Wednesday, 10 August 2022

RC CHALAMILA AWATAKA WATUMISHI KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KWA MAENDELEO YA MKOA WA KAGERA

...
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Albert Chalamila amewataka watumishi kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.

Akizungumza na vyombo vya habari katika kikao kikao cha Mkuu wa Mkoa na watumishi kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa tarehe 9 Agosti 2022, amewataka watumishi na viongozi wote kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha Mkoa unapata maendeleo kupitia umoja wao.

"Viongozi mnapotofautiana na mmoja wapo kumchongea maneno ya uzushi mwingine kwa mkubwa wao ujue yeye ndiye mwenye tatizo maana zipo ajenda nyingi za kuzungumza kama shule, afya, maji na barabara na si kumsema mwenzako. Kaeni kwa pamoja na zungumzeni kwa pamoja ili muwe na malengo ya pamoja" ,amesema Mh. Chalamila.

Ameongeza kuwa yote hayo ni kuepusha migogoro maana hakuna migogoro yenye visababishi viwili, siku zote migogoro mingi kisababishi ni kimoja lazima kuna mmoja ndiye sababu ya mgogoro.

"Na mimi Mkuu wa Mkoa sipendi kusikia hivyo napenda kusikia Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani na Mameya mko pamoja na kama kuna jambo linashindikana tunalirekebisha kwa njia za kitumishi zinazoeleweka", amesema Mh. Chalamila.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger