Wednesday, 9 September 2026

WAANDISHI WA HABARI WAPEWA MAFUNZO YA UBUNIFU UNAOMLENGA MTUMIAJI (HCD) KUKABILIANA NA HABARI POTOFU

...
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kuhusu Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD), Dkt. Hellen Maziku, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanzilishi wa HCD Services Tanzania, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Na Waandishi wetu - Malunde 1 blog

 Waandishi wa habari, wahariri na wataalamu wa masoko na biashara kutoka taasisi 10 za habari nchini Tanzania wamejengewa uwezo wa kukabiliana na taarifa potofu na za upotoshaji kupitia mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (Human-Centred Design - HCD), yanayolenga kuwasaidia kutambua changamoto zinazohusiana na taarifa potofu na kubuni suluhisho zinazozingatia mahitaji, uzoefu na tabia za watumiaji wa taarifa.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 11, 2026, yakiendeshwa na Shirika la International Media Support (IMS) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), JamiiAfrica na Nukta Africa.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen, amesema taarifa sahihi ni jambo nyeti katika jamii kwa kuwa zina nafasi kubwa katika kusaidia wananchi na taasisi kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu.

Dausen ameeleza kuwa, kuenea kwa taarifa potofu kunaweza kuathiri sekta mbalimbali na kuhatarisha ustawi wa jamii, hivyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kuwa na ujuzi na mbinu za kisasa za kubaini na kukabiliana na taarifa hizo.

Ameongeza kuwa, mafunzo hayo yanatoa fursa kwa wadau wa habari kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu za kisasa za kukabiliana na habari potofu katika vyombo vya habari, kwa lengo la kusaidia jamii kupata taarifa sahihi na kufanya maamuzi yenye tija kwa maendeleo yao.

Amesema Mafunzo hayo ni sehemu ya programu ya Maabara ya Fikra Bunifu na Uvumbuzi (Design Thinking and Innovation Lab) inayosimamiwa na IMS na washirika wake, ikiwa na lengo la kuwajengea washiriki uelewa na uwezo wa kutumia kanuni, hatua na mbinu za HCD katika kutambua na kutatua changamoto zinazohusiana na taarifa potofu.

Kwa upande wake, Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, amesema taasisi hiyo inashirikiana na wadau wa habari nchini Tanzania katika kutekeleza mradi unaolenga kukabiliana na misinformation na disinformation, ili kusaidia vyombo vya habari kuwa na mbinu sahihi za kuelimisha jamii na kukabiliana na taarifa zinazoweza kupotosha umma.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa.

Musokwa amesema juhudi hizo ni muhimu katika kuongeza uwezo wa vyombo vya habari kukabiliana na changamoto ya taarifa potofu, hasa katika kipindi ambacho teknolojia za mawasiliano zimefanya taarifa kusambaa kwa kasi kubwa.

Musokwa amesema kuenea kwa taarifa potofu na maudhui ya chuki ni miongoni mwa changamoto zinazozidi kujitokeza duniani, huku ukuaji wa matumizi ya simu janja na upatikanaji mpana wa intaneti, sambamba na viwango vya chini vya uelewa wa mfumo wa taarifa, ukiongeza uwezekano wa kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi na zinazopotosha hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari kuwa mstari wa mbele kulinda jamii ipate taarifa sahihi ili ifanye maamuzi sahihi.

Amebainisha kuwa, hali hiyo inaweza kuleta madhara kwa watu binafsi na jamii kwa ujumla, ikiwemo kuathiri namna wananchi wanavyofanya maamuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayogusa maisha yao.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Dkt. Hellen Maziku, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanzilishi wa HCD Services Tanzania, amesema mafunzo hayo yanasisitiza umuhimu wa kutumia mtazamo unaomlenga mtumiaji katika kutafuta suluhisho la changamoto ya taarifa potofu.

Amesema mtazamo huo unazingatia mahitaji, matarajio, uzoefu na tabia za wananchi wanaokumbwa na changamoto ya taarifa potofu, hatua inayolenga kuhakikisha suluhisho zinazobuniwa zinakidhi mahitaji halisi ya watumiaji wa taarifa.

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kupata uelewa na mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kutambua, kuchambua na kukabiliana na habari potofu na taarifa za upotoshaji katika kazi zao za kila siku.

Wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza umakini katika kuchakata taarifa kabla ya kuzifikisha kwa wananchi, hatua ambayo itachangia kuimarisha uaminifu wa jamii kwa vyombo vya habari na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na zenye manufaa kwa maisha yao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya teknolojia na habari ya Nukta Africa, Nuzulack Dausen akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Programu Meneja wa International Media Support (IMS), Fausta Musokwa, akizungumza wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kuhusu Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD), Dkt. Hellen Maziku, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanzilishi wa HCD Services Tanzania, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kuhusu Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD), Dkt. Hellen Maziku, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanzilishi wa HCD Services Tanzania, akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Malunde Media, Kadama Malunde, akichangia hoja wakati wa mafunzo ya Ubunifu Unaomlenga Mtumiaji (HCD) yanayolenga kuwajengea uwezo wadau wa habari kukabiliana na taarifa potofu, jijini Arusha.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger