Sunday, 16 February 2020

Tahadhari Kwa Waishio Pembezoni Mwa Mikondo Ya Maji Ya Bwawa La Mtera Na Kidatu

...
TAARIFA YA TAHADHARI KWA WANANCHI WANAOISHI PEMBEZONI MWA MKONDO WA MAJI YATOKAYO KWENYE VYANZO VYA KUFUA UMEME KWA MAJI VYA MTERA NA KIDATU

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa taarifa kuwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha bwawa la Mtera limejaa kwa kiwango cha juu na kina cha maji kimepanda hadi kufikia mita 698.50 juu ya usawa wa bahari na hivyo kulazimu ziada inayoendelea kuingia kuanza kutolewa kupitia milango mahususi kuanzia  Februari 15, 2020 kwa ajili ya usalama wa Mabwawa na Mitambo.

Aidha, wastani wa mita za ujazo 1,200 kwa sekunde kinaendelea kutiririka bwawani.

TANESCO inaendelea kutoa tahadhari kwa Wananchi hususani wale wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile Uvuvi, kulisha Mifugo, Kilimo na shughuli nyingine kwenye mkondo wa mto, vidimbwi au pembezoni mwa bwawa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu, kijamii na kiuchumi kwa kipindi hiki ambacho mvua za Vuli zikiwa zinaendelea kunyesha.

TANESCO itaendelea kutoa taarifa kadri hali ya kuruhusu ziada ya maji kupita upande wa pili itakavyokuwa inaendelea.

Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger