Mkuu wa idara Ulinzi na mahusiano Chem chem Charles Sylivester akimkabidhi kadi ya gari Mkurugenzi wa halmshauri ya Babati vijijini ,Anna Mbogo kwa ajili ya kazi za uhifadhi Burunge WMA
Mkurugenzi halmashauri Babati vijijini Anna Mbogo


Mwandishi wetu, Babati
Halmashauri ya Babati vijijini, imetangaza kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wapya katika eneo la Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge,baada ya kukamilika maboresho ya Katiba ili kuifanya hifadhi hiyo kuwa bora barani Afrika.
Burunge WMA ipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Hifadhi ya Taifa ya Manyara , mkoa wa Manyara chini ya usimamizi wa halmashauri ya Babati na Mamlaka ya usimamizi wanyamapori ( TAWA).
Uchaguzi huo unafanyika baada ya kusimamishwa viongozi waliokuwepo madarakani kwa tuhuma kadhaa na baadae kumaliza muda wao.
Akizungumza na waandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi wilayani Babati, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Babati vijijini,Anna Mbogo jana amesema, chaguzi maboresho hayo yanafanyika pia kuendana na dhamira ya Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuongeza mapato ya Taifa kupitia Utalii.
Mbogo anasema tayari maboresho ya Katiba na mfumo wa uendeshaji Burunge WMA umekamilika na sasa chaguzi za viongozi wa jumuiya hiyo, zimeanza katika vijiji 10 vinavyounda jumuiya hiyo.
Anasema vijiji hivyo ni, Mwada.Sangaiwe,Vilima Vitatu,Ngoley,Kakoi,Olasiti ,Manyara,Magara,Maweni
na Minjingu.
"Chaguzi zimeanza tunatarajia zikikamilika tutapa viongozi bora ambao wataweza kuja kusimama Uhifadhi, Utalii na kubwa kuongeza mapato ya Utalii kwa manufaa ya vijiji na serikali kwa ujumla",anasema.
Anasema Rais wa Jamuhuri ya Muungano, Dkt Samia Suluhu Hassan, tayari ilikamilisha kazi ya kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour hivyo, sasa kazi iliyopo ni kuweka mazingira mazuri ya kuvutia watalii katika maene yote yaliyohifadhiwa.
Mkurugenzi huyo anasema, katika eneo la Burunge WMA tayari matunda ya uhifadhi yameanza kuonekana baada ya hivi karibuni, hoteli ya Chem chem iliyopo ndani ya hifadhi hiyo, kushinda tuzo ya Safari Luxury lodge Afrika na Tanzania tuzo zilizotolewa na shirika la Utalii duniani la WTA.
"Tuzo hii inaendelea kuitangaza Burunge WMA vizuri na itavutia watalii zaidi na tunaomba na wawekezaji wengine katika eneo hili kuboresha huduma zao ili kuendelea kuvutia watalii",anasema.
Mbogo amewataka wananchi wenye sifa na nia ya dhati kuendeleza uhifadhi na Utalii katika vijiji hivyo kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Chem chem, Clever Zulu anasema, lengo lao ni kuifanya WMA ya burunge kuwa bora barani Afrika, kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, huduma bora ya malazi na kubwa kuhifadhiwa vizuri.
"Hili ndio lengo kubwa la wakurugenzi wa chem chem Nicolaus Negri na Fabia Bausch kuifanya Burunge WMA kuwa bora na ushindi wa tuzo ni sehemu ya mikakati lakini pia sasa tumeanza kupokea maafisa wa uhifadhi maeneo kadhaa Afrika kuja kujifunza hapa",anasema.
Anasema hifadhi hiyo, kwa sasa wanyama wameongezeka, ujangili umedhibitiwa na wananchi wananufaika sana na uhifadhi kupitia fedha zinazokusanywa.
Spika wa Burunge WMA, Erick Lilayoni ambaye anamaliza muda wake, anasema mapato ya Burunge WMA yamekuwa yakiongezeka hadi kufikia takriban billion 4 kwa mwaka na vijiji vimekuwa vikipata mgao zaidi ya millioni 200 kwa mwaka.
"Binafsi sitarajii kugombea tena uongozi lakini naamini eneo hili tukilitunza vizuri, manufaa makubwa yataendelea kupatikana kwa wananchi wa vijiji 10 na serikali kwa ujumla",anasema.


0 comments:
Post a Comment