Thursday, 18 August 2022

DEREVA WA DALADALA MBARONI TUHUMA ZA KUUA KONDAKTA 'MPENZI WAKE'

...
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Maarifa Matala mwenye umri wa miaka 45, ambaye ni dereva wa daladala na mkazi wa Kimara kwa tuhuma za mauaji ya mtu aliyedaiwa kuwa mpenzi wake ambaye alikuwa ni kondakta.


Akizungumza Agosti 17, 2022, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kutoroka na kukimbilia mkoani Lindi akidaiwa kumuua mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Sharifa ambaye alikuwa ni kondakta.


Aidha Muliro ameeleza kuwa katika hatua nyingine wamemkamata Gama Swai, anayetuhumiwa kwa kuuza spea za magari zinazodhaniwa kuwa vifaa vilivyoibwa kwenye magari ya wananchi.

Via >EATV
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger