Monday, 22 August 2022

TBS YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUSAJILI BIDHAA ZA CHAKULA NA VIPODOZI

...
Kaimu Meneja Usajili wa Bidhaa na Majengo TBS, Bi.Gwantwa Mwakipesile akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti22,2022 katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bi.Mbumi Mwampeta akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti22,2022 katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Jijini Dar es Salaam.

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kuwakumbusha wazalishaji,wasambazaji na wauzaji wa bidhaa kuhakikisha wanasajili bidhaa zao za chakula na vipodozi na majengo ili kuweza kumlinda mtumiaji.

TBS imekuwa inafanya usajili wa bidhaa za chakula na vipodozi na majengo yanayofanyiwa usajili ni majengo ambayo yanajihusisha na biashara za bidhaa za chakula na vipodozi.

Akizungumza leo Agosti 22,2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Usajili wa Bidhaa na Majengo TBS, Bi.Gwantwa Mwakipesile amesema lengo la kufanya usajili wa bidhaa na majengo ni kujiridhisha kabla ya kuruhusu majengo kutumika kuhifadhi bidhaa za vipodozi na chakula kwamba yanakidhi vigezo vilivyowekwa ambavyo vitafanya bidhaa zinazotunzwa kwenye majengo hayo ziendelee kuwa bora na salama kwaajili ya matumzi.

Amesema usajili wa vyakula unafanyika kabla ya vyakula havijaruhusiwa kuingia nchini na kuuzwa ili kujiridhisha kwamba bidhaa hizo zinakidhi viwango na vigezo mbalimbali vya usalama na ubora vilivyowekwa kabla ya bidhaa hizo hazijaruhusiwa kuuzwa kwaajili ya matumizi ya binadamu.

"Katika usajili wa bidhaa, yapo mahitaji tofautitofauti kulingana na aina ya bidhaa zinazosajiliwa. Suala hili la usajili linafanyika kwa mujibu wa sheria ya viwango ambapo pia zipo kanuni zilizotungwa chini ya sheria hiyo na kanuni moja wapo ipo kanuni ambayo inahusika na mambo ya import regestration na product registration ambayo yenyewe inapatikana kwenye tovuti ya TBS". Amesema Bi.Mwakipesile

Aidha amesema katika usajili mambo makubwa ambayo Shirika linaangalia ni suala zima la vifungashio vinavyotumika kuhifadhi bidhaa hizo za chakula na vipodozi lakini pia wanaangalia usalama na ubora wa viambato na vikolezo vilivyotumika katika kutengeneza bidhaa hizo na vilevile pia wanaangalia taarifa zilizopo kwenye lebo ya bidhaa.

"Taarifa zinazowekwa kwenye lebo ni aina ya mawasiliano kutoka kwa mtengenezaji wa bidhaa kwenda kwa mtumiaji kumpa taarifa kwamba hii bidhaa unayotaka kuitumia au bidhaa niliyoitengeneza ina vitu mbalimbali kama jina na matumizi". Amesema

Nae Afisa Udhibiti Ubora TBS, Bi.Mbumi Mwampeta amesema mara baada ya mfanyabiashara kusajili bidhaa yake ya Vipodozi atapatiwa Cheti na atatakiwa kuhuwisha Cheti hicho kila baada ya miaka Mitano (5) hivyo amewaomba wafanyabiashara wote wa Vipodozi nchini kutembelea tovuti ya TBS kwa kuanza taratibu za usajili maana ni takwa la kisheria.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger