Thursday, 22 January 2026

WANANCHI WA UKONGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUDUMISHA AMANI NA USALAMA

...




Na Mwandishi wetu, Dar

Wananchi wa Ukonga Mkoani Dar Es Salaam wametoa pongezi na Shukrani kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha amani, utulivu na usalama katika Jimbo lao la Ukonga, suala ambalo limewezesha shughuli za kiuchumi na kijamii kuendelea.

Kwaniaba ya wananchi wengine wa Jimbo hilo wakati akizungumza na Chombo chetu cha habari, Bw. Salum Issa Salum, Mkazi wa Kata ya Buyuni ameeleza kuwa licha ya kupitia baadhi ya changamoto mwishoni mwa mwaka jana, hali kwasasa ni shwari na hatua za maendeleo zimeendelea kushuhudiwa katika Kata hiyo na maeneo mengine kote Tanzania.

"Nisemee zaidi katika miundombinu, Mama amesikia kilio chetu na sasa barabara nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa DMDP kutoka hapa kwetu kwenda Kivule." Amesema Bw. Salum.

Katika maelezo yake, Mwananchi huyo amemuombea uhai zaidi na afya njema Rais Samia, akisisitiza pia umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuilinda amani ya Tanzania ili kutoa fursa ya Taifa na kila mwananchi kupiga hatua za kimaendeleo.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger