Sunday, 16 February 2020

Picha : MANGULA AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM SHINYANGA .....ATOA ONYO KALI WAGOMBEA CCM UCHAGUZI MKUU 2020



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula (kulia) akiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wakielekea kwenye kikao cha ndani kabla ya kwenda kuzungumza na wajumbe wa halmashauri kuu, na kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Philip Mangula amewaonya wagombea wa viti vya udiwani na ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kuwa wale ambao wataanza kampeni mapema kabla ya muda muafaka pamoja na kutoa zawadi mbalimbali watakatwa majina yao.

Mangula amebainisha hayo leo Februari 16,2020 kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu, na kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.

Amesema Chama Cha Mapinduzi CCM kina kanuni na taratibu zake hivyo wagombea wote wanapaswa kufuata kanuni na maadili ya chama.

Ametoa onyo kwa wagombea wote ambao wana nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kuwa wale ambao wataanza kampeni kabla ya muda hawatasita kukata majina yao.

“Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, tunataka taratibu, kanuni na ya chama zifuatwe kwenye kugombea nafasi za udiwani na ubunge, wale ambao wataanza kampeni kabla ya muda pamoja na kutoa zawadi tutafyeka majina yao, bali msubiri muda ukifika ndipo muanze kujinadi,” amesema Mangula.

“Tunataka nidhamu ndani ya chama, na hakuna jamii ambayo haina taratibu namna ya kuishi, hivyo kamati za siasa chungeni sana wagombea ambao wataanza kufanya kampeni kabla ya muda wachukulieni hatua, na mkishindwa sisi tutaiwajibisha kamati nzima,”ameongeza.

Pia amewataka wana CCM kuendelea kushikamana na kuwa wa umoja hasa kwenye kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, pamoja na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura, ili chama kipate ushindi wa kishindo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amemuhakikishia Mangula kuwa chama hicho kimejipanga vizuri kuelekea kwenye uchaguzi, ambapo hakuna hata kiti kimoja ambacho watakipoteza, kuanzia nafasi ya udiwani na ubunge, huku akiahidi kutekeleza maagizo ambayo ameyatoa ikiwamo wagombea kuanza kampeni kabla ya muda.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, amemuomba Mangula kupeleka salamu za pongezi kwa Rais John Magufuli, kutokana na kazi kubwa ambayo anaifanya, huku akibainisha namna alivyotekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ndani ya Miaka Mitano, kwa kufanya shughuli za kijamii kwa asilimia 80 ikiwamo sekta ya afya na elimu.

Pia amemuomba kwenda kulisemea tatizo la kutokamilishwa kwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga, ambapo mwaka 2018 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipofanya ziara mkoani Shinyanya alitoa ahadi ya kukamilisha hospitali hiyo, ambapo mwaka 2019 ingeanza kutoa huduma lakini hadi leo hakuna kinachoendelea huku majengo yakikaliwa na popo.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Capinduzi CCM Tanzania bara Philip Mangula, akisoma kanuni za chama leo Jumapili Februari 16,2020 wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu na kamati za siasa za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga. Alionya wagombea kuanza kampeni mapema kabla ya muda muafaka na atakaye kiuka atakatwa jina lake . Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Tanzania bara Philip Mangula, akiwataka wajumbe kuwa kitu kimoja hasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu  2020 ili chama kipate ushindi wa kishindo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula na kumuahidi ushindi wa kishindo uchaguzi mkuu na hakutakuwa na kiti hata kimoja kwenda upinzani iwe udiwani na ubunge.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa salamu za Serikali kwenye mkutano huo.

Mbunge wa viti maalum mkoa  Shinyanga Azza Hilal Hamad akiElezea namna alivyotekeleza Ilani ya Uchaguzi kwenye majimbo yote sita ya mkoa wa Shinyanga ikiwamo sekta ya afya na elimu.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele akielezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akielezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, akielezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, akielezea utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM kwenye Jimbo lake.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (wa kwanza kushoto), akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba katikati kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum (mwenye kofia) akiwa na wajumbe wengine kwenye mkutano wa makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.

Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philip Mangula akisalimiana na wajumbe mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kufanya mkutano, akisalimiana na mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum.


Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Philipo Mangula, akisalimiana na mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakar Mukadam.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara PhilipoMangula, akisalimiana na mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge.

Wajumbe wakitoa burudani kwenye mkutano huo, kwa kucheza nyimbo za CCM.

Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Share:

Ubalozi wa Marekani Iraq na Kambi ya Jeshi Wapigwa Tena Kwa Makombora

Makombora manne leo hii yamevurumishwa karibu na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad na kambi ya kijeshi ambayo inatumiwa na vikosi vya Marekani ndani la Ukanda wa Kijani. 

Hata hivyo hakuna athari kubwa zilizoripotiwa. Msemaji wa operesheni ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq, Kanali Myles B. Caggins, amesema mashambulizi hayo yalitokea majira ya tisa na nusu Alfajiri, na kuongeza kuwa yalipiga tu kambi inayohifadhi wanajeshi wa Marekani na wa muungano.

 Hata hivyo maafisa watatu wa usalama wa Iraq wamesema mawili kati ya makombora hayo yaliangukia katika eneo la ubalozi wa Marekani, wakati lingine likitua katika kambi ya jeshi la muungano.

 Maafisa hao wa Iraq waliyasema hayo kwa masharti ya kutotajwa majina kwa kuwa hawana mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.


Share:

Watumishi Wa Maliasi Watakiwa Kuhamishia Ofisi Katika Maeneo Ya Hifadhi Ili Kulinda Maliasili

NA TIGANYA VINCENT
WATUMISHI wa Mamlaka na Wakala zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wametakiwa kuhamia katika maeneo ya hifadhi ili kulinda na kuzuia uharibifu wa maliasili kwa ajili ya maendeleo ya Nchi.

Kauli hiyo imetolewa  na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Tabora , Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori(TAWA), Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi na Hifadhi za Taifa(TANAPA) kwenye ziara yake ya kikazi.

Alisema Taasisi zote zinahusika na usimamizi na ulinzi wa  maliasili zinatakiwa kujenga Ofisi ndani ya Hifadhi na watumishi kuhamia huko ili iwe rahisi kukabiliana na uharibifu wowote unaotaka kufanyika.
Dkt. Kigwangala aliongeza katika Ofisi zilizopo nje ya hifadhi wabaki watumishi wachache ikiwemo Watendaji wakuu na waliobaki waende porini kwa kuwa tayari walishapata mafunzo ya jinsi ya kupambana na waharibifu wa maliasili.

"Hatuwezi kulinda maliasili tukiwa maofisini ...ni lazima tujenge post kwenye hifadhi zetu na watumishi wahamie huko wakalinde maliasili zetu , ofisi wabaki wachache ikiwemo viongozi wa Kanda... wao watakwenda kukagua utendaji kazi wa watumishi wanaowasimamia" alisisitiza

Alisema ni jukumu lao kuhakikisha maliasili zilipo ikiwemo wanyamapori , ndege na mimea inalindwa kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kijacho na kuhakikisha wanazuia uharibifu wowote ndani ya Hifadhi nchini.

Waziri huyo alisema kuwa Kanda ya Magharibi ndio pekee imebaki na mistu mingi ya asili ni vema watendaji wanaohusika kulinda na kuhifadhi wakahakikisha haiendelei kuharibiwa.

Katika hatua nyingine Dkt. Kigwangala ametoa siku 14 kwa Taasisi zilizopo chini Wizara ya Maliasili na Utalii katika kanda ya Magharibi kukaa pamoja na kuanisha mipaka halisi ya Hifadhi mpya za Taifa, mapori ya akiba na Hifadhi ya Mistu  na maeneo ya wananchi ili kuondoa mwingiliano na migogoro.

Alisema kumekuwepo na mlingiliano ambao umetokana na baadhi ya maeneo ya hifadhi moja kusomeka katika eneo jingine la hifadhi na kuleta utata.

Aidha Dkt. Kigwangala alizitaka Taasisi hizo kuhakikisha wanaweka upya mipaka katika Msitu wa Hifadhi wa Ulyankulu ambapo kuna sehemu ambayo wananchi wameshavamia na kufanya makazi na kujenga huduma mbalimbali.

Alisema mipaka hiyo itasaidia wananchi kuendelea kuingia katika msitu huo na kuendesha shughuli mbalimbali ambazo zinatishia uendelevu wa msitu huo.

Mwisho


Share:

Watakao Tumia Rushwa Uchaguzi Mkuu CWT ,kunyang’anywa Ushindi

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa chama cha walimu Tanzania CWT utakao anza mapema mwezi  Februari hadi Mei mwaka huu , Rais wa Chama hicho Mwalimu Leah Ulaya amewatahadharisha wanachama watakao gombea kujiepusha na vitendo vya rushwa na atakayekiuka maadili ya chama kuhusu uchaguzi atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kunyang'anywa ushindi

Akizungumza  na Waandishi wa Habari  leo Februari 16,2020 Jijini Dodoma katika Makao Makuu ya Chama hicho, Ulaya amesema kuwa chama kinapinga kwa nguvu zote matumizi ya  fedha ,Rushwa na uvunjaji wa Maadili .

“Nitoe wito wanachama  wote wa Chama cha Walimu Tanzania[CWT]kuwa ni wajibu wa kila mmoja  kushiriki katika uchaguzi wa viongozi mbalimbali Wa CWT ila nitahadharishe tu katika masuala ya rushwa katika uchaguzi huu na rushwa ni adui wa haki hivyo ni lazima tupinge kwa nguvu zote,na kingine ambacho nataka niwasisitize Walimu wenzangu ni kuendelea kuilinda amani na uzalendo kwa nchi yetu”amesema.

Akitoa Ratiba  ya  Uchaguzi huo ,  Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Deus Seif , amesema kwa Mujibu wa katiba ya CWT chama kinawataka  kufanya chaguzi zao kila baada ya Miaka mitano hivyo, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kwa chama chao.

“Ngazi ya Tawi [sehemu ya kazi]utachaguzi unafanyika kuanzia tarehe 15-27  Februari ,2020 ,chaguzi hizi zitafanyika katika shule,vyuo vya ualimu[TTC],Vyuo vya maendeleo ya Jamii[FDC’s]Wizara na Taasisi mbalimbali zenye wanachama  pamoja na taasisi zilizo ngazi ya wilaya zinazojumuisha ofisi za Elimu za wilaya na waratibu   wa elimu ngazi kata”amesema.

Katika ngazi ya wilaya uchaguzi utafanyika kuanzia Tarehe 16 -27 Machi,2020 na ratiba ya uchukuaji  na urejeshaji fomu  itapangwa na kamati ya uendeshaji ya wilaya husika.

Ameendelea kufafanua kuwa uchaguzi ngazi ya Mkoa utafanyika kuanzia Tarehe 20 -30 April,2020 na ratiba ya uchukuaji na kurejesha fomu itapangwa na kamati tendaji ya mkoa.

Akizungumzia kwa ngazi ya Taifa Seif amesema mkutano mkuu wa Taifa utafanyika  Mei 27-28 mwaka huu,ambapo uchaguzi wa ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 28  Mei mwaka huu na wagombea watajulishwa mahali pa mkutano kabla ya mkutano mkuu wa uchaguzi huku utaratibu wa kuwa na wawakilishi wa makundi Maalumu kama  vile walimu wanawake na walimu wenye ulemavu watapewa kipaumbele zaidi.

Nafasi zinazogombewa  ambapo ngazi ya tawi [sehemu ya kazi]katibu wa chama,ngazi ya Wilaya ni Mwenyekiti    wa CWT Wilaya,Mweka hazina CWT Wilaya,mwakilishi wa walimu wanawake CWT Wilaya,mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu  CWT wilaya, mwakilishi vijana[miaka 18-35]CWT  wilaya, na wawakilishi wa walimu wanaofundisha shule za awali,msingi,sekondari,shule/vyuo vya serikali,vyuo vya walimu,vyuo vya maendeleo ya jamii[FDC’s]na Taasisi za elimu za serikali zinazowajumuisha waratibu wa elimu kata,waratibu wa TRC’s na walimu maafisa ngazi za wilaya.

Nafasi zinazogombewa ngazi ya mkoa ni mwenyekiti  CWT mkoa,mweka hazina CWT mkoa,mwakilishi wa walimu wanawake CWT mkoa,mwakilishi wa walimu wenye ulemavu CWT mkoa, mwakilishi wa vijana CWT mkoa,mwakilishi wa wenyeviti wa wilaya kwenye baraza la Taifa,mwakilishi wa mkoa kwenye kamati tendaji ya Taifa na wawakilishi wa CWT Kwenye vikao vya TUCTA .

Na nafasi zinazogombewa ngazi ya Taifa ni Rais wa Chama,Makamu wa Rais,Katibu Mkuu,Naibu katibu mkuu,Mweka Hazina wa Taifa,mwakilishi wa walimu wenye ulemavu kwenye kamati tendaji ya taifa ,mwakilishi wa walimu wanawake kwenye kamati tendaji ya Taifa,mwakilishi wa vijana[18-35] kwenye kamati tendaji ya taifa pamoja na pamoja na wadhamini watatu[3]wa chama.

Hivyo,CWT Kimetoa wito kwa wanachama wake hasa wanawake walimu na wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kugombea  nafasi mbalimbali huku wakiwashauri wanachama kusoma kwa makini katiba ya CWT Toleo la 6 la mwaka 2014,kanuni za chama Toleo la 4 la mwaka 2015.


Share:

Watumishi Wizara Ya Mambo ya Nje Watakiwa Kuchapa Kazi Kwa Bidii na Ushirikiano

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Katibu Mkuu mpya, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge. 
 
Mhe. Prof. Kabudi ametoa rai hiyo jana jijini Dodoma wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilitoo fursa ya kutakiana heri ya mwaka mpya 2020 na kumkaribisha Wizarani Katibu Mkuu Mpya, Balozi Kanali Ibuge  kilichofanyika 
 
Aidha, mhe. Prof. Kabudi aliwaeleza watumishi hao kuwa, mwanzo wa mwaka ni kipindi kizuri cha kujipanga na kuweka mikakati ya namna bora ya kutekeleza majukumu  kwa ajili ya maendeleo ya Taifa ikiwa ni pamoja na kufahamu vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Joseph Pombe Magufuli.
 
Kadhalika amewataka kufanya kazi kwa bidii, kujitambua na kujenga umoja  na ushirikiano katika kutekeleza majukumu hayo kikamilifu.
 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge ameahidi ushirikiano kwa watumishi wa Wizara na kuwakumbusha kuwa kila mmoja ana wajibu mkubwa wa kuchangia maslahi mapana ya Taifa ili mradi kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa kuendelea kujituma, kuwa tayari kurekebishwa, kuwa watiifu na kuwa tayari kupokea maelekezo.
 
"Watumishi wenzangu, kila mmoja hapa ana mchango mkubwa kwa maslahi ya Taifa letu. Ninasisitiza kuwa mwendelee kujituma, kufanya kazi kwa weledi, kuwa watiifu, kuwa tayari kurekebishwa na kuwa tayari kupokea maelekezo. Binafsi nitaendelea kutoa usikivu kwenu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu" alisema Balozi Ibuge. 
 
Kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili Wizara, Balozi Kanali Ibuge amewataka Watumishi wote kushirikiana kuzitatua kwani hakuna changamoto ya kudumu endapo Watumishi wote watakuwa kitu kimoja.


Share:

Waziri Mkuu Majaliwa Kasema Leo Jumapili Kuwa Watanzania Waliopo Wuhan nchini China Wapo Salama

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vijana wa Tanzania wapatao 497 wanaosoma katika vyuo mbalimbali vilivyoko kwenye mji wa Wuhan nchini China wote wapo salama.

Kwa sasa Mji wa Wuhan umewekewa zuio hakuna mtu anayeruhusiwa kutoka wala kuingia, lengo likiwa ni kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo. Mlipuko wa virusi vya corona ulianzia katika mji wa Wuhan.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Februari 16, 2020) kwenye Kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam iliyoandaliwa na Nida Textile Mills (T) ltd, na kufanyika katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar-es-Salaam. Watu zaidi ya 1,500 wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa virusi hivyo.

Waziri Mkuu amesema kutokana na zuio hilo wakazi wote wa mji huo wakiwemo vijana wa Kitanzania wanapata huduma mbalimbali kupitia njia ya mtandao ukiwemo ununuzi wa bidhaa mbalimbali.

“…Hakuna usafiri hata wa umma unaofanya shughuli za kusafirisha watu katika mji wa Wuhan kila mmoja anaetakiwa abakie katika makazi yake na kwamba Serikali ya China na uongozi wa vyuo unawatunza wanafunzi wote wakiwemo na Watanzania.”

Waziri Mkuu amesema kwamba kwa sasa Wachina wameimarisha utoaji huduma kwa njia ya mtandao hata kama mtu anataka kununua kitu ananunua kwa njia ya mtandao. “Kama kijana ameishiwa basi atumiwe fedha kwa njia ya mtandao ili aweze kujikimu wakati huu wa zuio.”

Waziri Mkuu amesema jambo la muhimu kwa sasa ni usalama wao na kujali maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya China juu ya usalama wao pamoja na wananchi wengine walioko katika eneo hilo.

Amesema Serikali imeweka mitambo ya kupima watu katika maeneo yote ya mipaka na kwamba inawataka wananchi washirikiane nayo katika kuhakikisha watu wote wanaoingia nchini wanapita kwenye njia sahihi.

Pia, Waziri Mkuu amerua kuwataka Watanzania waendelee kuwa watulivu na kuitegemea Serikali katika kupata taarifa za mara kwa mara kuhusu masuala mbalimbali zikiwemo na ya mlipuko wa virusi hivyo.

(MWISHO)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Waziri Mkuu: Tutaendelea Kushirikiana Na Madhehebu Yote Nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua na kuheshimu dini zote nchini,hivyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa madhehebu yote katika kutunza na kulinda amani.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Februari 16, 2020) kwenye Kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam iliyoandaliwa na Nida Textile Mills (T) ltd, na kufanyika katika mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar-es-Salaam.

Amesema amani ndiyo msingi wa kila binadamu kufurahia maisha ya dunia na kufanya ibada zake kulingana na imani yake. “Kwa hiyo,tunapoazimisha mazazi ya Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam, tuna kila sababu ya kumuenzi kwa kufuata mafundisho yake.“

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Serikali kwa upande wake inatambua na itaendelea kuthamini, mchango wa dini, taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na hata mtu mmoja mmoja katika kutunza na kulinda amani ya nchi yetu.

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi wa dini zote na jamii kwa ujumla waendelee kuvumiliana na kustahamiliana hususan pale zinapotokea tofauti miongoni mwao, lengo likiwa ni kudumisha amani na ulivu uliopo nchini.

“Kuvumiliana na kustahamiliana ndiko kulikotufanya tuendelee kuwa wamoja na kuitunza neema hii kubwa ya amani katika nchi yetu. Kila mmoja wetu anapaswa kutambua kuwa anao mchango mkubwa katika kutunza na kuimarika kwa amani ya nchi yetu.”

Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo ya Mazazi ya Mtume Muhammad (S. A. W), Waziri Mkuu amesema kwamba hiyo ni fursa muhimu kwa waislamu wote kuyasoma na kuyatafsiri kwa kivitendo maisha ya Bwana Mtume katika mfumo wao wa maisha ya kila siku ili kuyafanya maisha yao hapa duniani yawe bora zaidi.

“Tukio hili la leo ambalo nimefahamishwa kuwa linafanyika kwa mwaka wa 25 sasa, ni kielelezo cha umoja, mapenzi na undugu miongoni mwetu. Katika Quran Surah ya 49 (Al-Hujurat) ayah ya 10, Mwenyezi Mungu anatufahamisha kuwa ’hakika waumini ni ndugu.......’ Kwa msingi huo, tukiwa Waislamu suala la kuimarisha umoja, undugu na ushirikiano katika nyanja zote ni wajibu wa kila mmoja wetu.“

Kadhalika, Waziri Mkuu ameongeza kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) naye katika kusisitiza suala hilo la umoja, kwenye hotuba yake ya kuaga alihimiza kuwa mtu yeyote yule hawezi kuwa bora dhidi ya mwingine kwa sababu tu ya rangi yake au kabila lake lakini kitu pekee kitakachompa yeye daraja hilo la kuwa bora ni kutenda haki na kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Awali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakari Bin Zuberi alisema katika kuadhimisha Mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) waislamu nchini wanapaswa waendelee kuwa watulivu na wasikivu wa kila jambo linalotolewa kwao na viongozi.

Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na masheikh na viongozi wa Serikali kutoka maeneo mbalimbali nchini. Pia yamehudhuriwa na masheikh kutoka nchi za Paksani, Iraq na Misri ambao kwa ujumla wao wameisifu Serikali ya Tanzania kwa kudumisha amnai, utulivu pamoja na umoja.

(MWISHO)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

Executive Assistant at School of St. Jude

Job Summary We are looking to appoint an Executive Assistant to provide support to and work directly for the Academic Manager. The ideal candidate will have a passion for community development and a strong interest in NGOs. Minimum Qualification: Bachelor Experience Level: Mid level Experience Length: 2 years Job Description Ref: TSOSJ/HR/AM/01/2020 Duty Station: Moshono Business Office, Arusha, Tanzania (travel between campuses is… Read More »

The post Executive Assistant at School of St. Jude appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jobs at EWURA – Water Quality Analyst

Water Quality Analyst   The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an independent, world class regulatory authority responsible for licensing, tariff regulation and quality of service regulation of the electricity, water, petroleum and Natural gas sectors. EWURA has the following vacancies for which suitably qualified Tanzanian citizens are invited to apply. WATER AND SANITATION DIVISION Post Title… Read More »

The post Jobs at EWURA – Water Quality Analyst appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Information and Communications Technology Officer at EWURA

Information and Communications Technology Officer   The Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is an independent, world class regulatory authority responsible for licensing, tariff regulation and quality of service regulation of the electricity, water, petroleum and Natural gas sectors. EWURA has the following vacancies for which suitably qualified Tanzanian citizens are invited to apply. DIRECTOR GENERAL’S OFFICE Post… Read More »

The post Information and Communications Technology Officer at EWURA appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Nafasi Mpya Za Kazi SERIKALINI...Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 26 Mwezi huu

Share:

Job at Uchumi Commercial Bank – Bank Operations & Business Development Manager

UCHUMI COMMERCIAL BANK LTD UCB Vision is to become premier provider of banking services. Mission “To provide efficient, affordable and convenient banking services, promote Member-based Organizations (MBOs) and address the financial needs of under banked people in Tanzania. UCB is seeking a dedicated, self-motivated and highly organized BANK OPERATIONS AND BUSINESS DEVELOPMENT MANAGER to join at Uchumi Commercial… Read More »

The post Job at Uchumi Commercial Bank – Bank Operations & Business Development Manager appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Jobs at Braeburn schools – School Nurse

SCHOOL NURSE BRAEBURN SCHOOLS (TANZANIA) LIMITED is seeking a highly motivated, professional Nurse to work in our Dar es Salaam campus. The ideal candidate must be trained in paediatrics and be fluent in English and Kiswahili. Experience working in an International school is advantageous. Head of Admin at Danish Embassy February, 2020 Interested applicants should send a letter… Read More »

The post Jobs at Braeburn schools – School Nurse appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

15 Job vacancies at Aga Khan Health Service Tanzania (AKHST)

Overview: The Aga Khan Health Service, Tanzania (AKHST) an institution of The Aga Khan Development Network, has completed a major expansion of the Aga Khan Hospital, Dar es Salaam. This expansion aims at enhancing the Hospital’s facilities, technology and capacity which will allow it to become the leading provider of high-quality medical care focusing on tertiary medicine, reversing… Read More »

The post 15 Job vacancies at Aga Khan Health Service Tanzania (AKHST) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Teaching jobs DSM at ABC Capital School Nursery and Primary

NURSERY TEACHERS NEEDED Company: Reputable School Location: Tanzania State: Dar Es Salaam Jobs Job type: Full-Time Job category: Education/Teaching Jobs in Tanzania Job Description ABC PRIMARY AND NURSEY SCHOOL IS LOOKING FOR THE COMPETENT NURSERY TEACHERS, THE REQUIRED TEACHERS SHOULD HAVE THE FOLLOWING ABILITY AND QUALIFICATION: DIPLOMA IN EARLY CHILDHOOD EDUCATION CERTIFICATE IN ORDINARY LEVEL SECONDARY SCHOOL EXPERIENCE… Read More »

The post Teaching jobs DSM at ABC Capital School Nursery and Primary appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

IDADI YA WATALII HIFADHI YA TAIFA YA SAADAN WAONGEZEKA

 Sehemu ya wanyama aina ya Pundamilia wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani
 Mnyama aina ya Mamba akiwa pembezoni mwa Mto Wami unapita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan akiota jua
 Wanyama aina ya Twiga wakijivinjari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan kama walivyokutwa
 Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakila majani
 Sehemu ya watalii wakiwa kwenye gari la wazi wakifanya utalii ndani ya hifadhi hiyo kama walivyokutwa


 Mnyama aina ya Ngiri akila majani pembezoni mwa Bahari kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani
 Mnyama aina ya Kiboko akiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao unapita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama walivyokutwa
 Makundi ya ndege wakiwa wamejenga viota vyao ndani ya Mto Wami kwenye miti ili kujiepusha na maadui zao kama wanavyoonekana
IDADI ya Watalii wanaokwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan imeelezwa imekuwa ikiongezeka kutoka 3750 mwaka 2005 hadi kufikia 22890 mwaka 2018.

Hayo yamebainishwa na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae wakati akielezea mafanikio ya Hifadhi hiyo tokea ilipoanzishwa kwake huku akieleza idadi hiyo imekuwa ikipanda mwaka hadi mwaka.

Alisema hicho ni kiwango kikubwa kilichoifanya hifadhi hiyo iendelee kukua kutokana na uwepo wa vivutio vyingi vya utalii ikiwemo upekee wa hifadhi na zilivyo nyengine hapa nchini.

Akizungumzia mafanikio ya kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli tokea mwaka 2015 alisema idadi ya wageni imepanda kutoka 15000 na kufikia idadi ya wageni 22920 ambapo ni ongezeko la wageni 7900.

Afisa Utalii huyo alisema kwamba ongezeko hilo limetokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza kwenye ununuzi wa ndege jambo ambalo linakuza utalii.

Alieleza kwamba uwekezaji huo wa ndege umesaidia kwa asilimia kubwa watalii kutoka kwenye nchi zao na kutua moja kwa moja nchini na hivyo kutokutumia muda mwingi.

Akielezea shughuli za utalii zinazofanyika kwenye hifadhi hiyo alisema kwamba ni utalii wa kutembea na magari hifadhini,utalii wa matembezo ambapo mtalii anakuwa na askari kwa ajili ya usalama ambapo unatoa fursa wageni kuona wanyama kwa ukaribu sana.

Aliongeza aina nyengine ya utalii ni utalii wa usiku ambapo wanyama awengine jamii ya Paka huwezi kuwaona mchana maana wanakuwa wamepumzika wakiwemo Simba, Chui, Fisi ambao usiku mara nyingi wanaweza kuonekana.

Hata hivyo alisema kwamba kwenye hifadhi hiyo wana wanyama wakubwa wanne ambao huitwa Big 4 ambao ni Nyati, Tembo, Simba, Chui na mnyama ambaye anakosekana ni Faru.

“Lakini hivi sasa niwaambie kwamba wageni wanaoongoza kutembelea hifadhi yetu ni kutoka nje ya nchi za Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Marekani,wa Rusia na baadhi ya nchi za ulaya huku akieleza masoko mapya ambayo yameibuka sasa ni Israel,Wahindi ,Wachina”Alisema

Share:

Tahadhari Kwa Waishio Pembezoni Mwa Mikondo Ya Maji Ya Bwawa La Mtera Na Kidatu

TAARIFA YA TAHADHARI KWA WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA MKONDO WA MAJI YATOKAYO KWENYE VYANZO VYA KUFUA UMEME KWA MAJI VYA MTERA NA KIDATU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa taarifa kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha bwawa la Mtera limejaa kwa kiwango cha juu na kina cha maji kimepanda hadi kufikia mita 698.50 juu ya usawa wa bahari na hivyo kulazimu ziada inayoendelea kuingia kuanza kutolewa kupitia milango mahususi kuanzia  Februari 15, 2020 kwa ajili ya usalama wa Mabwawa na Mitambo.

Aidha, wastani wa mita za ujazo 1,200 kwa sekunde kinaendelea kutiririka bwawani.

TANESCO inaendelea kutoa tahadhari kwa Wananchi hususani wale wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile Uvuvi, kulisha Mifugo, Kilimo na shughuli nyingine kwenye mkondo wa mto, vidimbwi au pembezoni mwa bwawa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu, kijamii na kiuchumi kwa kipindi hiki ambacho mvua za Vuli zikiwa zinaendelea kunyesha.

TANESCO itaendelea kutoa taarifa kadri hali ya kuruhusu ziada ya maji kupita upande wa pili itakavyokuwa inaendelea.

Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger