Friday, 6 August 2021

Partnership Officer at SIL International Tanzania

About SIL Tanzania SIL Tanzania, a branch of SIL International, is a registered Society in Tanzania, whose vision is to see people flourishing in community, using the languages they value most. As a faith-based organisation we partner with many churches and community organisations to help communities to translate the Bible, develop their languages, and achieve […]

This post Partnership Officer at SIL International Tanzania has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Phamacist at International Rescue Committee (IRC)

Phamacist     Job Title: Phamacist Sector: Health Employment Category: Fixed Term Employment Type: Full-Time Open to Expatriates: No Location: Kibondo, Tanzania Job Description ORGANIZATIONAL DESCRIPTION: The International Rescue Committee (IRC) is one of the largest humanitarian agencies in the world, providing relief, rehabilitation, and post-conflict reconstruction support to victims of oppression and violent conflict. IRC […]

This post Phamacist at International Rescue Committee (IRC) has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Protection Team Leader at Danish Refugee Council

Job title: Protection Team Leader (CBP) Employment Category: Grade D, level 6 Reporting to: Protection Manager Technical line manager: Protection Manager Direct reports: Protection Officer, Protection Assistant Unit/Department: Protection Location: Kibondo (Nduta/Mtendeli) The overall purpose of the role: The Protection Team Leader is responsible for the overall management and implementation of activities of the DRC protection program. […]

This post Protection Team Leader at Danish Refugee Council has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Livelihoods Interns – Energy and Environment at Danish Refugee Council

Name of the Position: – Livelihoods Interns – Energy and Environment Reports to: – Livelihoods Officer Supervise: – Incentive staffs and Village Agents. Duty Station: – Kibondo and Kasulu Introduction Danish Refugee Council (DRC) is an international non-governmental organization that provides assistance and promotes durable solutions for refugees and internally displaced people, based on humanitarian principles […]

This post Livelihoods Interns – Energy and Environment at Danish Refugee Council has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 6,2021













Share:

Thursday, 5 August 2021

Nafasi Mpya za Kazi: Field Officers( Nafasi 100), Administrative Officers( Nafasi 10), Project Coordinator ( Nafasi 10) na Nyingine Nyingi

Kama unatafuta kazi kwa muda mrefu bila mafanikio, basi hii ni nafasi yako!! Hapa kuna  Nafasi za kazi zaidi ya 300 zilizotangazwa wiki .
 
Chagua unayoitaka hapo chini

_________

 1.Field Officers- Nafasi 100 <<Bofya Hapa>>

2.Administrative Officers.- Nafasi 10<<Bofya Hapa>>

3.Monitoring & Evaluation Officers.- Nafasi 10  <<Bofya Hapa>>

4.Project Coordinator .-Nafasi 10 <<Bofya Hapa>>

5.Procurement, Logistics And Administrative Officer-Food Hunger  . <<Bofya Hapa>>


6.Project Coordinator -Food Hunger.
<<Bofya Hapa>>

7.Administrative Associate.-FoodHunger...<<Bofya Hapa>>

____________

BOFYA HAPA KWA NAFASI ZAIDI ZA KAZI



Share:

Wanafunzi Watatu Shule Ya Msingi Wauawa Baada Ya Kushambuliwa Na Simba

 Wanafunzi watatu katika Shule ya Msingi Ngoile wanaoishi Kijiji cha Ngoile wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wamefariki dunia baada ya kuliwa na Simba.

Akizungumza tukio hilo leo Agosti 5,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema watoto hao wameuwa Agosti 3 mwaka huu na amewataja wanafunzi hao ni Olobiko Metui(10),Ndaskoi Sangu(9) na Sanka Saning'o( 10) ambao wote ni wanafunzi wa darasa la tatu



Share:

Mama Auwa Na Mumewe Kwa Kushirikiana Na Watoto Wake Wakiume


Na Lucas Raphael,Tabora 

JESHI LA polisi mkoani Tabora linawashikilia watu watatu wakiwemo mume na watoto wake wawili kwa kula njama za kuumua mama yao na mume kuumua mkewe       aliyetambulika kwa ajina la Maria Kishiwa baada ya mwanamke huyo kuungua maradhi kwa muda mrefu waliona kero hivyo wakalazimaka kummalizaia mbali mama huyo .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Tabora Safia Jongo alisema kwamba tukio hilo lilitokea agasti 3 mwaka huu  Asubuhi katika kijiji cha Isalalo kata ya Utwigu wilaya ya Nzega mkoani hapa .

Alisema kwamba chanzo ni kuugua maradhi kwa muda mrefu na mbinu iliyotumika ni kumfanga kamba shingoni na kumninginiza ili aonekane kuwa amejinyonga.

Alisema kwamba Maria alikuwa amefariki akiwa amefungwa kamba shingoni huku akininginia na kamba ikiwa imefungwa kwa kukazwa kwenye nguzo ya jiko kitu ambacho marehemu hakuwa na nguvu kiasi hicho baada ya kuugua kwa muda mrefu

Hata hivyo kamanda huyo wa polisi  alisema kwamba baada ya kumninginiza marehemu waliacha kinu na kigoda bila kuanguka chini ili kuonyesha kuwa ndipo alipopanda na kujinyoga .

 “Wakati ni vigumu kwa mtu mgonjwa kupanda hadi kuwe na masada wa watu wengine jambo ambalo lilileta mashaka “ alisema kamanda Safia .

Alisema kwamba marehemu Maria alikuwa analala na mjukuu wake ambaye alifichwa ili asibaini mbinu hiyo ya mauaji jambo hilo ndilo lilipelekea polisi kuanza kuchuguzi ambapo mjukuu huyo alisema kila kitu kilichofanyika kumuua bibi yake.

Alisema kwamba majina ya watu hao watatu yamehifadhi kwa ajili ya uchuguzi mzima wa tukio hilo la kinyama

Hili nituo la pili kutokea katika wilaya ya nzega kwa muda wa usiozidi wiki Tatu baada ya watoto wawili wakiwa wanachunga mifugo kuuawa na kufukiwa kwenye shimo ili kupoteza ushaidi.



Share:

Nchi Za Kiafrika Kupeleka Agenda Ya Maendeleo Ya Kidigitali Benki Ya Dunia Na IMF

 


Na Benny Mwaipaja, Bujumbura
Mawaziri wa Fedha na Uchumi na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi 54 barani Afrika ikiwemo Tanzania, wamekutana mjini Bujumbura nchini Burundi katika Mkutano wa 58 wa Afrika ili kujadili namna ya kulishawishi Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, kuziwezesha nchi za Afrika kujenga miundombuni ya kidijitali ili kukuza uchumi wa nchi hizo baada ya changamoto ya ugongwa wa Uviko-19.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaofanyika katika Jengo la Bunge la nchi ya Burundi (Kigobe) na kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Mheshimiwa Generali Evariste Ndayishimiye, unaongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Frolens Luoga.

Lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kuzishawishi taasisi za fedha za kimataifa ikiwemo Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia kuziwezesha nchi za Afrika kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia hususan katika suala la biashara ya mtandao, uchumi wa kidigitali na ujenzi wa  miundombuni ya kidijitali ili kuweza kuifikia sehemu kubwa ya wanachi mijini na vijijini.

Mkutano huo ambao umebebwa na dhima isemayo “umuhimu wa mifumo ya kidigitali katika kukuza uchumi shirikishi na endelevu” (digitalization for inclusive recovery and sustainable growth) ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2021.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Yussuf Masauni alisema kuwa wakati wa kilele cha Mkutano huo, Magavana hao wa IMF na Benki ya Dunia, wanatarajia kuweka msimamo wa pamoja juu ya vipaumbele vya Bara la Afrika na  namna taasisi hizo za kimataifa zinaweza kusaidia nchi hizo kupata rasilimali fedha za kuwekeza katika miundombinu ya kidigitali, mifumo na sera rafiki zitakazowezesha wananchi kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia za kidijitali katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Alisema kuwa kizazi kilichoelimika kuhusu matumizi ya kidigitali, kinachangia maendeleo na kubuni nyenzo zinazosaidia kutekeleza kazi za ubunifu zitakazosaidia kukuza ajira na kuboresha maisha ya wananchi.

Alizungumzia pia suala la umuhimu wa kufua umeme kutokana na vyanzo vya gharama nafuu kama maji na gesi asilia pamoja na kuhakikisha kuwa huduma hiyo ya umeme inawafikia wananchi wengi ili uwezeshe upatikanaji wa huduma za kidigitali. Mheshimiwa Masauni pia alisema kuwa, kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo ya umeme na miundombinu ya kidigitali, robo tatu ya wakazi bilioni 1.3 Barani Afrika hawatumii Intaneti jambo linalokwaza wananchi kutumia fursa za kidijitali katika kuendesha maisha yao hususan katika kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Uviko-19.

Mhandisi Masauni alifafanua kuwa hivi karibuni Benki ya Dunia imekubali kuipatia Tanzania mkopo nafuu wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma za mtandao wa intaneti kupitia mkongo wa taifa kwa ajili ya matumizi ya Serikali, sekta ya biashara na wananchi na kwamba watatumia maazimio hayo kuiomba Benki ya Dunia iongeze kiwango cha fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huo pamoja na kuboresha miundombinu ya umeme ambayo ni muhimu katika kutekeleza miradi ya kidigitali kupitia madirisha ya IDA 19 na IDA 20.

“Tumelenga kwamba ifikapo mwaka 2025 tuwe tumefikisha mtandao wa intaneti kwa zaidi ya asilimia 80 kwa watanzania wote na kuhakikisha sekta hiyo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inachangia pato la Taifa kwa asilimia 3 badala ya asilimia 1.5 za sasa” alifafanua Mhandisi Masauni.

Alisema kuwa Mambo yaliyojadiliwa kutokana na mawasilisho kutoka kwa wataalam mbalimbali yamegusa maeneo ambayo nchi za kiafrika zikiyafanyiakazi yatachangia Bara la Afrika kukuza uchumi wake na kuondokana na umasikini.

Mkutano huo wa 58 wa Magavana wa IMF na Benki ya Dunia unaofanyika Bujumbura Burundi ambapo kutokana na hali ya janga la UVIKO 19, baadhi ya nchi zilihudhuria na nyingine hazikuweza na hivyo kushiriki kwa njia ya mtandao, umehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayeshghulikia masuala ya Fedha za Nje Bi. Amina Khamis Shaaban na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango- Zanzibar Bw. Aboud Hassan Mwinyi.

Mwisho


Share:

PICHA: Wafuasi Chadema wakamatwa Kisutu

Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Wafuasi  hao waliokuwa wamefika kwaajili ya kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye hata hivyo hakufikishwa mahakamani walikamatwa baada ya kutoa mabango yenye jumbe mbalimbali na kuanza kuimba.

Baada ya wanachama hao kuanzisha nyimbo hizo, Polisi waliokuwa ndani ya magari wakiwa na silaha mbalimbali waliteremka na kuanza kuwakamata.

Kesi hiyo inayomkabili Mbowe na wenzake, ilikuwa inasikilizwa mahakamani hapo kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’, mbele ya Haki Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini baadae iliahirishwa  hadi kesho kutokana na tatizo la mtandao.



Share:

Deputy Vice-Chancellor For Planning, Finance and Administration at SUZA

 Deputy Vice-Chancellor For Planning, Finance and Administration   The Council of State University of Zanzibar seeks to recruit two Deputy Vice-Chancellors (Academic, Research and Consultancy and Planning, Finance and Administration) from suitably qualified and competent Zanzibaris with excellent credentials. The Deputy Vice- Chancellors shall work under the directive of the Vice-Chancellor of the University. Qualifications […]

This post Deputy Vice-Chancellor For Planning, Finance and Administration at SUZA has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

MAWAZIRI WA FEDHA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIRADI


Na. Saidina Msangi na Sandra Charles, WFM, Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, wamekubaliana kutatua changamoto za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kukuza uchumi wa Taifa.

Mawaziri hao wamekutana jijini Dodoma katika kikao kazi kilicholenga kuangalia masuala yaliyokuwa na changamoto wakati wa bunge la bajeti na Sheria ya Bajeti pamoja na masuala yanayohusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kikao hicho kimekuwa cha mafanikio ambapo mengi yamefikia hatua nzuri na kuongeza wigo wa ushirikishwaji hasa katika kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mipya ya kipaumbele iliyoko katika Bajeti Kuu ya Serikali.

“Katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo tunaangalia uwezeshaji na utekelezaji wa miradi inayoendelea na miradi mipya, na mengi tuliyojadili tumefikia hatua nzuri,” alisema Dkt. Nchemba.

Waziri Nchemba aliwaagiza wataalamu wa pande zote kuendelea kufanyia kazi maeneo ya changamoto yaliyosalia ikiwemo uboreshaji wa Sheria ya Usajili wa Vyombo vya Moto.

“Niwasihi msiishie kwenye Sheria ya Vyombo vya Moto ila muangalie na waendeshaji wa vyombo vya moto haipendezi mtu kuwa na leseni mbili wakati nchi ni moja”, alisisitiza Dkt. Nchemba.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali, alisema kuwa kikao kati yake na mwenzake Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kimetoa njia ya namna ya kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo hususani za miradi.

Alisema kuwa wamejadili namna ya kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati iliyopo upande wa Zanzibar, jambo ambalo lina tija kwa wananchi wa Zanzibar.

“Hili ni jambo muhimu tunashukuru uwepo wa kikao hiki ambacho kinatoa mwanga wa namna miradi ya kimkakati Zanzibar itatekelezwa na uwezeshaji wake,” alisema Mhe. Jamal Kassim Ali.

Aidha ameushukuru uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango upande wa bara kwa kikao hicho na kueleza kuwa kikao hicho ni vema kikawepo angalau kila baada ya miezi miwili ili kuona mambo mapya yatakayoibuka yanatatuliwa na kufanya ufuatiliaji wa makubaliano yaliyopita jambo ambalo lililidhiwa na pande zote.


Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA



Share:

TATIZO LA MTANDAO LAKWAMISHA KESI YA MBOWE, YAAHIRISHWA MPAKA KESHO

Kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, imeahirishwa hadi kesho Agosti 6, 2021, kutokana na muonekano hafifu wa video conference, kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo huo, ambapo kesho atafikishwa mahakamani majira ya saa 3:00 asubuhi.


Kesi hiyo ya ugaidi ilikuwa itajwe leo Agosti 5, 2021, ambapo Mbowe na wenzake walikuwa katika Gereza la Ukonga Dar es Salaam lakini kutokana na matatizo ya mtandao ilishindwa kuendeshwa vizuri.

Akizungumza hii leo mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala, amesema kuwa, "Teknolojia imefeli hivyo tumeshindwa kufanikisha mchakato huo kwa sababu kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya video conference facility za hapa katika Mahakama ya Kisutu na Gereza la Ukonga na tumekubaliana kwamba kesho washtakiwa waletwe mahakamani".


Share:

BABA NA MTOTO WAMUUA MAMA BAADA YA KUCHOKA KUMUUGUZA TABORA

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 57 mkazi wa kata ya Puge wilaya ya Nzega mkoani Tabora ameuawa na kisha kuning'inizwa kwenye kamba ili aonekane amejinyonga.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora ACP Sophia Jongo amesema tukio hilo limetokea Agosti 4, 2021 katika kijiji cha Isalalo tarafa ya Puge ambapo baba na mtoto wake walimuua na kutengeneza tukio la kujinyonga.

Share:

DC MSANDO AWATAKA WAFANYABIASHARA KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA...."SASA HAKUNA MUDA WA KUBEMBELEZANA"

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando

Na Jackline Lolah Minja Morogoro.
Wafanyabiashara mkoani Morogoro wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na serikali za namna ya ufanyaji biashara katika maeneo ya manispaa ili kuufanya mji kuwa safi.

Akizungumza na wafanyabiashara hao leo Alhamis Agosti 5,2021 katika Soko kuu la Kingalu ,Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema kwa sasa hakuna muda wa kubembelezana katika kufuata utaratibu hivyo kama hutaki kufuata utaratibu ni vyema ukawapisha ambao wanaweza kufuata utaratibu.

“Na niliwaahidi hata kama zoezi hili litachukua muda mrefu lazima tuhakikishe wamachinga wote wanakaa sehemu anabyo ni sahihi hivyo kwa mara ya mwisho, tufuate utaratibu ambao tutawekeana hapa ,kama unadhani utabembelezwa sahau,kama unadhani utalialia kwamba kuna TV au Redio itakuonyesha unalialia na utahurumiwa sahau,heshimu wamachinga wenzako wanaopambana kutafuta maisha kama unayotafuta wewe hivyo usiwaharibie wenzako wanaohitaji kufuata utaratibu ,usijione wewe unafaa zaidi wenzako wakae sokoni juu wewe ushuke uje ufanye biashara hapa chini au uweke katikati ya barabara”, amesema .

Hivyo Msando amesema ataanzisha zoezi la kuhakiki mitaa ili kubaini wafanyabiashara ambao wamejiorodhesha ni sahihi na watatoa sababu kwa mitaa ambayo haitakuwepo kwenye orodha.

“Sasa basi kwa zaidi ya wiki tatu nilielekeza kuandikwa kwa majina ya wamachinga wote wanaofanya biashara katika mitaa ambapo hadi Jana Agosti 4 2021 saa kumi na mbili jioni wamachinga waliojiandiskisha ni 1312 ikiwemo viongozi 35 na sitapitia majina moja moja lakini nitataja mitaa ili kabla ya kwenda mbali tukubaliane kwa pamoja kwamba mitaa iliyoandikwa ni yote na tutatoa sababu kwamitaa iliyoachwa ,kwa kuwa sehemu zitakazotolewa kwaajili ya biashara zitatolewa kufuatana na majina yaliyoandikwa”, ameongeza.



Share:

SALUNI INAYOTEMBEA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM


Gari maalum iliyozinduliwa yenye ubora na vifaa vyote vya Saluni za kike na kiume ambalo litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wateja wake.
 ***
KATIKA kuweza kuwaepusha wateja wao na changamoto ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona, Kampuni ya J&R Mtita Unisex inayojishughulisha na huduma za Saluni imezindua gari mahususi litakalokua linawafuata wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma hiyo.

Gari hilo lenye ubora na vifaa vyote vya Saluni za kike na kiume litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wateja wake lengo likiwa kupunguza msongamano wa wateja wanaofika kwenye Saluni zao kupata huduma lakini pia kuwahudumia wateja ambao wanakosa muda wa kwenda Saluni.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa gari hilo, Mgeni rasmi katika tukio hilo, Mtangazaji na Mchungaji maarufu jijini Dar , Haris Kapiga amesifu ubunifu uliooneshwa na Kampuni hiyo ya kizalendo akisema ni mfano wa kuigwa na utawasaidia katika pia Kupambana na ushindani wa kibiashara.

"Huu ni ubunifu mkubwa ambao inabidi vijana hawa wapongezwe, katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona kuna watu wanaogopa kuja Saluni kwa sababu za kiafya hivyo uwepo wa gari hili litakalokuwa linazunguka maeneo mbalimbali litakua msaada kwao.

Na siyo tu kupambana na Corona lakini pia wapo wafanyakazi wa maofisini ambao wapo bize na hawana muda wa kwenda Saluni sasa uwepo wa gari hili kwao ni faida kwani watafuatwa walipo na kupewa huduma, vivyo hivyo na kwa wanafunzi hasa wanaoishi bweni," amesema Kapiga.

Kwa upande wake Meneja wa J&R Unisex, Suleiman Muhina amesema huduma zao ni nafuu licha ya kwamba wao ndio wanaowafuata wateja na kwamba ndani ya gari hilo huduma zote zitolewazo Saluni zitapatikana kwa Wanawake na Wanaume.

Nae Operesheni Meneja wa J&R, Belina Mlokozi amesema licha ya kufanya huduma zote za kike na kiume pia wanapamba na kuremba maharusi huku akisema kunakuepo na punguzo la bei kwa wale wanaotoa oda zao mapema.

"Huduma zetu ni nafuu sana mfano kunyoa kwa wanaume ni Sh 2,000 hivyo mtaona tunalenga kuwahudumia watanzania wa kada zote, tuko hapa Dar es Salaam maeneo ya Buguruni Rozana, Tandika Sudan, Kwa Aziz Ali, Zahanati ya Mtoni na Mikoani tuko Kibaha Pwani," amesema Belina.
Mgeni rasmi katika tukio hilo Mtangazaji na Mchungaji maarufu jijini Dar , Haris Kapiga akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Gari maalum litakalokua linawafuata wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma.
Mgeni rasmi katika tukio hilo Mtangazaji na Mchungaji maarufu jijini Dar , Haris Kapiga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari maalum litakalokua linawafuata wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma.
Gari maalum iliyozinduliwa yenye ubora na vifaa vyote vya Saluni za kike na kiume ambalo litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wateja wake.
Meneja wa J&R Unisex, Suleiman Muhina akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu huduma zao, amesema huduma zao ni nafuu licha ya kwamba wao ndio wanaowafuata wateja na kwamba ndani ya gari hilo huduma zote zitolewazo Saluni zitapatikana kwa Wanawake na Wanaume.
Operesheni Meneja wa J&R, Belina Mlokozi amesema licha ya kufanya huduma zote za kike na kiume pia wanapamba na kuremba maharusi huku akisema kunakuwepo na punguzo la bei kwa wale wanaotoa oda zao mapema.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger