Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli katika kikao cha kawaida cha Kamati hiyo kilichoketi leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Dar es salaam imeazimia kumfukuza uanachama Bernard Membe.
Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Yusuf Makamba, amesamehewa kutokana na kuomba kusamehewa makosa aliyokuwa akidaiwa kuyatenda ya kwenda kinyume na maadili ya chama hicho.
Aidha, Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana,amepewa adhabu ya kalipio kwa mujibu wa kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho.
0 comments:
Post a Comment