“Sina hofu na ndio maana nimerudi bila shida yoyote kwa sababu hamna kosa lolote nimefanyana ,nitaendeea kufanya shughuli zangu kama kawaida,.” alisema
Hivi karibuni Zitto Kabwe alitupiwa lawama nyingi na wabunge mbalimbali katika mkutano wa 18 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma kwa kitendo chake cha kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka isiidhinishe mkopo wa Sh1.2 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya sekta ya elimu.