Thursday, 5 August 2021

SALUNI INAYOTEMBEA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

...

Gari maalum iliyozinduliwa yenye ubora na vifaa vyote vya Saluni za kike na kiume ambalo litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wateja wake.
 ***
KATIKA kuweza kuwaepusha wateja wao na changamoto ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona, Kampuni ya J&R Mtita Unisex inayojishughulisha na huduma za Saluni imezindua gari mahususi litakalokua linawafuata wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma hiyo.

Gari hilo lenye ubora na vifaa vyote vya Saluni za kike na kiume litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wateja wake lengo likiwa kupunguza msongamano wa wateja wanaofika kwenye Saluni zao kupata huduma lakini pia kuwahudumia wateja ambao wanakosa muda wa kwenda Saluni.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa gari hilo, Mgeni rasmi katika tukio hilo, Mtangazaji na Mchungaji maarufu jijini Dar , Haris Kapiga amesifu ubunifu uliooneshwa na Kampuni hiyo ya kizalendo akisema ni mfano wa kuigwa na utawasaidia katika pia Kupambana na ushindani wa kibiashara.

"Huu ni ubunifu mkubwa ambao inabidi vijana hawa wapongezwe, katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona kuna watu wanaogopa kuja Saluni kwa sababu za kiafya hivyo uwepo wa gari hili litakalokuwa linazunguka maeneo mbalimbali litakua msaada kwao.

Na siyo tu kupambana na Corona lakini pia wapo wafanyakazi wa maofisini ambao wapo bize na hawana muda wa kwenda Saluni sasa uwepo wa gari hili kwao ni faida kwani watafuatwa walipo na kupewa huduma, vivyo hivyo na kwa wanafunzi hasa wanaoishi bweni," amesema Kapiga.

Kwa upande wake Meneja wa J&R Unisex, Suleiman Muhina amesema huduma zao ni nafuu licha ya kwamba wao ndio wanaowafuata wateja na kwamba ndani ya gari hilo huduma zote zitolewazo Saluni zitapatikana kwa Wanawake na Wanaume.

Nae Operesheni Meneja wa J&R, Belina Mlokozi amesema licha ya kufanya huduma zote za kike na kiume pia wanapamba na kuremba maharusi huku akisema kunakuepo na punguzo la bei kwa wale wanaotoa oda zao mapema.

"Huduma zetu ni nafuu sana mfano kunyoa kwa wanaume ni Sh 2,000 hivyo mtaona tunalenga kuwahudumia watanzania wa kada zote, tuko hapa Dar es Salaam maeneo ya Buguruni Rozana, Tandika Sudan, Kwa Aziz Ali, Zahanati ya Mtoni na Mikoani tuko Kibaha Pwani," amesema Belina.
Mgeni rasmi katika tukio hilo Mtangazaji na Mchungaji maarufu jijini Dar , Haris Kapiga akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Gari maalum litakalokua linawafuata wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma.
Mgeni rasmi katika tukio hilo Mtangazaji na Mchungaji maarufu jijini Dar , Haris Kapiga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari maalum litakalokua linawafuata wateja kwa ajili ya kuwapatia huduma.
Gari maalum iliyozinduliwa yenye ubora na vifaa vyote vya Saluni za kike na kiume ambalo litakuwa linazunguka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa wateja wake.
Meneja wa J&R Unisex, Suleiman Muhina akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu huduma zao, amesema huduma zao ni nafuu licha ya kwamba wao ndio wanaowafuata wateja na kwamba ndani ya gari hilo huduma zote zitolewazo Saluni zitapatikana kwa Wanawake na Wanaume.
Operesheni Meneja wa J&R, Belina Mlokozi amesema licha ya kufanya huduma zote za kike na kiume pia wanapamba na kuremba maharusi huku akisema kunakuwepo na punguzo la bei kwa wale wanaotoa oda zao mapema.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo .
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger