Mwanamume mmoja ameungua moto hadi kuaga dunia nyumbani kwake katika Kaunti ya Busia nchini Kenya baada ya kurejea akiwa mlevi.
Moto unasemekana kuanza baada ya mwanaume huyo kwa jina George Otieno kuwasha sigara kisha kushikwa na usingizi.
Moto huo ulisambaa katika nyumbani lakini Otieno alikuwa bado mlevi na alishindwa kuutoroka wakati alipogutuka usingizini.
Monicah Oteno, mama wa mwanaume huyo aliyekuwa mfugaji, amebaki na machungu kwa kumpoteza mwanawe aliyekuwa na umri wa miaka 33.
0 comments:
Post a Comment