Thursday, 5 August 2021

DC MSANDO AWATAKA WAFANYABIASHARA KUFUATA TARATIBU ZILIZOWEKWA...."SASA HAKUNA MUDA WA KUBEMBELEZANA"

...
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando

Na Jackline Lolah Minja Morogoro.
Wafanyabiashara mkoani Morogoro wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na serikali za namna ya ufanyaji biashara katika maeneo ya manispaa ili kuufanya mji kuwa safi.

Akizungumza na wafanyabiashara hao leo Alhamis Agosti 5,2021 katika Soko kuu la Kingalu ,Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando amesema kwa sasa hakuna muda wa kubembelezana katika kufuata utaratibu hivyo kama hutaki kufuata utaratibu ni vyema ukawapisha ambao wanaweza kufuata utaratibu.

“Na niliwaahidi hata kama zoezi hili litachukua muda mrefu lazima tuhakikishe wamachinga wote wanakaa sehemu anabyo ni sahihi hivyo kwa mara ya mwisho, tufuate utaratibu ambao tutawekeana hapa ,kama unadhani utabembelezwa sahau,kama unadhani utalialia kwamba kuna TV au Redio itakuonyesha unalialia na utahurumiwa sahau,heshimu wamachinga wenzako wanaopambana kutafuta maisha kama unayotafuta wewe hivyo usiwaharibie wenzako wanaohitaji kufuata utaratibu ,usijione wewe unafaa zaidi wenzako wakae sokoni juu wewe ushuke uje ufanye biashara hapa chini au uweke katikati ya barabara”, amesema .

Hivyo Msando amesema ataanzisha zoezi la kuhakiki mitaa ili kubaini wafanyabiashara ambao wamejiorodhesha ni sahihi na watatoa sababu kwa mitaa ambayo haitakuwepo kwenye orodha.

“Sasa basi kwa zaidi ya wiki tatu nilielekeza kuandikwa kwa majina ya wamachinga wote wanaofanya biashara katika mitaa ambapo hadi Jana Agosti 4 2021 saa kumi na mbili jioni wamachinga waliojiandiskisha ni 1312 ikiwemo viongozi 35 na sitapitia majina moja moja lakini nitataja mitaa ili kabla ya kwenda mbali tukubaliane kwa pamoja kwamba mitaa iliyoandikwa ni yote na tutatoa sababu kwamitaa iliyoachwa ,kwa kuwa sehemu zitakazotolewa kwaajili ya biashara zitatolewa kufuatana na majina yaliyoandikwa”, ameongeza.



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger