Sunday, 15 March 2020

Upelelezi Sakata la Halima Mdee, Bulaya na Wafuas wa CHADEMA kudaiwa Kuvamia Gerezani Wakamilika

...
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa, amesema kuwa wafuasi wa CHADEMA wakiongozwa na Halima Mdee na Ester Bulaya, walivamia kwa nguvu katika Gereza la Segerea, wakitaka kumtoa Mbowe bila kufuata utaratibu, hali iliyopelekea kumchania sare ya Jeshi Askari aliyekuwa lindo.

Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Machi 15, 2020, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kusema kuwa tayari upelelezi wa wafuasi 27 wa CHADEMA, umekwishakamilika na kesho watalipeleka jalada kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua zingine.

"Walikuwa na wafuasi wengi waliokuwa wamekusanyika kwenye geti la kuingilia Gerezani, na kutaka kulazimisha kuingia kwa nguvu, getini pale kuna ulinzi, walitumia nguvu, ambapo hata Askari aliyekuwa lindo alichaniwa sare yake, kwahiyo wao walitaka kwenda kumtoa Mwenyekiti wa chama hicho bila kukamilisha taratibu" amesema Kamanda Mambosasa.  

“Tulifika eneo la tukio na kukuta askari wa magereza wakiendelea kuwadhibiti wanachama hao ndipo polisi walipowakamata watuhumiwa 27 na kuwapeleka katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano.

“Baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeshakamilika,” ameongeza.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger