni 28.76 za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19. Jumla ya samani mbalimbali 39,750 zinatengenezwa kwa ajili ya vyuo 25 vya Wilaya zikihusisha za maofisini, madarasani, karakana, mabweni ya wanafunzi na bwalo la chakula. Utengenezaji umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti 2022.

Hata hivyo amesema utengenezaji wa samani hizo unafanyika katika Kiwanda cha Samani cha VETA kilichopo Mkoani Dodoma na katika Karakana za Vyuo vya VETA vilivyopo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mwanza, Shinyanga, Tabora na Kigoma.
Share:

JINSI NILIVYOMALIZA HARUFU MBAYA KWENYE MWILI WANGU, KILA MARA MUME WANGU ALIKUWA AKILALAMIKA


Ama kwa hakika mwanamke ni mtu anayepaswa kuwa msafi kila mara. Hii ilikuwa tofauti na hali yangu kwani swala la kuwa nadhifu lilikuwa ni ndoto. Kwa jina ni Kathure kutokea kwenye kaunti ya Meru. Nilikuwa kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6 sasa.


Tulikuwa tunaishi kwa furaha na upendo na mume wangu kwani ndoa yetu ilikuwa yenye upendo na kuaminiana kila wakati. Nilimpenda mume wangu ajabu na sikutaka kuwa na ugomvi naye hata kwa wakati mmoja kwani hata tulikuwa tumechumbiana kupitia harusi kubwa iliyofanyika mbela ya umati wa watu kutoka katika familia yake na familia yangu.

Siku ziliposonga, nilianza kukumbwa na shida ambazo kamwe sikuelewa kabisa. Mwili wangu ulikuwa ukitoa jasho jingi lililoandamana na harufu mbaya. Harufu ile ilikuwa mbaya hata zaidi kwani hata nikitumia manukato ama mafuta yenye harufu nzuri harufu ile haikuwa inakwisha. Kila mara nilipokuwa kazini nilishanga kwa nini watu hawakupenda kuka karibu name na kila mara nilipowakaribia marafiki zangu pale kazini walisema kwamba nilikuwa na harufu mbaya isiyokuwa ya kawaida. Mume wangu chumbani pia alikataa kunitimizia swala la ndoa kwani alisema harufu mbaya iliyokuwa ikitoka kwenye mwili wangu ilikuwa inamnyima hamu ya nunitimitizia tendo la ndoa kila siku.

Ama kwa hakika nilijaribu mafuta mengi ya kuimarisha manukato yangu hata baada ya kukoga lakini hakuna suluhisho nililokuwa Napata kwa wakati ule. Kwa mara nyingi nilibakia mtu aliyejitenda kutoka kwa watu wengine kwani kila mara niliogopa wangelalamikia hali yangu ya kutoa harufu mbovu kutoka mwilini mwangu.

Dawa zote za kusitisha harufu ile nilizokuwa nimepewa na baadhi ya watu tajika hazikuwa na umuhimu wowote kwani harufu ile ingali ilikuwa. Hali ile ilipelekea mimi na mume wangu kuwa na mvutano kila mara. Mara nyingi hata aliogopa kulala na mimi kwenye kitanda kimoja kwa kusema kwamba harufu mbaya niliyokuwa natoa ilikuwa inamfanya kutokuwa na hamu name.

Kila mara angelala sebuleni swala ambalo ama kwa hakika lilinikosesha usingizi kwa kila hali. Baada ya kufanya utafiti wangu kwenye mtandao, nilipatana na daktari Kiwanga kutoka kwenye wavuti www.kiwangadoctors.com ambapo daktari huyu wa tiba asilia alikuwa amewasaidia watu kadha kutokana na swala kama langu. Nilimpigia simu na baada ya wiki moja nikawa nimefika afisini pake kupata nafuu. Alinichanganyishia madawa ya asilia na kunipa. Alinipa pia mafuta ambayo alinipa wosia kuwa kila baada ya kutoka maliwatoni niwe nikijipaka kwenye kila sehemu ya mwili wangu. Baaada ya siku tatu, mume wangu alianza kusema kwamba nilikuwa na harufu nzuri na hapo nikajua kwamba dawa za daktari Kiwanga zilikuwa zinafanya kazi. Kazini hakuna yeyote aliyelalamikia harufu yangu mbaya kama hapo kitambo. Mungu akubariki daktari Kiwanga.

Daktari Kiwanga hutibu maradhi kama kifua kikuu, kisukari, msukomo wa damu, kifafa na magonjwa mengineyo. Husuluhisha shida za kifamilia kama kutokouwa na uwezo wa kupata mtoto, kutopata mchumba wako wa maisha, shida za ndoa, kuwa na bahati katika maisha haswa katika michezo ya kamari na mengineyo. Ama kwa hakika daktri Kiwanga ni mtu wa kutegemewa katika jamii kwa ajili ya kusuluhisha mambo yanayowakosesha watu mbalimbali usingizi ama maisha bora yenye matamanio. Kwa mahojiano na daktari Kiwanga kwa ajili ya kusuluhisha shida zako, piga simu kwa nambari +254769404965/barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama tembelea wavuti wwww.kiwangadoctors.com kwa mengi zaidi.
Share:

POLISI SHINYANGA : AJALI YA MAGARI MANNE ILIYOUA NA KUJERUHI MWAKATA NI YA UZEMBE MKUBWA SANA, CHANZO IST NA HIACE

 

Na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog

Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga.

Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Malunde 1 blog kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa nne usiku Jumatatu Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamepoteza maisha na 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

"Watu 17 walipoteza maisha papo hapo eneo la tukio na watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospitali,majeruhi wapo 15", taarifa inaeleza.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Henry Mwaibambe  amesema ajali hiyo iliyotokea Agosti 8,2022 Majira ya saa nne kasoro usiku katika kijiji cha Mwakata kata ya Mwakata wilaya ya Kahama katika barabara kuu ya Isaka – Kahama imehusisha magari manne kugongana na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa vyombo hivyo vya usafiri.


"Ajali ilihusisha gari lenye namba za usajili T880 DUE Toyota IST iliyokuwa inatokea Isaka kuelekea Kahama, iliigonga kwa nyuma trekta yenye namba T719 AUP ikiendeshwa na dereva ambaye hajafahamika na kusababisha vifo vya watu watatu waliokuwa kwenye gari ya IST.

"Wakati huo imeshatokea ajali nyingine eneo hilo hilo kwenye barabara hiyo ambapo ajali ya pili ilihusisha gari la Hiace yenye namba T350 BDX ikiendeshwa na Salinja Lukelele (28) ikitokea Kahama kuelekea Isaka iliigonga kwa mbele gari yenye namba T658 DUW Scania ikiendeshwa na dereva ambaye bado hajapatikana na kusababisha vifo vya watu 13 waliokuwa kwenye hiyo Hiace",amesema Kamanda Mwaibambe.

"Hiyo Scania ilikuwa imepaki na huyo dereva wa Hiace akitokea huko alijua kabisa pale kuna ajali na kuna baadhi ya magari yalikuwa yamesimama lakini yeye akawa anafanya jitihada za kukwepa magari yaliyosimama ili awahi kule anakotaka kwenda matokeo yake akaenda kuivaa hiyo Scania.

“Kwenye hiyo IST waliofariki ni wanaume, uchunguzi wa awali unaonesha hiyo gari ilikuwa kwenye mwendo kasi imeharibika, iliingia chini ya Trekta, huenda dereva alikuwa amelewa kwani tumekuta pombe aina ya Kvant ndani ya gari”, ameongeza Kamanda Mwaibambe.

Amesema Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

“Ukiangalia muktadha wa hii ajali ni ajali ya uzembe mkubwa sana, hili trekta lilibeba kuni nyingi na halikuwa na Reflector, lakini pamoja na kwamba hii trekta haina reflector lakini IST ina taa aliingiaje chini ya trekta, mwenye IST na trekta wote wana makosa.

“Ajali ya pili nayo dereva wa Hiace anajua kabisa kuna ajali na magari yamesimama lakini anatoka mbio kuyapita magari hayo,huyu mwenye Scania aliona gari inayumba yumba kwa speed akapaki yeye akaivaa Scania",amesema.


Amewasisitiza watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia kanuni za usalama barabarani.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger