Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , William Lukuvi amemsimamisha kazi ofisa ardhi wa Wilaya ya Kigamboni ambaye siku kadhaa zilizopita Rais Magufuli alitaka achukuliwe hatua kwa kuwa ni mtoro
Siku hiyo Magufuli alisema, “Nina tatizo na ofisa ardhi wa Kigamboni ni mtoro na hajafanya kazi karibu miezi mitatu, aliandikiwa barua na Wizara ya Ardhi ili ashughulikiwe ila bado wizara wanaleta mshahara wake. Najua wizara watafikishiwa ujumbe, kama ni mtoro atoroke kabisa, sifahamu mkurugenzi mmechukua hatua gani kwa ofisa ardhi huyo ambaye hafanyi kazi.”
Katika maelezo yake ya jana wakati akikabidhi ekari 715 za ardhi kwa manispaa ya Kigamboni kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, Lukuvi alisema mtumishi huyo amesimamishwa kazi.
"Bahati nzuri tulishapata barua kutoka kwa mkurugenzi wa Kigamboni na tumeshamsimamisha kazi wakati hatua za kinidhamu zikiendelea .Kama kutakuwa na uhitaji tutaleta mtu mwingine," alisema Lukuvi.
0 comments:
Post a Comment