Friday, 11 September 2026

SHEIKH WA DODOMA ATOA AGIZO LA DUA MAALUMU MISIKITINI

...


Na Mwandishi wetu, Dodoma

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Dodoma limewaagiza Masheikh na Maimamu wote wa misikiti mkoani humo kufanya dua maalumu kwa ajili ya kuombea taifa na kuendelea kuomba mvua, kutokana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayotarajiwa.

Agizo hilo limetolewa leo Septemba 11,2026 na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Alhaji Dkt. Mustafa Rajabu Shabani, ambaye amewataka Masheikh na Maimamu wote wa misikiti mkoani Dodoma kutekeleza dua hizo kuanzia Ijumaa, Septemba 11, 2026, baada ya Swala ya Ijumaa na kuendelea.

Sheikh Dkt. Shabani,amesema dua hiyo ina mambo mawili muhimu, ikiwemo kumuombea Marehemu Mzee Hafidh Ameir Mume, aliyekuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema ni muhimu kwa viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu kumuombea marehemu huyo, huku akiwataka Masheikh na Maimamu kuhakikisha dua hiyo inafanyika katika misikiti mbalimbali mkoani Dodoma.

Aidha, Sheikh Dkt. Shabani ametoa agizo la kufanyika kwa dua endelevu ya kuliombea taifa kupukana na janga la mvua za El-Nino, ambazo zinatajwa kuwa na uwezekano wa kuleta athari kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema dua hiyo inapaswa kuendelea kufanyika kwa mujibu wa mamlaka za hali ya hewa na taarifa zinazotolewa kuhusu mwenendo wa hali ya hewa nchini.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger