Sunday, 20 September 2026

CCM KISHAPU YASIKILIZA KERO ZA WAFUGAJI MWAMALASA YAAHIDI SERIKALI KUZITATUA

...

Na Sumai Salum-Kishapu

Wananchi na wafugaji wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo, huku wakiiomba Serikali kuongeza matanki ya kuhifadhi maji na kuchimba visima.

Akizungumza katika kikao cha viongozi wa CCM Wilaya ya Kishapu kilichofika katika kata hiyo leo Septemba 20, 2026, Matu Kidai amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za kijamii, akitaja ujenzi na uboreshaji wa barabara pamoja na kufikishwa kwa umeme katika maeneo ya wananchi.

Naye Katibu wa Kikundi cha Wafugaji Miyuguyu, Majeshi Buyaye, amesema maji yanayopatikana kupitia matanki yaliyopo hayatoshi mahitaji ya wananchi na mifugo, hivyo ameomba kuongezwa kwa matanki pamoja na kuchimbwa kwa visima ili kuongeza upatikanaji wa maji.

Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mwamalasa, Makoye Kachemba amepongeza juhudi za viongozi wa CCM na Serikali kufika katika kata hiyo kusikiliza changamoto za wananchi, akisema hatua hiyo imeongeza matumaini ya kero zao kufanyiwa kazi.


Kachemba amesema Mwamalasa iko umbali wa zaidi ya kilomita 70 kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu, hivyo kufika kwa viongozi katika eneo hilo ni hatua inayowaonesha wananchi kuwa changamoto zao zinaendelea kusikilizwa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Shija Malisha Ntelezu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani humo cha kusikiliza kero zinazowakabili wafugaji wa Kata ya Mwamalasa Septemba 20, 2026


Amesema wananchi wanaendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Sita kutokana na miradi iliyotekelezwa katika maeneo yao, ikiwemo barabara na kusambazwa kwa umeme katika vitongoji, huku akitarajia changamoto zilizowasilishwa katika kikao hicho kuendelea kufanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mwamalasa, Mhe. Bushi Mpina, amesema tayari amefuatilia changamoto ya maji kwa kufika kwa Mhandisi wa Maji Dodoma, ambapo wataalamu walifika katika eneo hilo na kufanya usanifu wa mradi.

Amesema kinachosubiriwa ni kukamilika kwa taratibu za Serikali ili utekelezaji uweze kuanza. Kuhusu mabwawa ya kunyweshea mifugo, Mhe. Bushi amesema Halmashauri imekusudia kuyajenga kupitia mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.


Aidha, amesema suala la kilimo cha umwagiliaji limejadiliwa katika vikao vya madiwani na Kata ya Mwamalasa imepewa kipaumbele katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuendeleza shughuli hiyo.Katimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Regina Ndulu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani humo cha kusikiliza kero zinazowakabili wafugaji wa Kata ya Mwamalasa Septemba 20, 2026



Akizungumza kwenye mkutano huo, Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu, Regina Ndulu, amewataka kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na El Niño, huku akiwahimiza kujenga nyumba imara na kuimarisha miundombinu iliyopo kulingana na uwezo wao.


Ndulu pia amewataka wananchi kuanza kuweka miundombinu ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua, akisema hatua hiyo inaweza kusaidia kukabiliana na changamoto ya maji wakati wakisubiri Serikali na wadau mbalimbali kuendelea kuboresha miundombinu ya maji. TMA imeeleza kuwa msimu wa Vuli 2026 unatarajiwa kuathiriwa na El Niño na imewashauri wadau, miongoni mwa hatua nyingine, kuvuna maji ya mvua na kuimarisha miundombinu.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Shija Malisha Ntelezu, amewahimiza wananchi kudumisha umoja na mshikamano, akiwataka pia kutafuta na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo yao.


Shija amesema wananchi wanaweza kujiunga na kuunda vikundi vya kiuchumi ili kuwa na uwezo wa kunufaika na mikopo mbalimbali ya Serikali, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Katibu Mwenyezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Seleli Jiyenze akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani humo cha kusikiliza kero zinazowakabili wafugaji wa Kata ya Mwamalasa Septemba 20, 2026


Amesema ushirikiano miongoni mwa wananchi ni muhimu katika kutatua changamoto zinazowakabili, huku akiwataka kutumia fursa hizo kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji badala ya kusubiri msaada pekee.


Halmashauri ya Kishapu tayari imeijumuisha Kata ya Mwamalasa katika kata 10 zitakazonufaika na Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya SCALE. Vipaumbele vilivyotokana na mahitaji ya wananchi ni pamoja na malambo, visima virefu, miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua na mitaro ya umwagiliaji.
Diwani wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Bushi Mpina akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani humo cha kusikiliza kero zinazowakabili wafugaji wa Kata hiyo Septemba 20, 2026
Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mwamalasa, Makoye Kachemba akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi CCM wilayani humo cha kusikiliza kero zinazowakabili wafugaji wa Kata hiyo Septemba 20, 2026

Katibu wa Kikundi cha Wafugaji Miyuguyu, Kijiji cha Magalata Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akizungumza kwenye mkutano huo Septemba 20,2026 Majeshi Buyaye
Katibu wa Kikundi cha Wafugaji Manyerere Kijiji cha Magalata Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Matu Kidai akizungumza kwenye mkutano huo Septemba 20,2026





































Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger