Sunday, 29 August 2021

ALIYETAKA KUJILIPUA KWENYE MAZISHI YA KIGOGO WA POLISI AKAMATWA

...

Mshambuliaji anayeshukiwa kuwa wa kujitoa muhanga amekamatwa nchini Uganda kwa kupanga kujilipua katika mazishi ya kamanda wa jeshi anayefahamika kama ‘they lion of Mogadishu’’.

Meja Jenerali Paul Lockech alipewa jina hilo la bandia tangu wakati alipokuwa Mkuu wa kikosi cha Muugano wa Afrika kilichopo nchini Somalia (Amisom) kuanzia mwaka 2000. Alisifika kwa kuwaondosha wanamgambo wa al-Shabab katika mji mkuu Mogadishu.

Amisom kilisema kuwa itamkumbuka kama “ mnara wa ishara ya heshima katika mapigano dhidi ya wanamgambo wenye silaha” , na kwamba atakumbukwa kama urithi ambao hauwezi kusahaulika.

Meja Jenerali Lokech mwenye umri wa miaka 55, ambaye alikuwa anafanya kazi akiwa Inspekta Jenerali wa polisi alifariki kutokana na ugonjwa wa kuganda kwa damu nyumbani kwake siku ya Jumamosi.

Rais Yoweri Museveni amekuwa akitarajiwa kuhudhuria mazishi yake katika wilaya ya kaskani Mwa nchi hiyo ya Pader. Mshukiwa alikamatwa Alhamisi mchana katika operesheni ya pamoja baina ya maafisa mbalimbali wa usalama.

Msemaji wa jeshi Flavia Byekwaso amesema kuwa alipatikana na zana za kutengeneza mabomu, ikiwa ni pamoja na mabegi ya mabomu, fulana za mabomu ya kujitoa muhanga, na kifaa cha kukata waya wa kulipua mabomu. Washukiwa wenzake pia wametambuliwa na operesheni bado inaendelea ili kuwapata, alisema.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger