Jeshi la Magereza nchini limesema kauli na taarifa za baadhi ya viongozi wa CHADEMA zilizoenezwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kulituhumu jeshi hilo kwa utendaji wake ni za kupuuza na hazina mashiko yoyote.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dodoma jana majira ya jioni Machi ,13,2020,eneo la Gereza la Isanga ,mrakibu wa jeshi la Magereza S.S.P Amina Kavirondo alisema gereza ni sehemu salama na mtu anapokelewa kama watu wengine hivyo mfungwa anapoingia gerezani anatakiwa awe salama na anatoka salama hivyo kukaguliwa ni jambo la muhimu bila kujali cheo chake.
“Jukumu letu kama jeshi la magereza ni kumkagua mfungwa pindi anapoingia gerezani ili ku- protect[kulinda]usalama wake na gereza kwa ujumla maana anaweza kuingia na kitu chochote kinachoweza kudhuru na hili halifanywi kwao tu kama viongozi wa CHADEMA linafanywa na kila mtu na utaratibu huu unafanyika maeneo mengi duniani ,kwa hiyo kauli wanazoeneza hazina msingi wowote”aLIsema.
Kuhusu vipigo S.S.P Amina aLIsema jeshi la Magereza lina sheria na taratibu zake hivyo haliwezi kumwonea mtu na endapo kutatokea mfungwa yeyote anataka kuhatarisha usalama wa wengine huwa kuna taratibu hufuatwa na mwanasiasa aliyesema wafungwa wanapokea kichapo hizo ni taarifa za kiharakati na zinapaswa kupuuzwa.
Katika hoja ya kujitosheleza kwa jeshi hilo S.S.P Amina amesema jeshi la Magereza kwa sasa linajitosheleza kwa chakula lakini kwa mahitaji mengine litahudumiwa na serikali kama vilivyo vyombo vingine vya ulinzi na usalama hivyo Mwanasiasa aliyesema jeshi hilo halijitoshelezi kwa chochote hoja yake haina msingi.
Pia amesema mfungwa ama mahabusu hupelekwa Mahakamani kwa Maamuzi na wito wa mahakama na tarehe husika na jeshi la magereza haliwezi kumpeleka mahakamani bila maamuzi na wito wa mahakama huku akisema Kwenye sakata la upimaji wa Afya S.S.P Amina amesema utaratibu wa kupimwa afya gerezani uko tofauti na hospitalini hivyo hoja ya mwanasiasa aliyelalamika kuwa magerezani wana pima VVU hadharani haina Mashiko.
0 comments:
Post a Comment