Sunday, 28 August 2022

TAIFA STARS ILIVYOJIANDAA KUIVURUGA UGANDA JIONI HII

...



KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Uganda utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.


Mchezo huo wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni.


Akizungumza na Spoti Xtra, Poulsen alisema wanatambua Uganda ni moja ya timu ngumu inayohitaji umakini kwenye kupambana nao.

“Uganda tunawatambua hasa kwa namna ambavyo wanatumia nguvu kutafuta ushindi, utakuwa ni mchezo ambao unahitaji nguvu na akili kubwa kwenye kutafuta ushindi ila tupo tayari, muunganiko unazidi kuwa imara.


“Kiakili na mbinu tumejipanga ukizingatia wachezaji wametoka kucheza mechi za ligi, hiyo inaongeza uimara, mchezo huu wa Uganda ni wa kwanza na mchezo wa pili ugenini utatupa picha ya sisi kufuzu CHAN ukichanganya na nguvu ya mashabiki basi kutakuwa na kitu cha kipekee,” alisema Poulsen.


Aishi Manula, Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars, alisema: “Wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda, ambacho tunahitaji ni kufuzu CHAN, benchi la ufundi limefanya kazi kubwa na tunawatambua Uganda na wao wanatujua pia.”
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger