Sunday, 15 March 2020

Wanaovujisha Mapato Uwanja wa Taifa Kuchukuliwa Hatua Kali

Serikali itawachukulia hatua kali  za kisheria wale wote watakaobainika kushiriki kuvujisha na upotevu wa mapato katika Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa mechi za mpira wa miguu. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji  Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema, pamoja na kuongezeka kwa mapato katika mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa hizi karibuni katika Uwanja a Taifa kufikia shilingi Milioni 545.4/=, bado  Serikali imebaini mianya ya upotevu wa mapato katika uwanja huo. 

“ Serikali inawaonya wale wote waliokuwa wanashiriki katika kuvujisha na kufanikisha upotevu  wa mapato wakati wa mechi katika Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru, na kwamba haitasita kuwachukulia hatua kali dhidi yao pale watakaobainika “. 

Amesema,  Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na uvujishaji na upotevu wa mapato katika viwanja hivyo ili kuziba mianya yote na tayari baadhi ya njia zinazotumika zimeshabainika. 

Dkt. Abbasi amesema kwamba, kwa upande wa watendaji watakaobainika kujihusisha na uvujishaji na upotevu wa mapato, nao watachukuliwa hatua kali bila kujali nafasi zao na maeneo wanayosimamia wakati wa mechi zitakazofanyika katika viwanja hivyo. 

Kutokana na kuongezeka kwa mapato ya mechi kati ya timu za Yanga na Simba , Serikali imepata mapato ya jumla ya shilingi milioni 153.2 tu. Hatua ya kudhibiti mianya ya uvujishaji na upotevu wa fedha za Serikali moja ya mikakati ya kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato yake sahihi kutoka katiuka vyanzo vyake. Mapato hayo ndiyo yanayoumika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kutatua kero za wananchi.


Share:

“Nchi Yetu iko Salama dhidi ya Corona” – Dkt. Abbasi

Na. Immaculate Makilika - MAELEZO
Serikali imesema nchi iko salama dhidi ya ugonjwa wa CORONA  na tayari imechukua hatua kadhaa za tahadhari ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini. 

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa, Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kwamba ugonjwa huo sio tu hauingii nchini, lakini pia kuzuia kusambaa kwa maambukizi endapo utaingia. 

“Zipo hatua zinazochukuliwa ndani ya Taasisi na Wizara moja moja, lakini pia zipo hatua za kitaifa za kukabiliana na ugonjwa huu, na hivyo naomba kuwatoa hofu watanzania kuhusu ugonjwa huu” alisema Dkt. Abbasi 

Akifafanua hatua ya kwanza ya kukabiliana na ugonjwa huo, Dkt. Abbasi alisema, Serikali imeandaa utaratibu maalum katika maeneo ya Viwanja vya  ndege na maeneo ya mipakani, ambapo watu hawapimwi ugonjwa  wa corona bali joto la mwili ili kuangalia endapo joto limezidi kiwango cha kawaida  cha binadamu. 

“Watanzania waendelee kuchukua tahadhari kama Rais Magufuli alivyoeleza na wazingatie maelekezo ya namna ya kujikinga yanayoendelea kutolewa na Wizara ya Afya kupitia wataalamu  wake” alisema Msemaji wa Serikali 

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa  katika hatua ya pili, Serikali imeandaa  vituo maalum vya kuwatenga washukiwa, na kuna vifaa vyote vya kupima huu ugonjwa. Aidha, hatua ya tatu ni kuwepo kwa hospitali maalum katika kanda zote nchini, ambazo zimetengwa  na zitatangazwa endapo atatokea mgonjwa wa CORONA.  

Vilevile, Serikali inaendelea  kufanya jitihada  katika kupambana na ugonjwa huo  ikiwemo kusitisha safari za ndege katika nchi za China na Italia na safari ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu iliyokuwa iende nchini Tunisia kwa ajili ya mchezo uliokuwa ufanyike hivi karibuni . 

Dkt. Abbasi amevipongeza Vyombo vya Habari nchini kwa kuitikia wito wa Rais wa kuhabarisha umma kuhusu ugonjwa huu, na kuwataka kuzingatia maelekezo ya wataalamu.


Share:

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Upelelezi Sakata la Halima Mdee, Bulaya na Wafuas wa CHADEMA kudaiwa Kuvamia Gerezani Wakamilika

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa, amesema kuwa wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Halima Mdee na Ester Bulaya, walivamia kwa nguvu katika Gereza la Segerea, wakitaka kumtoa Mbowe bila kufuata utaratibu, hali iliyopelekea kumchania sare ya Jeshi Askari aliyekuwa lindo.

Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Machi 15, 2020, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa tayari upelelezi wa wafuasi 27 wa CHADEMA, umekwishakamilika na kesho watalipeleka jalada kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua zingine.

"Walikuwa na wafuasi wengi waliokuwa wamekusanyika kwenye geti la kuingilia Gerezani, na kutaka kulazimisha kuingia kwa nguvu, getini pale kuna ulinzi, walitumia nguvu, ambapo hata Askari aliyekuwa lindo alichaniwa sare yake, kwahiyo wao walitaka kwenda kumtoa Mwenyekiti wa chama hicho bila kukamilisha taratibu" amesema Kamanda Mambosasa.  

“Tulifika eneo la tukio na kukuta askari wa magereza wakiendelea kuwadhibiti wanachama hao ndipo polisi walipowakamata watuhumiwa 27 na kuwapeleka katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano.

“Baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeshakamilika,” ameongeza.


Share:

Biteko Asema imetosha kuhusu Mchuchuma na Liganga

Na Issa Mtuwa – Ludewa
Serikali kupitia Waziri wa Madini Doto Biteko amesema, serikali ipo katika hatua za mwisho za majadiliano kuhusu miradi ya mchuchuma na Liganga ili iweze kuanza. Ameongeza kuwa mradi wa mchuchuma na Liganga ni miradi ya miaka mingi lakini haina tija na ndio maana serikali ya awamu ya tano iliamua kufuatilia kuhusu mikataba ya miradi hiyo ili kuona kama ina tija kwa taifa wakiwemo watu wa Ludewa. 

Akizungumza jana tarehe 15 Machi, 2020 wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Mundindi wilayani Ludewa,Waziri wa Madini Doto Biteko amesema, pamoja na kuchelewa kuanza kwa miradi ya Mchuchuma na Liganga, kuna manufa makubwa kwa wananchi na taifa kuliko miradi hiyo ingeanza kabla kufanyika kwa majadiliano yanayoendelea.  

“Ndugu zangu niseme stori za Mchuchuma na Liganga imetosha. Nafahamu mnamahitaji makubwa kuona hii miradi ianze, hata mimi nikiwa mdogo nimeshasikia sana kuhusu miradi ya Mchuchuma na Liganga, serikali tunayo sabau ya kuangalia maslai yenu na taifa. naomba niwaambie, serikali yenu ipo kwa ajili yenu, naomba kuweni na  subira” alisema Biteko. 

Biteko ameongeza kuwa serikali iligundua mambo mengi yasiyo na tija kuhusu mikataba ya miradi hii ndio maana tuliamua kufanya majadiliano ilikuona namna gani serikali itakavyonufaika. Mmekuwa wapole, watulivu na wasikivu ni jambo zuri sana, niwaombe endeleni kuwa wavumilivu  viongozi wenu wa mkoa na wilaya, mbunge na diwani wenu wamekuwa na kilio kama chenu ndio maana niliamua nije niweze kuzungumza na ninyi.  

Biteko amesema, hakuna mwananchi yeyote atakae punjwa kuhusu fidia yake, serikali italisimamia suala hilo kwa uzito mkubwa. 

“Nawaomba. kuweni na imani na serikali yenu, nitasimamia kama nilivyosimamia fidia za wananchi wa  Nyamongo wilayani Tarime dhidi ya Mgodi wa North Mara waliokuwa wanahitaji maeneo ya wananchi.  

Ndugu zangu ninachotaka kila jamii inufaike na mali zilizopewa na mungu. Ludewa najua mnataka kunufaika na miradi ya Mchuchuma na Liganga kama ambavyo Geita wananufaika na Dhahabu, Shinyanga wananufaika na Almasi,  Songea wananufaika na Makaa ya Mawe, Arusha wananufaika na Tanzanite na Tanga wananufaika kuhusu vipepeo vya kila aina.” aliongeza Biteko. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amemshukuru Waziri kwa kutimiza ahadi yake ya kuja Njombe kwa ajili ya ziara hii na kutembelea maeneo mbalimbali ya maeneo ya sekta ya madini na kuzungumza na wananchi hasa wa Ludewa ambao wanakilio kikubwa kutokana na kuchelewa kwa miradi ya Mchuchuma na Liganga. 

Diwani wa Kata ya Mundindi, Wise Mgina, amemweleza Waziri kuwa watu wa Ludewa wanapenda kuona miradi hiyo ikianza kwa kuwa ni miradi ya muda mrefu na wananchi wake wanashindwa kuendeleza ardhi hiyo kutokana zuio hivyo wanaiomba serikali miradi hiyo ianze ili iwanufaishe wananchi wake.


Share:

MAMBOSASA ADAI KINA MDEE WALIMCHANIA SARE ASKARI


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP Lazaro Mambosasa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa, amesema kuwa wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Halima Mdee na Ester Bulaya, walivamia kwa nguvu katika Gereza la Segerea, wakitaka kumtoa Mbowe bila kufuata utaratibu, hali iliyopelekea kumchania sare ya Jeshi Askari aliyekuwa lindo.

Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Machi 15, 2020, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa tayari upelelezi wa wafuasi 27 wa CHADEMA, umekwishakamilika na kesho watalipeleka jalada kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua zingine.

"Walikuwa na wafuasi wengi waliokuwa wamekusanyika kwenye geti la kuingilia Gerezani, na kutaka kulazimisha kuingia kwa nguvu, getini pale kuna ulinzi, walitumia nguvu, ambapo hata Askari aliyekuwa lindo alichaniwa sare yake, kwahiyo wao walitaka kwenda kumtoa Mwenyekiti wa chama hicho bila kukamilisha taratibu" amesema Kamanda Mambosasa.
Chanzo - EATV
Share:

Serikali Yasitisha Michezo ya UMISETA, UMITASHUMTA ......Yatoa Maelekezo Kuhusu Mahafali Kidato cha 6




Share:

Wakurugenzi simamieni ukusanyaji wa Mapato

Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wameagizwa kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa Mapato ya ndani ili kutimiza malengo yaliyopangwa na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2019/2020

Agizo hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga alipokuwa akikagua  miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Ameseama kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepangiwa kukusanya  zaidi ya shilingi bilioni 765 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 lakini hadi kufikia Februari, 2020 Mamlaka hizo zimeweza kukusanya mapato kwa asilimi 61 ya malengo ya mwaka.

“Inasikitisha kuona baadhi ya maeneo fedha za makusanyo ya mapato zinaingia mifukoni mwa watu, unakuta wanakusanya fedha lakini haziingii kwenye akaunti za Halmashauri, jambo hili linaisababishia Serikali kupoteza Mapato”Amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga ameendelea kwa kusema kuwa ili Halmashauri ziweze kutekeleza mipango yake  na kufikia malengo waliojiwekea katika mwaka ni wajibu wa wakurugenzi wote kuweka nguvu katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuzitumia fedha hizo  kwa kazi zilizopangwa.

 “Ongezeni kasi ya kukusanya mapato ya ndani, hakikisheni malengo mliyoweka ya ukusanyaji wa mapato yanatimizwa, zibeni mianya ya upotevu wa mapato hasa kwa watumishi wanaosimamia ukusanyaji huo, jambo hili linatia doa na kusababisha Halmashauri nyingi kutokamilisha  miradi ya maendeleo kwa wakati” Amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.

Kuhusu matumizi ya fedha za ndani na ruzuku za Serikali Mhandisi Nyamhanga amesema Serikali inatoa fedha nyingi sana  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ni wajibu wa Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha.

Amesema kuwa baadhi ya Halmashauri fedha hizo zinakusanywa lakini zinaanza kutumika kabla hazijaingizwa kwenye akaunti za Halmashauri, hii ni sawasawa na kutumia fedha mbichi hivyo naelekeza fedha hizo zikusanywe na kuingizwa kwenye akaunti ndipo zianze kutumika

Amefafanua kuwa Fedha nyingi zinakusanywa katika Halmashauri lakini haziingii kwenye Akaunti, Wakurugenzi hakikisheni  mnatumia mifumo ya kielektroniki kukusanya mapato na kuhakikisha fedha hizo zinaingia kwenye Halmashauri

Mhadisi nyamhanga amesema kuwa Halmashauri hazina budi  kuongeza kasi  ya ukusanyaji wa mapato ya ndani  lakini kupanga matumizi  mazuri ya fedha hizo  kama yalivyopangwa  kwenye bajeti zao .

Aidha amesisitiza kuwa Serikali imesambaza mashine  7227  kwenye Halmashauri mbalimbali nchini  kwa ajili ya kuboresha  ukusanyaji wa mapato ambapo ugawaji umeenda sambamba  na  uwezo wa Halmashauri katika kukusanya mapato.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema kuwa wameweza kudhibiti wizi wa mapato ya ndani kwa kuhakikisha matapeli wote wa Mapato wanatafutwa na kuzirudisha fedha hizo

Wakati huohuo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga  amefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na kutembelea  mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Mvomero na mradi wa ujenzi wa Sekondari ya kumbukumbu ya Sokoine..

Na. Angela Msimbira MVOMERO


Share:

Mradi Wa Upangaji Na Upimaji Ardhi Manispaa Ya Shinyanga Waikuna Kamati Ya Bunge

Na Munir Shemweta, WANMM SHINYANGA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Malisili na Utalii imeridhishwa na maendeleo ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Mradi huo wa viwanja 320 ni mkopo usio na riba wa shilingi milioni 240 kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ukiwa na lengo la kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji ili kuondoa migogoro ya ardhi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mradi huo mkoani Shinyanga jana Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kemilembe Lwota alisema kamati yake imeridhishwa na mradi huo na kuuita wa mfano  kwa kuwa umetekelezwa kwa asilimia mia moja.

Kwa mujibu wa Kemilembe, kati ya halmashauri 24 zilizopatiwa mkopo wa aina hiyo halmashauri nne zimerejesha fedha zilizokopeshwa kwa asilimia mia moja na baadhi yake zimepata faida kupitia mkopo huo ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuzitaka halmashauri nyingine kwenda kujifunza katika Manispaa hiyo.

‘’Sote tunajua migogoro ya ardhi iliyopo Tanzania na tumekuwa tukihimiza kwa muda mrefu upangaji, upimaji na umilikishaji maeneo ili kuondoa migogoro na nia ya kamati yetu ni kutaka kuona kila kipande cha ardhi kinapimwa’’ alisema Kemilembe

Aliipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa hatua kubwa ya kutoa fedha za mkopo usio na riba kwa halmashauri ili kuongeza kasi ya upangaji ambapo alitoa wito kwa wananchi kununua maeneo yaliyopimwa na kumilikishwa kwa kuwa hati zake zinaweza kutumika kuchukulia mkopo benki.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula  alisema pamoja na mamlaka ya upangaji kuwa chini ya halmashauri lakini Wizara yake iliamua kuziwezesha baadhi ya halmashauri kwa kuzipatia mkopo wa fedha usio na riba ili kuongeza kasi ya upangaji, upimaji  na umilikishaji maeneo.

Amezitaja halmashauri zilizopatiwa mkopo katika mkoa wa Shinyanga mbali na Manispaa ya Shinyanga kuwa ni halmashauri ya Mji wa Kahama milioni 220 na ile ya Mji wa Msalala milioni 120 ambazo zote zimefanikiwa kurejesha mikopo yake kwa asilimia mia moja

‘’ Lengo la Wizara ya ardhi ni kupanga, kupima na kumilikisha kila kipande cha ardhi nchini na mkopo tunaoutoa sasa kwa baadhi ya halmashauri unatokana na upatikanaji fedha ‘’ alisema Dkt Mabula.

Hata hivyo, Naibu Waziri Mabula alisema, Wizara yake katika siku zijazo ina mpango wa  kupima kila kipande cha ardhi kutokana na Benki ya Dunia na ile ya Exim-Korea kuonesha nia ya kusaidia zoezi hilo na kusisitiza kuwa suala hilo litakapofanikiwa migogoro ya ardhi nchini itapungua kama siyo kuisha kabisa.


Share:

Fidia Chanzo Za Migogoro Ya Ardhi Kwa Wananchi.

 SALVATORY NTANDU
Kamati ya Bunge ardhi Mali asili na Utalii imezishauri  Halmashauri zote  nchini kutowahamisha wananchi katika maeneo yao kabla ya kuwalipa fidia pindi wanapotaka kutubadilisha matumizi ya ardhi ili kupunguza migogoro isiyokuwa na tija baina yao na serikali.

Kauli hiyo imetolewa Machi 14 Mwaka huu Mkoani Shinyanga na Mwenyekiti wa Kamati Bunge ardhi Mali asili na Utalii, Kemilemba Lwota, Mbunge wa Viti maalum kupitia Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza (CCM) baada ya kutembelea mradi wa upimaji na upangaji makazi katika Manspaa ya Shinyanga.

Alisema Wizara ya Ardhi imetoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 8 kwa Halamshauri 20 hapa nchini kwaajili ya kupima,kupanga na kurasimisha makazi ya wananchi sambamba na kutoa hati miliki za viwanja na nyumba kwa wananchi ili kuwawezesha kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha.

“Katika Miradi iliyotembelewa na kamati yetu tumebaini kuwepo kwa kasoro mbalimbali katika utwaaji wa maeneo ya wananchi ambapo wengi wao wamekuwa wakiondolewa katika maeneo yao kabla ya kupewa fidia na kusababisha migogoro ambayo inaweza kusababisha kukwamkisha shughuli za maendeleo”,alisema Lwota.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi  Anjelina Mabula alisemakatika mkoa wa Shinyanga, Halmashauri ya Mji kahama ilikopeshwa shilingi milioni 220 Manispaa ya shinyanga shilingili milioni 240 na Halmashauri ya Msalala 120 kwaajili ya Upimaji na upangaji wa maeneo ya Makazi.

“Halmashauri ya Mji kahama  na Manspaa ya Shinyanga ndio zimerejesha mikopo yake kwa asilimia 100 huku Msalala ikiendelea na zoezi la kulipa mkopo huu,Wakurugenzi naomba hamasisheni wakazi wa meneo yenu wawena hati miliki za ardhi ambazo zitawasidia pindi wanapohitaji mikopo”alisema Mabula.

Mabula alisema kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha unatokomeza migogoro ya ardhi katika maeneo ambayo hayajapimwa na kupangwa kwaajili ya shughuli za Makazi ili kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi zao kisheria sambamba na serikali kupata mapato.


Share:

Maalim Seif Sharif Hamad achaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha ACT Wazalendo

Maalim Seif Sharif Hamad amechaguliwa kuwa mwenyekti mpya wa chama cha ACT- Wazalendo huku Zitto Kabwe akitetea nafasi kiongozi wa chama hicho kwa mara ya pili mfululizo katika uchaguzi uliofanyika jana Machi 14, 2020.

Kwa matokeo hayo Maalim Seif ambaye pia ni mshauri mkuu wa ACT-  Wazalendo anakuwa mwenyekiti wa pili wa chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 2014.

Maalim Seif na Zitto Kabwe ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini walichaguliwa usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 15, 2020 katika mkutano mkuu wa pili wa chama hicho uliokuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi wa viongozi wa nafasi ya uenyekiti na kiongozi wa ACT- Wazalendo.



Share:

Nyumba (pagala) limeshuka bei: Mapinga jirani na Bunju

Nyumba (pagala) limeshuka bei: Mapinga jirani na Bunju

Pagala la vyumba 3 na kiwanja cha sqm 416 (mita 16/26) linauzwa kwa bei ya kutupwa. Huduma za umeme na maji zipo na lipo mtaa wa maana. Lipo umbali wa km 2 kutoka main road.

Kwa mwenye milion 11 awahi kulipia, alipaue na kuhamia.

Kwa taarifa zaidi call 0758603077


Share:

FAINALI YA REDE KUPIGWA LEO MKWAKWANI TANGA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertaiment Nasoro Makau ambao ndio waandaaji wa Mashindano ya Rede Jijini Tanga akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Fainali ya Mashindano hayo kushoto ni
Mratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango kulia ni Msimamizi wa Waamuzi Magdalena Liwemba
 Mratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango akisisitiza jambo kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertaiment Nasoro Makau ambao ndio waandaaji wa Mashindano ya Rede Jijini Tanga na Msimamizi wa Waamuzi Magdalena Liwemba
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali

FAINALI ya Mashindano ya Rede itafanyika leo kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga huku ushindani mkubwa ukitarajiwa kujitokeza kutokana na timu zilizoingia kwenye hatua hiyo.

Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yameandaliwa na Kampuni ya Five Brothers Intertaiment kupitia Mkurugenzi wake Nassoro Makau.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuekelea fainali hiyo Makau alisema kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na timu ambazo zitachuana zimeanza kujiandaa vema.

Alisema kwamba wamejikita kuhakikisha michezo yote ya zamani wanairudisha ikiwemo Rede ambao kwa sasa mashindano hayo ni msimu wanne ambao umekuwa mchezo mkubwa na kuweza kutambulika na kupata mialiko mbalimbali hata kwa mikoa ya jirani.

Aidha alisema malengo yao na kuhakikisha mchezo huo unafika mbali kama ilivyokuwa michezo mingine hapa nchini kutokana na kwamba inatoa fursa kwa wanawake kuweza kushiriki kwenye michezo na kupata manufaa.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba mashindano hayo yalianza 2017 yamekuwa yakikumbana na changamoto mbalimbali lakini kubwa ni ukosefu wadhamini na ndio maana kupelekea zawadi kuwa za kususasua.

Hata hivyo alisema pamoja na hayo aliwashukuru wahisani kwa kuendelee kumsapoti na kuwaunga mkono katika mashindano hayo ikiwemo Benki ya NMB, Tanga Women Group, Arbarb Intertainment na Mkulima.

Aliwataja wahisani wengine ni Tanga City Lounge,Dion Pub,Lacosta Pub,Cholloo Spare Party,Quality Class Wear,G1 Security wakatao weza ulinzi,All Stars One 21 huku akiwataka wadhamini kujitokeza kudhamini mchezo huo.

Awali akizungumza Mratibu Mkuu wa Mashindano hayo Zaituni Mango alisema kwamba huo ni msimu wa nne wa mashindano hayo yaliyoanza 2017 .

Alisema msimu huo wa wanne ulianza February 10 mwaka huu na february 13 ndio walianza mashindano kwa timu tisa ambazo ni Magomeni Queen,Costo Ladiers,Mkwakwani Basket,Kwaminchi Queeni,Magomeni Sisiter,Mwarongo,Street Colurs,Tanga Kwanza na Daba, Jangos.

Mratibu huyo alisema kwamba timu hizo zilicheza na baadae kujichuja na kubakia timu mbili ambazo zimeingia kwenye hatua hiyo ya fainali ili kumpata bingwa.

Akielezea suala la zawadi kwa ajili ya washiriki ambapo alisema mshindi wa kwanza ataapata medali za fedha kwa wachezaji saba ,cheti ch ushiriki kwa timu ,Unga wa ngano kg 25,Mafuta ya kupikia lita 10 na fedha taslimu.

Alisema mshindi wa pili medali za fedha kwa wachezaji saba,cheti na ngano kg 15 na mafita lita sita na fedha taslim huku mshindi wa tatu akipata cheti ngano kg 10 mafuta lita 3 na fedha taslimu.


Hata hivyo alisema kwa upande wa mshindi wanne watapata cheti, ngano kg 10 na mafuta lita 3 na fedha na washiriki wote tisa watapata cheti huku mchezaji bora atakapata fedha na mpira utakaotumika kucheza fainali.

Alisema mfungaji bora atapata fedha na kitropiki huku timu yenye nidhamu itapata kikombe
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili March 15













Share:

Saturday, 14 March 2020

Jeshi La Magereza Lakanusha Madai Ya CHADEMA Ya Ukiukwaji Wa Haki Za Binadamu Magerezani

Na.Faustine Gimu Galafoni- Dodoma
Jeshi la Magereza nchini limesema kauli na taarifa za baadhi ya viongozi wa  CHADEMA zilizoenezwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kulituhumu jeshi hilo kwa utendaji wake ni za kupuuza na hazina mashiko yoyote.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma jana majira ya jioni  Machi ,13,2020,eneo la Gereza la Isanga ,mrakibu wa jeshi la Magereza S.S.P Amina Kavirondo alisema   gereza ni sehemu salama na mtu anapokelewa kama watu wengine hivyo mfungwa anapoingia gerezani anatakiwa awe salama na anatoka salama hivyo kukaguliwa ni jambo la muhimu bila kujali cheo chake.

“Jukumu letu kama jeshi la magereza ni kumkagua mfungwa pindi anapoingia gerezani ili ku- protect[kulinda]usalama wake na gereza kwa ujumla maana anaweza kuingia na kitu chochote kinachoweza kudhuru  na hili halifanywi kwao tu kama viongozi wa CHADEMA linafanywa na kila mtu na utaratibu huu unafanyika maeneo mengi duniani ,kwa hiyo kauli wanazoeneza hazina msingi wowote”aLIsema.

Kuhusu vipigo S.S.P Amina aLIsema jeshi la Magereza lina sheria na taratibu zake hivyo haliwezi kumwonea mtu na endapo kutatokea mfungwa yeyote anataka kuhatarisha usalama wa wengine huwa kuna taratibu hufuatwa na mwanasiasa aliyesema wafungwa wanapokea kichapo hizo ni taarifa za kiharakati na zinapaswa kupuuzwa.

Katika hoja ya kujitosheleza kwa jeshi hilo S.S.P Amina  amesema jeshi la Magereza kwa sasa linajitosheleza kwa chakula lakini kwa mahitaji mengine litahudumiwa na serikali  kama vilivyo vyombo vingine vya ulinzi na usalama hivyo Mwanasiasa aliyesema jeshi hilo halijitoshelezi kwa chochote hoja yake haina msingi.

Pia amesema mfungwa ama mahabusu hupelekwa Mahakamani kwa Maamuzi  na wito wa mahakama na  tarehe husika    na jeshi la magereza haliwezi kumpeleka mahakamani bila maamuzi  na wito wa mahakama  huku akisema Kwenye sakata la upimaji  wa Afya S.S.P Amina amesema  utaratibu wa kupimwa  afya gerezani uko tofauti na hospitalini hivyo hoja ya mwanasiasa aliyelalamika kuwa magerezani wana pima VVU hadharani haina Mashiko.


Share:

COMPLIANCE OFFICER. – 2 POST – Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO)

POST COMPLIANCE OFFICER. – 2 POST POST CATEGORY(S) HR & ADMINISTRATION LEGAL EMPLOYER Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO) APPLICATION TIMELINE: 2020-03-13 2020-03-26 JOB SUMMARY N/A DUTIES AND RESPONSIBILITIES i.To carry out ad hoc and  monthly safety aerodrome inspections; ii.To compile safety general reports quarterly; iii.To  prepare monthly safety inspection reports and submit on time; iv.To monitor, observe and… Read More »

The post COMPLIANCE OFFICER. – 2 POST – Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasi na Utalii Yakataa Milioni 150 Kukarabati Jengo La Utawala

NA TIGANYA VINCENT
WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi , Maliasi na Utalii wameagiza kujengwa kwa Jengo la Utawala katika Chuo cha Mafunzo ya ufagaji nyuki (BTI) badala ya kukarabati lilipo kwa gharama ya shilingi milioni 150.

Ilisema fedha hizo zinaweza kujenga jengo jipya kwa fedha kidogo na zitakazobaki zikatumika katika shughuli nyingine.

Kamati hiyo imetoa kauli hiyo leo wakati wajumbe wake walipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kukagua jengo linatotaka kukarabatiwa na kukagua shughuli nyingine za mafunzo ya ufugaji nyuki mkoani Tabora.

Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massay alisema matumizi ya milioni 150 kwa ajili ya ukarabati ni kinyume na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya matumizi kidogo ya fedha matokeo makubwa ya mradi.

Aliiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamisha matumizi ya fedha hizo ili ziliekelezwe katika ujenzi wa jengo jipya na la kisasa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Longido Dkt. Steven Kiruswa alisema ni vema utaratibu wa utekelezaji wa mradi huo utatumia ujenzi kwa kutumia mafundi wa ndani( force account) ili kuwezesha sehemu ya fedha zikabaki na kuelekekwa kujenga miundo mbinu mingine. 

Mbunge Jimbo la Chambani Yussuf Salim Hussein alimwomba Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuhakikisha anasimamia ili utaratibu wa ujenzi uwezo wa kutumia mafundi ya ndani ya Taasisi kwa ajili ya kuhakikisha matumizi sahihi.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Kaliua  Magdalena Sakaya alisema utendaji kazi wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) sio mzuri na ndio miradi yao mingi inakuwa na gharama kubwa.

Alisema kuwa pamoja na kuwa ni Taasisi ya umma ni vema Serikali ikatumia utaratibu mwingine kuliko kuwapa miradi ambayo wanashindwa kuikamirisha kwa wakati na wakati mwingine ubora wake hauridhishi.

Aidha alisema badala ya kujenga jengo la utawala ni vema fedha hizo zikatumika kujenga Maabara kwa ajili kutoa mafunzo ya uzalishaji asali bora.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kemirembe Lwota aliitaka Wizara hiyo kubadili mpango wa awali wa kutumia fedha hizo ili zielekezwe kwenye ujenzi wa jengo jipya la utawala.

Naye  Naibu Katibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki amesimamisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo ambayo ilikuwa ifunguliwe wiki ijayo.

Alisema wamekubaliana na ushauri wa Kamati wa kutumia fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya na sio ukarabati.

Mwisho


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger