Thursday, 14 May 2020

Finance Team Leader at Hyatt

Finance Team Leader  Summary Person responsible for below Account payable Cost control General cashier Qualifications To be Successful in This Role, You Will Require to Have; Minimum of two years’ experience in the industry and previous experience at a 5 start hotel. Certificate or qualification in Finance and/or Accounting. CLICK HERE TO APPLY

The post Finance Team Leader at Hyatt appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA TAASISI ZIFUATAZO; TIE, NIT, MNH NA KEC 14-05-2020

Share:

SHIRIKA LA SEMA LATOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA ASKARI POLISI WA MKOA WA SINGIDA

Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa akitoa elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Mkoa wa Singida leo asubuhi.
Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Mkoa wa Singida, wakipata elimu hiyo.
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Florence Mwenda, akisisitiza jambo kwa askari wa kituo hicho, wakati wa kutolewa kwa elimu hiyo.
Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa, akisisitiza jambo wakati akitoa elimu hiyo.
Maafisa wa Shirika lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) la Mkoa wa Singida, Gerson Janga (kushoto) na Witness Anderson wakitoa elimu hiyo kwa askari hao kwa njia ya mabango.
Askari hao wakiwa wamesimama kwa tahadhari ya kuacha mita zaidi ya moja kama njia ya kujikinga na maambukizi ya Corona.


Na Dotto Mwaibale,Singida

SHIRIKA lisilo la Kiserikali  la Sustanable Environment Management Action (SEMA) kwa kushirikiana na wadau kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya wamtoa  elimu ya kujikinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kwa Askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Singida .

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo,leo asubuhi Mdau wa mapambano dhidi ya Corona kutoka Taasisi ya Empower Youth Prosperity  ( EYP) ya mkoani Mbeya, Ipyana Mwakyusa alisema elimu hiyo ililenga kukumbusha namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

"Kila mtu anajua uwepo wa ugonjwa huu tunatoa elimu hii kwenu kwa ajili ya kukumbusha tukizingatia nyie wenzetu huwa mnakutana na watu wengi", alisema Mwakyusa.

Akielezea jinsi ya kujikinga na homa ya Virusi vya corona Mwakyusa alitoa tahadhari kwa askari hao kukaa mbali angalau mita 1 au 2 na mtu wakati wakiwa kazini.

Tahadhari nyingine alioitoa ni pamoja na kufunika mdomo na pua wakati wa kukohoa kwa kutumia kitambaa safi au sehemu ya mbele ya kiwiko cha mkono, kuepuka kugusana, kusalimiana kwa kushikana mikono.

Tahadhari nyingine ya jinsi ya kujikinga pamoja na mambo mengine ni kuepuka kugusa macho, pua au mdomo baada ya kunawa. 

"Safisha mikono yako mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kwa dawa ya kutakasa mikono", alisema Mwakyusa.

Akizungumzia ugonjwa huo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Florence Mwenda, alisema kwa upande wao wamechukua tahadhari zote za kujikinga pamoja na watu wanao wahudumia.

Kampeni ya utoaji wa elimu hiyo inafanywa  kwa ufadhili wa Shirika la Stromme East Africa Foundation lenye Makao Makuu Kampala nchini  Uganda huku ufadhili mkuu wa mashirika hayo ukitolewa na Shirika la Stromme Foundation la Norway kupitia mradi wa uwezeshaji jamii kiuchumi unaowalenga vijana wa kiume, wa kike, watoto na wakina mama. 

Share:

WAZIRI KABUDI AANIKA MAFANIKIO LUKUKI WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi jana amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2020/2021.


Wizara  hiyo imeliomba Bunge liiidhinishie jumla ya Shilingi bilioni mia moja tisini na tisa, milioni mia saba hamsini, laki sita themanini na nne elfu (199,750,684,000) zikiwa ni fedha kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na  bajeti ya miradi ya maendeleo.

Akiwasilisha makadirio hayo, Mhe. Prof. Kabudi alielezea mafaniko ambayo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeyapata katika kipindi hiki cha kwanza cha Serikali ya Awamu ya Tano 2015-2020.

==>>Mafanikio hayo ni:
 * Ufunguzi wa Balozi mpya nane katika nchi za Qatar; Uturuki; Sudan; Cuba; Israel; Algeria; Jamhuri ya Korea; na Namibia; 

* Kuifanya lugha ya Kiswahili kutumika katika Jumuiya ya Kimataifa na nchi mbalimbali;

* Kufanikisha kufanyika kwa viwango vya juu Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Dar es Salaam mwezi Agosti 2019;

*Kuhamasisha watalii kuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii;

*Kufanikisha uenyekiti wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo mwezi Machi 2016 nchi yetu iliteuliwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo;

*Kuratibu Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Nordic (Africa - Nordic Foreign Ministers’ Meeting) uliofanyika kwa mafanikio makubwa mwezi Novemba 2019 jijini Dar es Salaam;

*Kufanikisha ujumuishwaji wa miradi ya Tanzania katika miradi ya kipaumbele ya miundombinu iliyoidhinishwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki;

*Kutekeleza Itifaki ya Umoja wa Forodha na Itifaki ya Soko la Pamoja za Jumuiya ya Afrika Mashariki;

*Kuratibu upatikanaji wa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato jijini Dodoma na upatikanaji wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 180 kutoka Benki hiyo kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya pete katika jiji la Dodoma na

* Kushawishi nchi marafiki kutufutia madeni, kuyapunguza au kuweka masharti nafuu ya kuyalipa.


Share:

SERIKALI YATANGAZA BEI ELEKEZI YA CHANJO 13 ZA MAGONJWA YA MIFUGO

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imetangaza bei elekezi ya chanjo 13 za magonjwa ya mifugo ya kimkakati ambapo sasa wafugaji watapa ahueni kubwa kwa kutumia gharama ndogo kupata chanjo hizo huku Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akitaka bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania TVLA kuhakikisha Kliniki za mifugo zinajengwa kwenye halmashauri 185 kote nchini ifikapo Juni 2021.

Akitangaza bei elekezi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania, Profesa Hezron Nonga amesema bei hiyo itaanza kutumika leo na kwamba wafugaji na wafanyabiashara wote wanapaswa kufuata bei hiyo iliyotangazwa na Serikali.

Prof. Nonga amezitaja bei elekezi hizo kuwa ni pamoja ya Chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ngombe (CBPP) bei ya dukani kwa dozi itauzwa sh. 300 huku bei ya uchanjaji kwa mfugo ikiwa ni sh. 550, Chambavu (Black quarter) dozi dukani shilingi 500 kwa mfugo atachanjiwa sh. 800 

Amesema Kimeta (Anthrax) dozi dukani ni 250 na kwa mfugo itakuwa sh. 500, Mchanganyiko wa Chambavu na Kimeta (TECOBLAX) kwa Ng’ombe dozi dukani sh. 560 na kwa mfugo utachanjwa kwa sh. 800, Mchanganyiko wa Chambavu na Kimeta (TECOBLAX) kwa mbuzi na kondoo dozi kukani sh. 280 kwa mfugo ni sh. 500.

Aidha amesema ugonjwa wa Kutupa Mimba (Brucellosis) dozi dukani ni 1,000 na kwa mfugo ni 1,500, Mdondo (Newcastle disease) dozi ni shilingi 50 na mfugo ni 50, Mapele Ngozi (Lumpy Skin Disease) kwa ng’ombe dozi dukani ni sh. 400 na kwa mfugo ni sh. 600 huku Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) dozi dukani ni sh. 200 na kwa mfugo ni 350.

Pia Homa ya mapafu ya mbuzi (CCPP) dozi dukani ni 200 na mfugo itakuwa ni 350, Ugonjwa wa Miguu na Midomo (FMD) dozi dukani ni sh. 2,500 na kwa mfugo ni 3,000, Kichaa cha Mbwa (Rabies) dozi dukani ni 1,000 kwa mfugaji ni sh. 1,500.

Profesa Nonga ameongeza kuwa ugonjwa wa Ndigana Kali (ECF) dozi dukani ni sh. 10,000 na kwa mfugo ni sh. 17,000huku Homa ya Bonde la Ufa (RVF) dozi dukani ni sh. 400 huku kwa mfugo ikiwa ni sh. 700.

Akizungumza mara baada ya kuzindua Bodi hiyo ya TVLA, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema kupitia mabadiliko hayo ya Kanuni za kutoa bei elekezi, Serikali itakuwa imepunguza gharama kwa wafugaji kutoka shilingi bilioni 482.4 walizokuwa wakizutumia kununua chanjo hadi kufikia shilingi bilioni 237 ikiwa ni punguzo la asilimia 51.

Hivyo ameitaka bodi hiyo mpya kufanya kazi usiku na mchana kuwalea wafugaji wa Tanzania kupitia eneo hilo muhimu la chanjo na matibabu ya mifugo na kukuchochea ungezeko la uzalishaji mifugo hali itasaidia kuhudumia viwanda vya mazao ya mifugo vinavyojenga maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kupeleka kwenye masoko mbalimbali duniani.

Pia ameitaka bodi hiyo kukomesha matumizi ya dawa feki na zilizomaliza muda wake , kurahisisha upatikanaji wa chanjo hatua itakayowezesha kuendelea kupungua kwa magonjwa na kuweza kuongeza masoko na ushindani kimataifa.

Mpina ameigiza bodi hiyo kuhakikisha kuwa ifikapo Juni, 2021 chanjo 7 ambazo ziko katika hatua mbalimbali zizalishwe hapa nchini ili kuwawezesha wafugaji kuzipata kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

Pia Waziri Mpina ameitaka bodi huhakikisha kuwa ujenzi wa Kliniki za mifugo kwa halmashauri zote 185 kote nchini pamoja na mikoa 15 ambayo haina maabara kwa sasa ziwe zimekamilika ifikapo Juni 2021.

Mwenyekiti wa Bodi ya TVLA, Profesa Amandus Muhairwa amemhakikisha Waziri Mpina kuwa watatumia weledi wao wote kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote aliyoyatoa ili kuiwezesha Sekta ya Mifugo kupita hatua kubwa kwa kipindi chote cha uongozi wao.

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Dk. Haruni Mapesa kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Akida Khea kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Casmir Kyuki kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania na Selina Lyimo ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu(Mstaafu).


Share:

Vifo Vya Corona Marekani Vyafika 85,197.....WHO Yatoa Onyo, Ulaya Yaanza Kufungua Mipaka Yake

Vituo vya kuzuia na kudhibiti magonjwa nchini Marekani (CDC) vimetangaza vifo vipya 1,426 vinavyohusiana na Corona, na kufikisha jumla ya watu 85,197 waliofariki dunia tangu kuzuka kwa janga hilo.

Vituo vya CDC pia vimeripoti visa vipya 21,647 vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19, na kufikisha jumla ya idadi ya visa 1,430,348 vya maambukizi nchini humo.
 
Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani limeyataka mataifa kuchukua tahadhari za hali ya juu.

Katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya video kutoka Geneva, Mkurugenzi wa dharura wa WHO, Dkt Mike Ryan ameonya dhidi ya kujaribu kubashiri ni lini virusi vya Corona vitatoweka.

"Ni muhimu kufahamu hili: Virusi vinaweza kuwa janga jingine katika jamii zetu, na virusi hivi huenda visiishe, " Dkt Mike Ryan amesema.

Hayo yanajiri wakati Ulaya imeanza kuchukua hatua za awali kuelekea kufungua mipaka yake ya ndani, baada ya miezi miwili ya vizuizi vya kukabiliana na janga la Covid-19, huku WHO ikiyataka mataifa kuchukua tahadhari za hali ya juu.



Share:

Kampuni Ya Everwell Cable And Engineering Co. Ltd Yachangia Sh. Milioni 100 Kukabiliana Na Corona

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb), amepokea msaada wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 100 iliyotolewa na kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, inayojishughulisha na uzalishaji wa nyaya za kusafirisha umeme kwenye miradi mbalimbali ya umeme hapa nchini, kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea mchango huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  tarehe 13 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma.
 
Akizungumza wakati wa kupokea mchango huo Waziri Mhagama ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19. 

“Kwa niaba ya serikali nawashukuru sana kwa kuwa sehemu ya watanzania katika kipindi hiki cha mapambano ya janga la COVID-19. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa sehemu ya shida na raha za Taifa hili,” ameeleza Waziri Mhagama. 

Aidha, Waziri Mhagama amewahakikishia watanzania kuwa michango hiyo inasimamiwa vyema na serikali kwa kuitumia michango hiyo katika kushughulikia majukumu yaliyopangwa ya kupambana na janga la ugonjwa wa COVID-19. 

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango wao kwa Serikali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.
 
“Kampuni hii ni moja ya wawekezaji waliojenga Kiwanda hapa nchini, lakini pamoja na shughuli za uwekezaji wameguswa katika kipindi hiki wakati serikali inapambana na
janga hili la ugonjwa wa COVID-19, tunawashukuru sana kwa mchango wenu kwa watanzania ”amesema Dkt. Kalemani. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, Bw. Jiaopeng Lu ameeleza kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na watanzania katika uzalishaji wa bidhaa za kiwanda kabla ya Janga hili la Ugonjwa wa COVID-19, hivyo hawana budi kuhakikisha watanzania wanakuwa salama ili waendelee kushirikiana nao katika shughuli za uzalishaji. 

IMETOLEWA NA: 
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI 
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Waziri Mkuu Akagua Maendeleo Ya Ujenzi Wa Jengo La Tume Ya Uchaguzi (NEC), Lililopo Jijini Dodoma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) linalojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.

Novemba 18, 2019, Waziri Mkuu alitembelea mradi huo na kuonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkandarasi aliyekuwa akijenga jengo hilo ambaye ni Wakala Majengo Tanzania (TBA) na kuagiza kuvunjwa kwa mkataba.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumatano, Mei 13, 2020) wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la NEC. Amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na anaamini litakamilika kwa wakati.

“…Ninahakika mkiongeza nguvu katika baadhi ya maeneo tutafika na haya ndio Serikali inataka kuona taasisi zake zikifanya. Kwenye jengo hili ndipo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuchukua fomu.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT kwa namna walivyoratibu vizuri ujenzi wa jengo hilo. “Miradi mingi waliyokabidhiwa Suma JKT imekuwa ikijengwa kwa weledi mkubwa.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama amesema Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT ilikabidhiwa mradi wa ukamilishaji wa jengo hilo Desemba 24, 2019 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, 2020.

Amesema mradi huo unaosimamiwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU) kama mshauri wa mradi hadi leo (Mei  13, 2020) ujenzi wa jengo kuu la ofisi umefikia asilimia 85, jengo la kutangazia matokeo ujenzi wake umefikia asilimia 68, kazi za nje zimefikia asilimia 85 huku jengo la ghala limefikia asilimia 92.

Naye, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema mkataba wa mradi huo ulipaswa ukamilike Aprili 30, 2020 lakini baada ya kutembelea eneo la mradi wamekubaliana kuwa kazi hiyo iwe imekamilika ifikapo Mei 30, 2020 na Juni 1, 2020 watumishi wahamie na kuanza kazi.

Amesema mradi huo unagharimu zaidi ya sh. bilioni 12 na tayari zaidi ya sh bilioni sita zimeshatolewa na kwamba kazi zinazoendelea kwa upande wa jengo kuu la ofisi ni pamoja na kupachika milango na madirisha, kupaka rangi na kuweka vigae kwenye sakafu.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Wagonjwa Wa Corona Nchini Uganda Wafika 139 Baada Ya Wengine 13 Kuongezeka

Taarifa ya Wizara ya afya nchini uganda kwa vyombo vya habari inaashiria maambukizi mapya 13 ya kirusi cha Corona na kuifikisha idadi ya visa kuwa 139.

Wagonjwa wapya wote ni Madereva wa Malori ambapo kati yao Waganda ni 7, Wakenya 5 na Raia wa Eritrea mmoja  aliyepitia Sudan Kusini,Kenya,Tanzania na kisha Uganda kupitia mpaka wa Mtukula.

Takribani sampuli 2,104 zimefanyiwa vipimo,miongoni mwazo 1741 zikiwa za madereva huku 363 kutoka maeneo tofauti ya ndani mwa Uganda.


Share:

SERIKALI YATANGAZA BEI ELEKEZI YA CHANJO 13 ZA MAGONJWA YA MIFUGO


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA), Profesa Amandus Muhairwa baada ya kuiziduia bodi hiyo na kupokea taarifa ya kutangazwa kwa bei elekezi ya Chanjo Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akimkabidhi vitendea kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) baada ya uzinduzi wa Bodi ya TVLA Makao Makuu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mtumba jijini Dodoma.




Wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ullega mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo Makao Makuu ya Wi

zara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma

WAZIRI MPINA AIPA KIBARUA KIZITO BODI YA TVLA 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma


SERIKALI imetangaza bei elekezi ya chanjo 13 za magonjwa ya mifugo ya kimkakati ambapo sasa wafugaji watapa ahueni kubwa kwa kutumia gharama ndogo kupata chanjo hizo huku Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akitaka bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania TVLA kuhakikisha Kliniki za mifugo zinajengwa kwenye halmashauri 185 kote nchini ifikapo Juni 2021.


Akitangaza bei elekezi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania, Profesa Hezron Nonga amesema bei hiyo itaanza kutumika leo na kwamba wafugaji na wafanyabiashara wote wanapaswa kufuata bei hiyo iliyotangazwa na Serikali.
 

Prof. Nonga amezitaja bei elekezi hizo kuwa ni pamoja ya Chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ngombe (CBPP) bei ya dukani kwa dozi itauzwa sh. 300 huku bei ya uchanjaji kwa mfugo ikiwa ni sh. 550, Chambavu (Black quarter) dozi dukani shilingi 500 kwa mfugo atachanjiwa sh. 800  

Amesema Kimeta (Anthrax) dozi dukani ni 250 na kwa mfugo itakuwa sh. 500, Mchanganyiko wa Chambavu na Kimeta (TECOBLAX) kwa Ng’ombe dozi dukani sh. 560 na kwa mfugo utachanjwa kwa sh. 800, Mchanganyiko wa Chambavu na Kimeta (TECOBLAX) kwa mbuzi na kondoo dozi kukani sh. 280 kwa mfugo ni sh. 500.

Aidha amesema ugonjwa wa Kutupa Mimba (Brucellosis) dozi dukani ni 1,000 na kwa mfugo ni 1,500, Mdondo (Newcastle disease) dozi ni shilingi 50 na mfugo ni 50, Mapele Ngozi (Lumpy Skin Disease) kwa ng’ombe dozi dukani ni sh. 400 na kwa mfugo ni sh. 600 huku Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) dozi dukani ni sh. 200 na kwa mfugo ni 350.
 

Pia Homa ya mapafu ya mbuzi (CCPP) dozi dukani ni 200 na mfugo itakuwa ni 350, Ugonjwa wa Miguu na Midomo (FMD) dozi dukani ni sh. 2,500 na kwa mfugo ni 3,000, Kichaa cha Mbwa (Rabies) dozi dukani ni 1,000 kwa mfugaji ni sh. 1,500.
 

Profesa Nonga ameongeza kuwa ugonjwa wa Ndigana Kali (ECF) dozi dukani ni sh. 10,000 na kwa mfugo ni sh. 17,000
huku Homa ya Bonde la Ufa (RVF) dozi dukani ni sh. 400 huku kwa mfugo ikiwa ni sh. 700.
 

Akizungumza mara baada ya kuzindua Bodi hiyo ya TVLA, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema kupitia mabadiliko hayo ya Kanuni za kutoa bei elekezi, Serikali itakuwa imepunguza gharama kwa wafugaji kutoka shilingi bilioni 482.4 walizokuwa wakizutumia kununua chanjo hadi kufikia shilingi bilioni 237 ikiwa ni punguzo la asilimia 51.
 

Hivyo ameitaka bodi hiyo mpya kufanya kazi usiku na mchana kuwalea wafugaji wa Tanzania kupitia eneo hilo muhimu la chanjo na matibabu ya mifugo na kukuchochea ungezeko la uzalishaji mifugo hali itasaidia kuhudumia viwanda vya mazao ya mifugo vinavyojenga maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kupeleka kwenye masoko mbalimbali duniani.
 

Pia ameitaka bodi hiyo kukomesha matumizi ya dawa feki na zilizomaliza muda wake , kurahisisha upatikanaji wa chanjo hatua itakayowezesha kuendelea kupungua kwa magonjwa na kuweza kuongeza masoko na ushindani kimataifa.

Mpina ameigiza bodi hiyo kuhakikisha kuwa ifikapo Juni, 2021 chanjo 7 ambazo ziko katika hatua mbalimbali zizalishwe hapa nchini ili kuwawezesha wafugaji kuzipata kwa urahisi na kwa gharama nafuu. 


Pia Waziri Mpina ameitaka bodi huhakikisha kuwa ujenzi wa Kliniki za mifugo kwa halmashauri zote 185 kote nchini pamoja na mikoa 15 ambayo haina maabara kwa sasa ziwe zimekamilika ifikapo Juni 2021. 


Mwenyekiti wa Bodi ya TVLA, Profesa Amandus Muhairwa amemhakikisha Waziri Mpina kuwa watatumia weledi wao wote kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote aliyoyatoa ili kuiwezesha Sekta ya Mifugo kupita hatua kubwa kwa kipindi chote cha uongozi wao. 


Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Dk. Haruni Mapesa kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Akida Khea kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Casmir Kyuki kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania na Selina Lyimo ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu(Mstaafu).
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi May 14





















Share:

Tumefanya Maboresho Kwenye App Yetu ya Mpekuzi Ili Kukuwezesha Kupata Habari zetu Haraka hasa Wakati huu wa janga la Corona

Tumefanya maboresho katika App yetu ya MPEKUZI ili kuendana na changamoto ya sasa ya janga la Corona inayoikumba dunia Nzima

Usikubali kupitwa na taarifa muhimu zinazoendelea hapa nchini na Duniani  kwa Ujumla . Tumejipanga vizuri sana kukupatia taarifa sahihi na kwa wakati.

👉1. Tumebadili muonekano na kuufanya kuwa mzuri zaidi
👉2. Kila habari tunayoweka kuanzia sasa utapata notification kwenye simu yako 
👉3. Habari zote kwa sasa zinafika kwa haraka kwenye simu yako kuliko ilivyokuwa hapo awali

KUMBUKA: App yetu ni BURE. Unachotakiwa kukifanya ni kuingia Playstore na kupakua MPEKUZI APP

Kama tayari unayo, basi Ingia Playstore kwa ajili ya kupata UPDATE hii ya Toleo Jipya

Tumekurahisishia, Unaweza pia ...<<KU BOFYA HAPA>> Kupata toleo hili Bure Kabisa


Share:

Wednesday, 13 May 2020

KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MBUNGE SULEIMAN NCHAMBI YAUNGURUMA MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imeanza kusikiliza maombi ya dhamana dhidi ya Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (CCM) mara baada ya Mahakama ya wilaya ya Shinyanga mahali kesi ilipo kutokuwa na uwezo wa kutoa dhamana kesi za uhujumu uchumi.


Maombi hayo yameanza kusikilizwa leo Jumatano Mei 13,2020 kwa Njia ya Mfumo wa Mtandao katika mahakama hiyo chini ya Jaji Phocus Mkeha, ambapo Wakili wa Mbunge huyo Frank Mwalongo amewasilisha Hati ya Maombi ya kupewa dhamana kwa mteja wake katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga baada ya Mahakama ya wilaya kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za Uhujumu Uchumi na kutoa dhamana.

Baada ya Jaji huyo kusikiliza maombi hayo kwa upande wa Wakili wa mtuhumiwa Frank Mwalongo, pamoja na Mkuu wa Mashitaka wa Serikali Magreth Ndaweka, ambaye alikuwa akipinga Mbunge huyo asipewe dhamana kwa sababu akitoka ataharibu upelelezi, alisema maamuzi ya utoaji wa dhamana hiyo atatoa Mei 15 mwaka huu.

Mei 11 mwaka huu Mahakama ya wilaya ya Shinyanga, ilishindwa kutoa dhamana ya Mbunge huyo, kwa maelezo kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi wala utoaji wa dhamana kwa makosa yasiyozidi Shilingi Milioni 10, ambapo hati ya mashitaka ya Mbunge huyo haijataja thamani na kuambiwa waombe dhamana kwenye mahakama kuu.

Mbunge huyo kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani Mei 8 mwaka huu katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga na kusomewa mashitaka 12 ya Uhujumu Uchumi kwa kumiliki silaha na risasi kinyume cha Sheria, na kufunguliwa kesi namba 10 ya mwaka 2020.

Mbunge huyo na mke wake Aisha Khalfan Soud wapo katika gereza la Mhumbu wakisubiri hatma ya dhamana.
Share:

MAHAKAMA KUU MUSOMA YASIKILIZA MASHAURI 18 KWA NJIA YA MAHAKAMA MTANDAO

Na. Francisca Swai- Mahakama Kuu Musoma
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma, imesikiliza jumla ya mashauri kumi 18 kwa njia ya Mahakama Mtandao ‘Video Conference’ tangu ilipoanza kutumia teknolojia hiyo Mei 5, mwaka huu.


Akizungumzia matumizi ya Mahakama Mtandao, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe, John Kahyoza alisema walianza kusikiliza mashauri mawili yote yakiwa yanayohusu maombi ya kukata rufaa nje ya muda yalisikilizwa mbele yake wakati wafungwa wakiwa katika gereza la Musoma bila ya wao kufika Mahakamani.

Jaji Kahyoza alifafanua kuwa   mashauri 10 yalisikilizwa mbele yake, manne  yalisikilizwa na Mhe, Jaji, Zephrine Galeba  na mashauri yaliyobakia  yalisikilizwa na  Mhe, Jaji Ephery  Kisanya.

‘‘Mahakama ya Tanzania ilianza kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao muda mrefu katika baadhi ya Mahakama nchini ikiwa ni katika kutekeleza mpango mkakati wake wa miaka mitano (2015/2016 – 2019/2020). Hata hivyo jitihada hizo zimetiliwa mkazo kama njia ya kuepuka kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID 19)”, alisema Jaji Kahyoza.

Aliongeza kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma pia imeanza kusikiliza mashauri kwa njia hiyo Mei 12, mwaka huu, ambapo mashauri matatu yalisikilizwa  mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe, Rahim Mushi na kuaihirishwa bila ya Wakili wa Serikali Mhe, Jesse Temba na washtakiwa kufika mahakamani hapo.

Jaji Kahyoza alisisitiza kwamba Mahakama hiyo, itaendelea kusikiliza mashauri kwa mtandao. Pia itawekeana ratiba maalumu na Mahakama ya Hakimu Mkazi, zikiwemo za Wilaya ili kutekeleza maagizo ya viongozi wa juu wa Mahakama wakiwemo viongozi wa kitaifa wanaosisistiza kuepuka msongamano na mikusanyiko hasa katika kipindi hiki cha janga la Corona.


Share:

Kigwangala: Watanzania Endeleeni Kuwa Wazalendo Acheni Kutoa Taarifa Ambazo Sio Sahihi

Na  Ahmed Mahmoud Arusha
Wizara ya maliasili na Utalii Imejipanga kuhuisha sekta ya Utalii nchini kwa kushirikiana na wadau wa Utalii baada ya watalii kuonyesha nia ya kuja nchini kuanzia mwezi ujao.

Suala hilo limekuja wakati dunia ilipojipata kwenye kisa cha Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu Covid 19 Unaosababishwa na virusi vya Corona na kuzifanya nchi nyingi dunia kufunga mipaka yao kudhibiti janga hilo huku Watalii wengi wakisitisha safari zao za kuja nchini.

Kwa Muktadha huo kwa siku za karibuni sekta hiyo Imeshuka kwa kasi kubwa ndio maana serikali kwa kushirikiana na wizara ya Afya pamoja na taasisi za serikali na binafsi wamekaa kwa pamoja kujadili suala hilo la kuhuisha sekta ya Utalii

Akisoma Maazimio ya mjadala huo wa siku mbili Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala Mara baada ya Mkutano wa wadau wa sekta ya Utalii kuona ni namna gani wataweza kuhuisha biashara ya Utalii nchini uliofanyika kwenye Hotel ya Aman Resort nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Dkt.Kigwangalla Alisema kuwa sekta hiyo kwa kipindi kifupi imeshuka kwa kasi sana ndio maana wamekutana kujadili kwa kina namna nzuri ya  kuendeleakuwavuta watalii kuja nchini kwa kipindi hichi cha Ugonjwa wa Covid 19 na kama nchi kuwahakikishia watalii usalama wao na baadae tutoke na maadhimio ya pamoja tutakayoyapeleka kwa wakubwa kuyapitisha.

Alisema kuwa wao kama serikali ndio maana wameshiriki kwenye kikao hicho kwa lengo la kuona utalii unasimama tena na kurudi kwenye kasi yake kwani unachangia ajira zaidi million 1.65 hivyo kuucha hivi hivi ni sawa na kupoteza nguvu kazi na kushusha mapato ya taifa kwa hiyo tumeandaa muongozo wa kushirikiana kwa pamoja ndio maana kila moja wetu yupo hapa.

“Sekta hii imekumbwa na anguko la ghafla duniani baada ya kuzuka kwa janga la Covid 19 kwa kila nchi kufunga mipaka yake hivyo kutoweza kuwa na muingilianao wa mara kwa mara hivyo baada a kuona nchi za wenzetu wanafungua mipaka na watalii kuonyesha nia ya kuja nchini ndio maana tumekutana kuweka miongozo ya pamoja itakayosaidia kuepuka maambukizi baina yetu na wageni wakati wote wakiwa nchini”

Alisema kuwa suala hilo la usalama wa wageni watakaoingia nchini ni muhimu sana ikiwemo kuweka mazingira mazuri ya kujikinga na Ugonjwa huo kwa Wananchi wetu na Wageni wetu kwa kuwa suala hilo ni mtambuka sana linahitaji kutoa mafunzo kwa watoa huduma ya utalii.

Kwa Upande mwingine Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kuwa serikali ndio msemaji mkuu na mtoa taarifa sahihi za Ugonjwa wa homa kali ya mapafu(Cocid 19) inayosababishwa na virusi vya Korona na hivyo kinyume cha Wale walioelekezwa kutoa taarifa wengine wanaotoa taarifa hizo ni feki.

Dkt.Kigwangala aliyasema hayo jijini Arusha wakati walipokuwa wakisoma maazimio ya mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya utalii uliofanyika jijini Arusha ambapo aliwataka watanzania kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kuacha kuposti taarifa feki zinazoharibu suala zima la utalii.

Alisema siku za karibuni kumeibuka taarifa feki nyingi na nyingine  zimekuwa zikitolewa na wanasiasa ambao hawana mamlaka ya kuongea zaidi ya Waziri Mkuu,Waziri wa Afya na Mganga Mkuu wa Serikali wao ndio wenye mamlaka ya kutoa taarfia sahihi za Ugonjwa huo.

“Unaposema hawatoi taarifa sahihi wewe unataka taarifa ipi zaidi ya  wataalamu wa sekta ya Afya hizo  nyingine ni taarifa feki ambazo tunatakiwa kuzipuuza kwani zinaleta taharuki miongoni mwa jamii yetu  hapa lazima tuwe wazalendo kwa nchi yetu kwa kuacha kutoa taarifa feki ambazo hazijatolewa na serikali”

Kigwangalla alilazimika kuyasema hayo alipoulizwa swali na waandishi wa habari waliotaka kujua kumekuwa na taarifa zinazoonyesha kuwa serikali haitoi taarifa sahihi za Ugonjwa wa Covid 19 jambo ambalo alijibu kuwa wasemaji wa suala hilo wapo na serikali haiwezi kutoa taarifa feki kwa kuwa hao wataalamu pia wana ndugu zao hivyo taarifa zinatolewa kwa usahihi.

Aliwataka kuacha kuzusha masuala ambayo hawana utaalamu nayo akisema utakuta  wewe DJ unataka kuzungumzia masuala ya uhandisi lazima tufike mahala tuache  kupotosha umma na kuwa wazalendo kwa nchi yetu kwani mwisho wa siku suala hapa ni Usalama wa maisha ya watanzania


Share:

Sheria Ya Kodi Yatoa Msamaha Kwa Mapato Yasiyozidi Milioni 4 Kwa Mwaka

Na. Josephine Majura na Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Serikali imeeleza kuwa Sheria ya Kodi imetoa msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na wastaafu ambao mapato yao kwa mwaka hayazidi Shilingi milioni nne.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Lupembe, Mhe. Joram Ismael Hongoli, aliyetaka kujua sababu za Serikali kutoweka utaratibu wa kutowatoza kodi wastaafu ambao biashara zao hazizidi mtaji wa Shilingi milioni nne.

Dkt. Kijaji alisema kuwa wastaafu walioanzisha miradi midogo ya kilimo na biashara ambayo inawaingizia kipato kisichozidi Shilingi milioni nne hawapaswi kutozwa kodi kwa kuwa Sheria ya Kodi imetoa msamaha.

Alisema kuwa Kifungu cha nne cha Sheria ya Kodi ya Mapato kinatoa msamaha wa kodi ya mapato kwa mfanyabiashara ambaye mapato yake ghafi ya mwaka hayazidi Sh. milioni 4, hii ikiwa ni pamoja na mapato ya wafanyabiashara wastaafu ambao kiwango chao cha mapato hakizidi kiasi hicho kwa mwaka.

Mwisho.


Share:

Environment Management Officers (Transfer Vacancies) Opportunities at NEMC

Environment Management Officer II (10  Posts) -Transfer Vacancies TRANSFER VACANCIES The National Environment Management Council (NEMC) is a body corporate re-established in 2004 by the Environmental Management Act Cap.191 (EMA Cap. 191) as a national environmental regulatory and enforcement institution responsible for overseeing management and protection of environment in Tanzania. The object and purpose for which the Council was… Read More »

The post Environment Management Officers (Transfer Vacancies) Opportunities at NEMC appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger