Sunday, 16 February 2020

IDADI YA WATALII HIFADHI YA TAIFA YA SAADAN WAONGEZEKA

...
 Sehemu ya wanyama aina ya Pundamilia wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani
 Mnyama aina ya Mamba akiwa pembezoni mwa Mto Wami unapita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan akiota jua
 Wanyama aina ya Twiga wakijivinjari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan kama walivyokutwa
 Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan wakila majani
 Sehemu ya watalii wakiwa kwenye gari la wazi wakifanya utalii ndani ya hifadhi hiyo kama walivyokutwa


 Mnyama aina ya Ngiri akila majani pembezoni mwa Bahari kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani
 Mnyama aina ya Kiboko akiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao unapita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani kama walivyokutwa
 Makundi ya ndege wakiwa wamejenga viota vyao ndani ya Mto Wami kwenye miti ili kujiepusha na maadui zao kama wanavyoonekana
IDADI ya Watalii wanaokwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan imeelezwa imekuwa ikiongezeka kutoka 3750 mwaka 2005 hadi kufikia 22890 mwaka 2018.

Hayo yamebainishwa na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae wakati akielezea mafanikio ya Hifadhi hiyo tokea ilipoanzishwa kwake huku akieleza idadi hiyo imekuwa ikipanda mwaka hadi mwaka.

Alisema hicho ni kiwango kikubwa kilichoifanya hifadhi hiyo iendelee kukua kutokana na uwepo wa vivutio vyingi vya utalii ikiwemo upekee wa hifadhi na zilivyo nyengine hapa nchini.

Akizungumzia mafanikio ya kipindi cha miaka minne ya Rais Magufuli tokea mwaka 2015 alisema idadi ya wageni imepanda kutoka 15000 na kufikia idadi ya wageni 22920 ambapo ni ongezeko la wageni 7900.

Afisa Utalii huyo alisema kwamba ongezeko hilo limetokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza kwenye ununuzi wa ndege jambo ambalo linakuza utalii.

Alieleza kwamba uwekezaji huo wa ndege umesaidia kwa asilimia kubwa watalii kutoka kwenye nchi zao na kutua moja kwa moja nchini na hivyo kutokutumia muda mwingi.

Akielezea shughuli za utalii zinazofanyika kwenye hifadhi hiyo alisema kwamba ni utalii wa kutembea na magari hifadhini,utalii wa matembezo ambapo mtalii anakuwa na askari kwa ajili ya usalama ambapo unatoa fursa wageni kuona wanyama kwa ukaribu sana.

Aliongeza aina nyengine ya utalii ni utalii wa usiku ambapo wanyama awengine jamii ya Paka huwezi kuwaona mchana maana wanakuwa wamepumzika wakiwemo Simba, Chui, Fisi ambao usiku mara nyingi wanaweza kuonekana.

Hata hivyo alisema kwamba kwenye hifadhi hiyo wana wanyama wakubwa wanne ambao huitwa Big 4 ambao ni Nyati, Tembo, Simba, Chui na mnyama ambaye anakosekana ni Faru.

“Lakini hivi sasa niwaambie kwamba wageni wanaoongoza kutembelea hifadhi yetu ni kutoka nje ya nchi za Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Marekani,wa Rusia na baadhi ya nchi za ulaya huku akieleza masoko mapya ambayo yameibuka sasa ni Israel,Wahindi ,Wachina”Alisema

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger