Wizara ya maliasili na Utalii Imejipanga kuhuisha sekta ya Utalii nchini kwa kushirikiana na wadau wa Utalii baada ya watalii kuonyesha nia ya kuja nchini kuanzia mwezi ujao.
Suala hilo limekuja wakati dunia ilipojipata kwenye kisa cha Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu Covid 19 Unaosababishwa na virusi vya Corona na kuzifanya nchi nyingi dunia kufunga mipaka yao kudhibiti janga hilo huku Watalii wengi wakisitisha safari zao za kuja nchini.
Kwa Muktadha huo kwa siku za karibuni sekta hiyo Imeshuka kwa kasi kubwa ndio maana serikali kwa kushirikiana na wizara ya Afya pamoja na taasisi za serikali na binafsi wamekaa kwa pamoja kujadili suala hilo la kuhuisha sekta ya Utalii
Akisoma Maazimio ya mjadala huo wa siku mbili Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangala Mara baada ya Mkutano wa wadau wa sekta ya Utalii kuona ni namna gani wataweza kuhuisha biashara ya Utalii nchini uliofanyika kwenye Hotel ya Aman Resort nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Dkt.Kigwangalla Alisema kuwa sekta hiyo kwa kipindi kifupi imeshuka kwa kasi sana ndio maana wamekutana kujadili kwa kina namna nzuri ya kuendeleakuwavuta watalii kuja nchini kwa kipindi hichi cha Ugonjwa wa Covid 19 na kama nchi kuwahakikishia watalii usalama wao na baadae tutoke na maadhimio ya pamoja tutakayoyapeleka kwa wakubwa kuyapitisha.
Alisema kuwa wao kama serikali ndio maana wameshiriki kwenye kikao hicho kwa lengo la kuona utalii unasimama tena na kurudi kwenye kasi yake kwani unachangia ajira zaidi million 1.65 hivyo kuucha hivi hivi ni sawa na kupoteza nguvu kazi na kushusha mapato ya taifa kwa hiyo tumeandaa muongozo wa kushirikiana kwa pamoja ndio maana kila moja wetu yupo hapa.
“Sekta hii imekumbwa na anguko la ghafla duniani baada ya kuzuka kwa janga la Covid 19 kwa kila nchi kufunga mipaka yake hivyo kutoweza kuwa na muingilianao wa mara kwa mara hivyo baada a kuona nchi za wenzetu wanafungua mipaka na watalii kuonyesha nia ya kuja nchini ndio maana tumekutana kuweka miongozo ya pamoja itakayosaidia kuepuka maambukizi baina yetu na wageni wakati wote wakiwa nchini”
Alisema kuwa suala hilo la usalama wa wageni watakaoingia nchini ni muhimu sana ikiwemo kuweka mazingira mazuri ya kujikinga na Ugonjwa huo kwa Wananchi wetu na Wageni wetu kwa kuwa suala hilo ni mtambuka sana linahitaji kutoa mafunzo kwa watoa huduma ya utalii.
Kwa Upande mwingine Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla amesema kuwa serikali ndio msemaji mkuu na mtoa taarifa sahihi za Ugonjwa wa homa kali ya mapafu(Cocid 19) inayosababishwa na virusi vya Korona na hivyo kinyume cha Wale walioelekezwa kutoa taarifa wengine wanaotoa taarifa hizo ni feki.
Dkt.Kigwangala aliyasema hayo jijini Arusha wakati walipokuwa wakisoma maazimio ya mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya utalii uliofanyika jijini Arusha ambapo aliwataka watanzania kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao kwa kuacha kuposti taarifa feki zinazoharibu suala zima la utalii.
Alisema siku za karibuni kumeibuka taarifa feki nyingi na nyingine zimekuwa zikitolewa na wanasiasa ambao hawana mamlaka ya kuongea zaidi ya Waziri Mkuu,Waziri wa Afya na Mganga Mkuu wa Serikali wao ndio wenye mamlaka ya kutoa taarfia sahihi za Ugonjwa huo.
“Unaposema hawatoi taarifa sahihi wewe unataka taarifa ipi zaidi ya wataalamu wa sekta ya Afya hizo nyingine ni taarifa feki ambazo tunatakiwa kuzipuuza kwani zinaleta taharuki miongoni mwa jamii yetu hapa lazima tuwe wazalendo kwa nchi yetu kwa kuacha kutoa taarifa feki ambazo hazijatolewa na serikali”
Kigwangalla alilazimika kuyasema hayo alipoulizwa swali na waandishi wa habari waliotaka kujua kumekuwa na taarifa zinazoonyesha kuwa serikali haitoi taarifa sahihi za Ugonjwa wa Covid 19 jambo ambalo alijibu kuwa wasemaji wa suala hilo wapo na serikali haiwezi kutoa taarifa feki kwa kuwa hao wataalamu pia wana ndugu zao hivyo taarifa zinatolewa kwa usahihi.
Aliwataka kuacha kuzusha masuala ambayo hawana utaalamu nayo akisema utakuta wewe DJ unataka kuzungumzia masuala ya uhandisi lazima tufike mahala tuache kupotosha umma na kuwa wazalendo kwa nchi yetu kwani mwisho wa siku suala hapa ni Usalama wa maisha ya watanzania
0 comments:
Post a Comment