Monday, 24 December 2018

SUMAYE AGEUKA KUWA “MBOGO” AIBUKA NA KUDAI DEMOKRASIA INAKUFA

NA KAROLI VINSENT WAZIRI Mkuu Mstaafu,Fredrick Sumaye ameibuka na kuuponda Mswaada wa vyama vya siasa kwa kusema umekuja kuiizika Demokrasia pamoja na Mfumo wa Vyama vingi. Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Amesema endapo wabunge wa CCM wakitumia wingi wao na kuupitishwa muswada huo aliouita ni “hatari” basi demokrasia itakufa hadi ndani ya chama chao kwa kuwa mtu mmoja ndiye atakuwa na mamlaka ya kuamua wagombea wa…

Source

Share:

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU AVIWASHIA UMEME VIJIJI VINGINE ZAIDI

Hapo jana tarehe 24.12.2018 Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amewasha umeme katika Kijiji cha Kilangalanga kilichopo kata ya Mtongani ndani ya halmashauri ya mji wa Mlandizi mkoani Pwani na kutoa maagizo kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwaunganishia umeme wateja wote waliolipia huduma hiyo. Ametoa maagizo hayo wakati akiwa ziarani Mlandizi, Pwani ambapo amewasha umeme kwenye kijiji cha Kilangalanga halmashauri ya mji wa Mlandizi,kabla ya tukio hilo la kuwasha umeme Mgalu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho kuwa wameshalipa fedha za kuunganishiwa umeme lakini mpaka sasa…

Source

Share:

SERIKALI YAANGUKIA “PUA” KWENYE KESI HII YA RUSHWA KUHUSU WAZIRI HUYU

NA KAROLI VINSENT SERIKALI  imeangukia “pua” tena kwenye kesi inayohusu masuala ya Rushwa baada ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemuachia huru, Mohamed Kiluwa (50) aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa sababu ushahidi wa mashtaka ulikuwa wa hisia. Akisoma hukumu hiyo leo Jumatatu Desemba 24, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Samuel Obas amesema ushahidi uliotolewa na upande wa Serikali haukuwa na mashiko kwa sababu umeshindwa kuthibitisha kosa. “Ushahidi wa upande wa mashtaka…

Source

Share:

UVCCM YAUCHAMBUA NA KUUSIFU “USHUJAA” WA RAIS MAGUFULI.

  24, Disemba, 2018. Umoja wa Vijana  Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa leo mbele ya waandishi wa habari wamezungumzia utendaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano(5) inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu. Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za Umoja huo jijini Dar es salaam katibu mkuu wa Umoja wa vijana CCM Taifa mwl. Raymond Mwangwala amesema mpaka sasa Serikali ya chama cha Mapinduzi chini ya Rais Dkt Magufuli imefanya utekelezaji mkubwa wa mambo mbalimbali ya maendeleo…

Source

Share:

BASATA YAWALEGEZEA ADHABU DIAMOND NA RAYVANNY...YAWAFUNGULIA KUPIGA SHOW NJE YA NCHI

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limemruhusu msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Raymond Mwakyusa ’Rayvanny’ kufanya maonyesho yao nchini Kenya na Comoro ingawa rufaa yao itajadiliwa Februari mwakani.

Katika ratiba zake, Diamond na wasanii wake wataendelea na onyesho la Tamasha la Wasafi ambapo leo Desemba 24 watakuwa katika mji wa Embu, kabla ya kuhamia jiji la Mombasa Desemba 26 na kuelekea Comorro kwa shoo ya Desemba 28 na kumalizia Nairobi Desemba 31, 2018.

Diamond na Rayvanny walifungiwa Desemba 18, 2018 kutofanya maonyesho ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali tangu kuanza kwa Tamasha la Wasafi ikiwemo kuimba wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa.

Pamoja na hilo siku tatu zilizopita waliendelea kutangaza kuendelea na maonyesho hayo pamoja na Basata kueleza hawajawaruhusu.

Katibu wa baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema sababu ya kuwaruhusu ni baada ya kikao kilichoketi leo na kujadili maombi yao kuomba kusamehewa huku moja ya jambo walilolibaini ni kwamba wasanii hao walikuwa wameshaingia mkataba wa kufanya maonyesho hayo kabla ya kupewa adhabu.

“Pia kwa kuzingatia mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na nyingine na athari kwa mashabiki wa nchi hizo ambao tayari walishakata tiketi za maonyesho hayo, Basata imewaondolea katazo la maonyesho hayo ya nje na kubakiza katazo la ndani ya nchi hadi pale Diamond na mwenzake Rayvany watakapoonyesha mabadiliko chanya kitabia,” amesema

Wakati kuhusu kukata rufaa, Mngereza amekiri wameipokea na kueleza wamewasiliana na mwenyekiti wa bodi ambapo suala lao hilo litajadiliwa kwa kina katika kikao cha kawaida cha bodi cha Februari 5 mwakani.

Share:

SERIKALI KUWAWEZESHA KIUCHUMI VIJANA KWENYE SEKTA YA UVUVI ILI KUONGEZA FURSA ZA AJIRA.

  Serikali kupitia mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi imedhamiria kuwawezesha vijana kwenye sekta ya uvuvi kwa kuwapatia mikopo ya nyenzo za uvuvi na mitaji ili Vijana wengi zaidi washiriki kwenye sekta ya uvuvi halali hali itakayopelekea ongezeko na nafasi zaidi za Ajira hususani kwa Vijana.   Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe Anthony Mavunde wakati akiongea na Vijana katika kata za Chato kati na Muganza,Wilayani Chato,Geita ambapo Mavunde alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Vijana kuunda Vikundi vya Uzalishaji mali ili kuwa na…

Source

Share:

YANGA YAIADHIBU TUKUYU STARS......TAMBWE ATAKATA , BOBAN AISHIA NJIANI


Kikosi cha Yanga katika mchezo wa leo

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tukuyu Stars katika uwanja wa taifa na kusonga mbele hatua ya 32 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Amissi Tambwe ambaye amefunga hat-trick katika dakika ya 14, 36 na 55 huku bao la mwisho likifungwa na Heritier Makambo katika dakika ya 88.

Pia mchezho huo ulikuwa ni wa kwanza kwa kiungo mpya wa klabu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili mwezi huu kutokea KMC.

Hata hivyo Boban hakuweza kumaliza mchezo, ambapo alitolewa dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza kutokana na majeraha.

Yanga inasonga mbele hatua ya 32 bora ya michuano hiyo, ikiungana na kigogo Azam FC ambaye alicheza mchezo wake jana Desemba 23 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Share:

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU AVIWASHIA UMEME VIJIJI VINGINE ZAIDI

Hapo jana tarehe 24.12.2018 Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu amewasha umeme katika Kijiji cha Kilangalanga kilichopo kata ya Mtongani ndani ya halmashauri ya mji wa Mlandizi mkoani Pwani na kutoa maagizo kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwaunganishia umeme wateja wote waliolipia huduma hiyo. Ametoa maagizo hayo wakati akiwa ziarani Mlandizi, Pwani ambapo amewasha umeme kwenye kijiji cha Kilangalanga halmashauri ya mji wa Mlandizi,kabla ya tukio hilo la kuwasha umeme Mgalu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho kuwa wameshalipa fedha za kuunganishiwa umeme lakini mpaka sasa…

Source

Share:

SUMAYE AWACHONGANISHA CCM

Baraza Kuu la Chadema Kanda ya Pwani limetoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua watu walioanzisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya au wanaokwamisha mchakato huo, likidai kuwa uamuzi huo umepoteza fedha za umma.

Akitoa maazimio ya baraza hilo, leo tarehe 24 Desemba 2018 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema kama mchakato huo ulioanzishwa na serikali ya CCM ya awamu ya nne haukuwa uamuzi sahihi, wahusika wachukuliwe hatua kwa ubadhirifu wa fedha za umma.

“Kama mchakato wa katiba ulioanzwa na serikali ya CCM ya awamu ya nne haukuwa uamuzi sahihi, wa serikali uliokuwa na Baraka za chama hicho tawala, sababu fedha zetu zimepoteza nyingi basi wahusika wachukuliwe hatua kwa ubadhirifu wa fedha za umma,” amesema Sumaye.

Katika hatua nyingine, Sumaye amesema kama mchakato huo ulikuwa halali na kupata baraka za CCM ,baraza hilo linaitaka CCM kuilazimisha serikali iliyopo madarakani kuuendeleza mchakato huo au kuwawajibisha wanaoukwamisha kwa kuwa fedha za umma zilizotumika katika mchakato huo zimepotea bila kuleta matokeo yaliyotarajiwa.

“Kama mchakato ulikuwa halali na wenye baraka za chama hicho tawala, basi watawala wa sasa ama chama chao kiwalazimishe kuendelea na mchakato wa katiba mpya au kiwashtaki na kuwawajibisha kwa ubadhirifu wa fedha za umma zilizopotea bila matokeo tarajiwa,” amesema Sumaye.

Sumaye ameeleza kuwa, kama mchakato huo ungefanikiwa, katiba mpya ingepatikana na kutoa mchakato mzuri kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.

Share:

SUMAYE : MUSWADA WA SIASA UKIACHIWA UTATAFUNA MPAKA CCM


Baraza Kuu la Chadema Kanda ya Pwani limetaka serikali kuuondoa muswada wa vyama vya siasa uliowasilishwa bungeni, kwa sababu unakiuka katiba kwa kuwa baadhi ya vifungu vyake vinaua demokrasia ya vyama vingi nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye amesema endapo wabunge hususan wa CCM wakiupitisha muswada huo, itakuwa ndio mwisho wa demokrasia, na kuwataka wabunge kuupinga kwa kuwa moto wake hautaunguza wapinzani pekee, bali hata wao utawaunguza.

Sumaye ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu, amewatahadharisha wabunge wa CCM kwamba endapo muswada huo wataupitisha demokrasia itakufa hadi ndani ya chama chao kwa kuwa mtu mmoja ndiye atakuwa na mamlaka ya kuamua wagombea wa ubunge na hata urais.

“Nawatahadharisha wabunge kama muswada huo utapita demokrasia itakufa hata ndani ya CCM mtu mmoja atakuwa na mamlaka ya kuamua nani awe mbunge au Rais,” amesema Sumaye.

Katika hatua nyingine, Sumaye amesema pamoja na mazingira magumu ya demokrasia, wataendelea kufanya siasa.

“Tunachotaka CCM itoke madarakani kupitia sanduku la kura ili tuwe na nchi ya upendo kama yalivyo mataifa mengine, hatuna haja ya kwenda ulaya ,” amesema na kuongeza.

“Na naamini Watanzania ni waelewa, kila mmoja ananung’unika kivyake sasa hawa wote naamini hawezi kuona mambo haya yanaendelea wananyamaza tu, itafikia hatua watasema hapana, naamini serikali ni sikivu haya tunayoandika wanasikia na watachukua hatua ili tusije fika huko tunakotaka kutoka.”

Sumaye ameeleza kuwa“Katika mfumo wa demokrasia wa vyama vingi, hakuna serikali isiyosemwa na wananchi wake sababu ndio walioiweka madarakani. Lengo kuu la demokrasia ya vyama vingi ni kutoa uhuru kwa wananchi kutoa maoni yao hata kama wanapinga maoni ya kiongozi.

Maoni ya tofauti ni kioo chako katika utawala ili uonyeshwe yale ambayo wa upande wako hawatakuambia au kukuonyesha, mfumo ambao haukubali kukosolewa kwa kiongozi wake au serikali yake ni mfumo wa utawala wa kiimla au wa kidikteta,” amesema na kuongeza Sumaye.

Chanzo - Mwanahalisi online
Share:

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MFANYABIASHARA ALIYETUHUMIWA KUMPA RUSHWA LUKUVI

Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemwachia huru mfanyabiashara, Mohamed Kiluwa (50) baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Kiluwa alikuwa anakabiliwa na shtaka moja la kutoa rushwa ya dola za kimarekani 40,000 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Desemba 24, 2018 na Hakimu Mkazi, Samuel Obasi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutolewa hukumu.

"Ushahidi wa upande wa mashtaka umekaa kihisia zaidi, hivyo mahakama yangu imeshindwa kumtia hatiani mshtakiwa, hivyo mahakama hii imemuachia huru Kiluwa" amedai Hakimu Obasi na kuongeza: "Hisia hata kama zina nguvu kiasi gani, haziwezi kufanya mahakama imtie hatiani," amesema Hakimu Obasi.

Na Hadija Jumanne, Mwananchi
Share:

MBUNGE WA CHADEMA APATA AJALI YA GARI..KUNA TAARIFA YA VIFO


Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kunti Yusuf Majala, amejeruhiwa vibaya baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali. Anaripoti Yusuph Katimba.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu, tarehe 24 Desemba, maeneo ya Kilema, katikati ya wilaya za Chemba na Kondoa.

Taarifa zilizothibitishwa na ofisa mmoja wa Bunge mjini Dodoma, ambaye hata hivyo, hakupenda kutajwa jina lake, zinaeleza kuwa katika ajali hiyo, watu wengine wanne wamefariki dunia.

Afisa huyo ambaye anasema siyo msemaji wa Bunge, anaeleza kuwa gari ambalo mbunge alikuwa akilitumia lilianguka baada ya kuchomoka tairi la mbele mkono wa kushoto wa dereva.

Anasema, “gari hili lilikuwa na watu 11 (kumi na moja), watoto saba na wakubwa wanne. Mhe. Kunti ana maumivu makali sana ya kiuno na shingo.”

Anasema, kufuatia hali ya mbunge huyo kuwa mbaya, ofisi ya Spika, imeanza kufanya utaratibu wa haraka wa kuhakikisha mara atakapofikishwa kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, aweze kusafirishwa yeye na majeruhi wengine, kupelekwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.”

Hata hivyo, afisa huyo hakuweza kuwafahamu mara moja majina ya wale waliofariki dunia; na au kujeruhiwa. Bali, taarifa kutoka maofisa wa Chadema zinasema, baadhi yao waliofariki, sehemu kubwa watakuwa familia ya mbunge huyo.

Kwa mashuhuda, gari lililokuwa limembeba Kunti na ambalo limepata ajali, lilikuwa na namba za usajili, T 624 DPE. Lilikuwa likitokea Dodoma mjini kuelekea Kondoa.

Dereva wa gari hilo alikuwa ni Stephano Masawe, ambaye ni dereva wa Katibu wa Chadema, Kanda ya Kati.

Chanzo - Mwanahalisi online
Share:

WAKURUGENZI WAZUIWA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA CHRISMAS


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakurugenzi kutosheherekea sikukuu ya Christmas mpaka watakapopata ufumbuzi wa ujenzi wa madarasa 99 yanayohitajika kwaajili ya kutumiwa na wanafunzi 4930 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019.

Ametoa maagizo hayo wakati akitoa salamu zake za Christmas kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa ambapo amesema kuwa ufaulu mwaka huu 2018 umekuwa kwa asilimia 73 ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo ulikuwa ni wa asilimia 68 na hivyo wanafunzi 4930 kukosa kuingia madarasani kutokana na changamoto ya upungufu wa madarasa.

Ameongeza kuwa serikali ya Mkoa imejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi ya kusoma hali ambayo itawafanya wanafunzi wote waliokosa nafasi kupatiwa fursa ya kuendelea na masomo yao kwa mwaka 2019.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewaomba wanachi kwa kushirikiana na halmashauri kuhakikisha vyumba hivyo vinapatikana hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa pili.

“Hawa wanafunzi tusiwakatishe tamaa ya kukosa nafasi ya kwenda kidato cha kwanza, hakuna mwanafunzi hata mmoja ataacha kwenda kidato cha kwanza, wakuu wa wilaya wote wasimamie zoezi hili na hakuna likizo na wale wakurugenzi wote hakuna kwenda likizo mpaka vyumba vya madarasa vyote view vimekamilika,” amesema.

Kati ya hayo madarasa 99, halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatakiwa kujenga madarasa 41 yatakayotumiwa na wanafunzi 2,042, huku Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikihitaji madarasa 27 ili kutumiwa na wanafunzi 1,365.

Halmashauri zingine ni Wilaya ya Nkasi inayohitajika kujenga madarasa 19 kwaajili ya wanafunzi 925 na halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikitakiwa kujenga madarasa 12 kwaajili ya wananfunzi 598.
Share:

WANANCHI WACHOMA MOTO NYUMBA NA MAGARI GEITA


Nyumba na gari vikiwa vimeungua

Watu zaidi ya 20, wakazi wa kijiji cha Nzera Kata ya Nzera, Wilayani Geita hawana sehemu ya kuishi kufuatia nyumba zao kubomolewa na zingine kuchomwa moto na kikundi cha watu ambao pia ni wakazi wa eneo hilo.

Tukio hilo limehusisha kubomolewa kwa nyumba zaidi ya nne na zingine kuchomwa moto kwa kile kinachoelezwa kuwa ni chuki binafsi zinazohusisha masuala ya kisiasa.

Mbali na nyumba hizo kubomolewa na zingine kuchomwa moto, pia magari mawili aina ya Hiace T 226 GBV na Noah, mali ya Mratibu Elimu Kata ya Katoma, Kulwa Sherembi yamechomwa moto.

Jeshi la Polisi limewakamata watu 25 wanaohusishwa na tukio hilo huku likilaani vikali kitendo hicho ilichokiita ni cha kishenzi na kuahidi kuwasaka watu wote waliohusika na kuwatia mbaroni.

Akifafanua kuhusiana na tukio hilo, lililotokea majira ya alfajiri, Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwalubambo amesema chanzo cha tukio hilo ni uvamizi uliotokea, ambapo vibaka walivamia nyumba mbili za wakazi wa eneo hilo, Faustine Kaswahili na Edward Samson kisha kujeruhi na kupora fedha na kutokomea kusikojulikana.

Baada ya tukio hilo ndipo kikundi kingine kilipojihamasisha na kwenda kubomoa na kuchoma nyumba hizo pamoja na magari kikiwahusisha wamiliki wa familia hizo kufadhili waharifu wa uvamizi uliotokea kijijini hapo ili hali wakijua si kweli.
Share:

Wimbo Mpya : MH TEMBA - KULIKONI

Wimbo Mpya wa Mh Temba – Kulikoni


Share:

MSAJILI AWATAKA WANASIASA KUACHA UTOTO...MALALAMIKO YAO YANA SABABU ZA PORINI

Baada ya muungano wa vyama 10 vya upinzani kutoa tamko lao la pamoja kupinga maamuzi ya ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kusitisha vikao vya baraza la vyama vya siasa bila kujulisha, ofisi hiyo imeibuka na kujibu tuhuma hizo.

Ofisi hiyo ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imewataka viongozi hao kuacha utoto wa kukwepa wajibu wao wa kuwasiliana na ofisi hiyo, pale wanapoona kuna jambo linawatatiza badala ya kukimbilia katika vyombo vya habari.


Akijibu tuhuma hizo kwa niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema, viongozi hao wa upinzani wanakwepa wajibu wao wa msingi kwa kufanya siasa nyepesi isiyoakisi maana mzima ya kukuza demokrasia nchini.


“Sasa hao wanaosema hawakuwashirikishwa wanataka ushirikishwaji wa namna gani,” amehoji Nyahoza.

Amesema kanuni ya baraza hilo linaruhusu kuahirishwa kwa kikao pale panapokuwa na sababu na uamuzi huo hufanyika baada ya majadiliano na Mwenyekiti wa baraza la vyama.

Nyahoza amesema Katibu wa baraza ambaye ni Msajili, aliwasiliana na Mwenyekiti wa baraza kisha wajumbe wakataarifiwa kwa simu na kwengine kwa njia ya mdomo kwa kuwa kanuni zinaeleza jambo hilo.


"Tumesikia malalamiko yao mengi hayana msingi, ni sababu za porini kwa kuwa ofisi yetu ipo wazi walipaswa kuja kupata ufafanuzi kabla ya kwenda kwenye vyombo vya habari na hii kwa kweli imetusikitisha,” ameongeza.


Pia amesema ofisi yake ilishatoa sababu ya kuahirishwa kwa kikao hicho kuwa ni kupisha uchaguzi mdogo wa marudio na kusisitiza kwamba baada ya uchaguzi huo baraza litakutana tena kujadili mambo yao.
Share:

JOKATE ATOA USHAURI UPIGAJI KURA TUZO ZA FILAMU ZA SINEMA ZETU INTERNATIONAL FILM FESTIVAL(SZIFF)

Mlezi wa Tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival(SZIFF), Jokate Mwegelo amewashauri watu kutowapigia kura washiriki kwa kuangalia umaarufu walio nao au mahaba walio nao kwao.

Akizungumza leo Desemba 24 katika mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kuelezea hatua ambayo mchakato wa tuzo hizo umefika, Jakate ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, amesema watu hawapaswi kuangalia umaarufu kama kweli wanataka kukuza Sanaa hiyo na badala yake waangalie uwezo na kipaji cha mtu.

Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia pia kuja na vipaji vipya badala tasnia hiyo kutawaliwa na watu walewale kila siku na kupongeza hatua ya waandaaji ya kwenda hadi mikoani kusaka washiriki.

“Pamoja na kwamba waandaji wameamua kutoa nafasi kwa watengeza filamu kutoa majina ya wale wanaowaona ni bora katika kipengele cha muigizaji bora wa kike na wa kiume, lakini hii katika upigaji kura haiwazuii kuchagua mnayemuona anafaa, na nina imani hata hao waandaaji hawatatuletea mtu ambaye wanajua hastahili." Amesema
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger