Saturday, 29 February 2020

LIUNDI AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA WANAWAKE WALIOFANIKIWA KATIKA UONGOZI

...

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi amewataka Waandishi wa habari nchini kuwapa nafasi kwenye vyombo vya habari wanawake waliofanya vizuri katika masuala ya uongozi ili kuwapa hamasa wanawake wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi.


Liundi ameyasema hayo, leo Jumamosi Februari 29,2020 wakati wa Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa

"Lengo la warsha hii kujenga na kuongeza uelewa na uwezo wa waandishi wa habari kuripoti masuala ya kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uongozi. Hakikisheni mnawapa nafasi wanawake waliofanya vizuri katika uongozi ili kuhamasisha wanawake wengi zaidi wajitokeze kushiriki katika masuala ya uongozi na ngazi za maamuzi",alisema Liundi.

"Wale wanawake watakaojitokeza kugombea nafasi za uongozi wapeni nafasi kwenye vyombo vya habari,angalieni michango yao,itangazeni kwa jamii ili jamii iweze kuwaona. Kuna mifano bora ya wanawake ambao wamefanya vizuri sana katika masuala ya uongozi,wale mkiwa mnawapa nafasi ,basi jamii itaona wanawake wana uwezo mkubwa sana katika kufanya kazi",aliongeza Liundi.

Aliwataka waandishi wa habari kutumia mafunzo wanayopewa kujiimarisha katika kuripoti habari kwa mrengo wa kijinsia na kuhamasisha mila na desturi chanya.

"Tuongeze nguvu katika kuondoa mawazo mgando na mitazamo hasi,tuhakikishe tunapanda mawazo chanya wezeshi ili wanawake waweze kushiriki katika nafasi za uongozi na maamuzi kwa wingi zaidi. Wanawake na wanaume wakishiriki katika ngazi za maamuzi kwa pamoja,kuna tija kwani inasaidia kuchochea maendeleo katika jamii",alisema.

"Wanawake ni zaidi ya asilimia 51 ya wananchi wa nchi za Afrika, kwa hiyo hatuwezi kuiacha hii asilimia 51 isishiriki katika kutoa maamuzi,ni muhimu sana kwa wanawake kushiriki katika michakato ya maendeleo,kushiriki katika nafasi za uongozi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo",alisisitiza Liundi.

Naye Afisa Habari wa TGNP Monica John alisema vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kubadilisha mitazamo hasi dhidi ya wanawake katika jamii inayosababisha wanawake wasishiriki katika nafasi za uongozi.

John alisema kupitia warsha hiyo washiriki wataweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti masuala ya kijinsia katika vyombo vya habari hasa kusambaza ilani ya uchaguzi ya wanawake na kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akizungumza leo Jumamosi Februari 29,2020 wakati akifungua Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akizungumza katika Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akiwasisitiza waandishi wa habari kuwapa nafasi wanawake waliofanya vizuri katika masuala ya uongozi ili wanawake wengine waweze kuhamasisha kugombea nafasi za uongozi.

Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa. 
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa Warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Njombe,Shinyanga,Kigoma na Tabora baada ya kupata mafunzo Mwezi Septemba mwaka 2019 juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo Siasa. 
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akielezea namna vyombo vya habari vinanatakiwa kushirikishwa katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika masuala ya uongozi.
Mwandishi wa habari kutoka Redio Faraja mkoani Shinyanga, Anikazi Kumbemba akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari wa Star Tv mkoani Tabora, Mustapher Kapalata akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari kutoka Redio Faraja mkoani Shinyanga,Moshi Ndugulile akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari wa Redio Sachita mkoani Mara, Ahmad Macha akichangia mada wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Shinyanga wakifanya kazi ya Kikundi
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Mara wakifanya kazi ya Kikundi
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Tabora na Kigoma wakifanya kazi ya Kikundi.
Washiriki wa warsha kutoka mkoa wa Simiyu na Njombe wakifanya kazi ya Kikundi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger