Monday, 24 December 2018

CHADEMA WASHTUKIA DHARURA TUME YA UCHAGUZI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Pwani kimetaka kufanyika kwa maboresho ya daftari la wapiga kura mapema ili kuepuka zima moto.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 24, 2018, Mwenyekiti wa kanda hiyo, Frederick Sumaye amesema kazi hiyo ifanyike kwa muda muafaka na mapema ili baadaye isije kufanyika kwa dharura.

"Ili kulinda haki za raia tunapenda kuikumbusha serikali kuwa ni lazima zoezi la kuhakiki daftari la wapiga kura ifanyike kwa muda muafaka bila kuifanya kama zoezi la dharura ili kila mpiga kura apate haki yake ya kuandikishwa"amesema Sumaye.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa tume huru ya Uchaguzi, Sumaye amesema; "Kwa ajili ya mapungufu kwenye muundo mzima wa Tume ya uchaguzi,kama jambo la umuhimu wa kipekee Tume HURU ya uchaguzi ambayo haitapewa maelekezo na utawala na itakuwa na watumishi wake bila kutegemea watumishi wa serikali,iundwe haraka kwa vyovyote kabla ya uchaguzi ujao"
Share:

CCM WATANGAZA HAKUNA LIKIZO MWISHO WA MWAKA

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema kuwa katika kipindi mwisho wa mwaka atakuwa katika utekelezaji wa majukumu ya chama bila kupumzika.
 
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twittwer Polepole ameandika kuwa atakuwa katika mkoa wa Ruvuma akiitekeleza Ilani ya Chama chake chini ya Rais, Dkt. John Magufuli.

"Mwisho wa Mwaka huu niko Mpitimbi, Likuyufusi, Lutapwasi, Mhukuru, Madaba, Bomba Mbili, Mkenda na Lipaya nitakuwa nakagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM. Heko John Pombe Joseph Magufuli na Wana CCM kwa kazi nzuri, hongereni", ameandika Polepole.

Akiwa jimboni humo Polepole kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza Mbunge wa Jimbo la Peramiho, lililopo Wilaya ya Songea Vijijini Mkoani wa Ruvuma, Jenista Mhagama kwa kuekeleza kwa asilimia kubwa Ilani ya chama hicho
Share:

CCM YAWAGEUKIA WABUNGE WASIOKWENDA MAJIMBONI... 2020 LAZIMA WAKATWE


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema wabunge ambao hawafiki kwenye majimbo yao baada ya kuchaguliwa na wananchi kwa kipindi cha miaka mitano, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakata majina yao mwaka 2020.
Alisema wabunge wengi wamekuwa na tabia kutoonekana majimboni na kuacha majimbo yao bila uwakilishi, hivyo kuifanya CCM kuwa na wakati mgumu uchaguzi unapofanyika.

Balozi Seif aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wanachama wa CCM wilayani Kahama wakati akijitambulisha baada ya kuteuliwa na na chama hicho kuwa mlezi wa Mkoa wa Shinyanga kichama, na kusema wabunge wengi wakichaguliwa wanahamishia makazi mjini Dodoma.

Alisema wakifika Dodoma husahau wananchi wao ambao waliwapatia dhamana ya kuwaongoza na kukifanya chama kuwa na wakati mgumu wa kuwanadi watu hao kwa wananchi uchaguzi mwingine unapofika.

“Mbunge ukiona jina lako halijarudi mwaka 2020 ujue umekatwa na Kamati Kuu ya CCM…kutokana na hali hiyo wabunge mnatakiwa kubadilika na kuyatembelea majimbo yenu mara kwa mara na kufanya mikutano na kuzungumza na wananchi wenu, ili kujua changamoto zilizopo na kuzitatua,” alisema Balozi Seif.

Alisema wananchi wamekuwa wakilalamikia kutowaona wabunge wao na kukosa baadhi ya huduma za kijamii na kuongeza kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha wananchi kutokuwa na imani na chama tawala na kuvipatia dhamana vyama vingine kuwaongoza.

Akimuunga mkono kuhusu hoja hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, alisema hata baadhi ya madiwani wanapopata ushindi kwenye kata zao huhamia mijini na kujenga miji mipya.

Alisema chama hakitawavumilia madiwani wa namna hiyo na kitawakata majina na kuweka watu wengine ambao watakuwa na uwezo wa kuwahudumiwa wananchi na kukaa karibu nao muda wote wa miaka mitano.

Share:

Askari polisi Njombe apandishwa cheo kwa kuhudumia ajari ya Mkuu wa majeshi.

Na Amiri kilagalila Askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Njombe mwenye namba H1914 pc Petro Philemon amepandishwa cheo cha KOPLO kutokana na kutoa huduma vizuri katika ajali aliyoipata Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Venance Mabeyo na msafara wake wilayani Ludewa mkoani Njombe novemba 25 mwaka  huu. Akizungumza  na waandishi wa habari mara baada ya kumpandisha cheo cha Coplo kutoka Constable askari huyo, kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Renatha mzinga amesema kuwa askari huyo alionyesha wajibu wake vizuri katika kuhudumia katika ajari hiyo na…

Source

Share:

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU DEC 24 2018, JUVENTUS WAMWINDA LUKAKU

Juventus imeonyesha kutaka kumsajili mshambulaji wa Manchester United Mbelgiji Romelu Lukaku ,25, (Calciomercato-in Rome)

Timu ya Juventus ya Italia inataka kumsajili kiungo wa Arsenal na timu ya Taifa ya Wales Aaron Ramsey, 27, akiwa mchezaji huru (sky Italia)

Lakini pia nayo timu ya Buyern Munich ya Ujeruman bado inavutiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Cardiff(Mail)Aaron Ramsey

Arsenal inaweza kuvunja rekodi yake ya usajili kwa kutaka kumsajili mchezaji wa Lille ya Ufaransa Nicolas Pepe na timu yake hiyo itaka dau la pauni Milioni 72 ili kumuuza winger huyo wa Ivory Coast. (Telefoot,via Metro)

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Tony Cascarino ameitaka timu yake hiyo ya zamani kumsajili mshambuliaji wa West Ham United Marko Arnautovic (Talksport)

Timu ya Lazio ya Italia inamtaka mshambuliaji wa timu ya Southampton Manolo Gabbiadini ,27, (La Nazione - In Italia)

Fulham inataka kumsajili mlinzi wa kati wa timu ya Besiktas ya Uturuki Domagol Vida raia wa Croatia (Fotomac - Uturuki)

Kocha wa Newcastle Rafael Benitez anatamani kusajili winga mwezi ujao ukufunguliwa usajili wa dirisha dogo (Chronicle)

Winger wa Bayern Munich Mfaransa Frank Ribery amewwka milango wazi wa timu yake hiyo kumuongezea mkataba kwa msimu ujao (Sky,via Goal)

Mashabiki wa timu ya Birmigham City wamesikirishwa na kitendo cha timu yao kukosa tiketi za ziada kwaajili ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya West Ham utakaochezwa January 5 (Birmingham Mail).
Share:

MIZENGO PINDA AELEZA ALIVYOUMIZWA NA WAPINZANI...NAYE KUUTAKA URAIS

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameweka wazi jinsi alivyokuwa akiumizwa na kauli za upinzani dhidi ya uongozi wake.

Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma jana, Pinda alisema kuna kipindi wakati wa uongozi wake, wapinzani walikuwa wakiinyooshea kidole Serikali yao kuwa ni dhaifu haina makali, hivyo walikuwa wanataka kiongozi mkali na mwenye uamuzi mgumu.

Alisema alikuwa haipendi kauli hiyo na ilikuwa ikimkera kwa sababu ilimlenga na yeye, lakini akasema sasa anashangaa kuona wapinzani haohao wameanza kulalamika tena juu ya utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye ndiye kiongozi wa aina waliyekuwa wakitamani kumpata.

Pinda aliteuliwa kuwa waziri mkuu na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete baada ya Edward Lowassa kujiuzulu.

Mwaka 2015, alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kugombea urais lakini jina lake liliondolewa katika hatua za awali.

Jana, mstaafu huyo alitumia jukwaa la UVCCM kutoa yaliyo moyoni mwake ikiwa ni miaka mitatu ya tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka 2015.

Alisema Rais Magufuli ndiye kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kutokana na uthubutu alionao katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Wakati ule kauli hii ilikuwa inaniudhi kwa sababu ilikuwa inanilenga mimi lakini sasa hivi tena ambapo Mungu amesikia kilio chao na kuwapa JPM wameanza kulalamika tena, ni jambo la kushangaza,” alisema Pinda.

“Wakati fulani kuna baadhi ya watu huwa wananiuliza, hivi mzee na wewe si ulikuwa unautaka urais, nawajibu tu aka huyuhuyu ndiye anayefaa, mimi ni miongoni mwa watu wanaomkubali sana Magufuli.”

Alisema Rais Magufuli ametekeleza miradi iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambayo serikali nyingine zilishindwa kuitekeleza kwa kisingizio cha kuogopa gharama kubwa.


Na Rachel Chibwete, Mwananchi
Share:

Video Mpya : GENIUS Ft. DOGO JANJA - ROHO YANGU

 Genius Ft. Dogo Janja - YANGU ROHO
Advertisement
Share:

Wimbo Mpya : YOUNG KILLER - APPLE DSM

Msanii wa muziki Bongo, Young Killer anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya unaokwenda Apple DSM. Isikilize hapa.

Advertisement
Share:

DNA SASA KUTUMIKA KUWABAINI WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI

Wilaya ya Nyang’hwale imesema itaanza kupima vinasaba kati ya mtoto na mwanamume aliyemuoa mwanafunzi ili kubaini kama ndiye baba halisi.


Hatua hiyo imekuja kutokana na wanafunzi wanaoacha shule kwa kupata ujauzito kukataa kuwataja wanaowapa mimba kwa madai hawawafahamu, lakini baada ya kujifungua huolewa na kudai aliyeoa si baba wa mtoto.


Akizungumza hivi karibuni kuhusu hatua zilizochukuliwa kutokana na wilaya hiyo kurekodi mimba zaidi ya 160 za wanafunzi kwa kipindi cha miaka mitatu, Mkuu wa Wilaya hiyo, Hamimu Gwiyama alisema Serikali imeamua kuwasaka hata ambao wameolewa ili kubaini kama wanaume hao ndiyo waliokatisha ndoto zao za masomo.


“Wanafunzi wengi waliopata mimba sasa wameolewa, lakini wanapohojiwa kujua aliyewapa mimba, wanadai hawamjui au hawamkumbuki, sasa polisi watafanya uchunguzi na kuwahoji wote wawili kujua ukweli itakapokuwa ngumu tutawapima vinasaba.”


Alisema Waraka wa Elimu namba tano wa mwaka 2011 unaoruhusu mwanafunzi kufukuzwa shule baada ya kuwa mtoro kwa siku 90, umechangia wazazi wengi kuwakatisha masomo wanafunzi na kuwaoza.


“Tumeanza operesheni ya kuwasaka wote walioacha shule haijalishi ni baada ya miaka mingapi, bali wote walioacha shule tutawachukulia hatua. Lengo la operesheni hii ni kumaliza tatizo la mimba, tuwajengee hofu wanaume wanaowaoa wanafunzi,” alisema Gwiyama.


Alisema moja ya sababu zinazochangia wanafunzi kubeba mimba ni mila ya Kisukuma ambayo huwapa chumba maalumu cha nje watoto wa kike baada ya kuvunja ungo, hali ambayo huwafanya wengi wao kuwaingiza wanaume na kulala nao.


Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel akizungumzia tatizo la mimba kwa wanafunzi, alisema wazazi na jamii wanayo nafasi kubwa ya kusaidia kulimaliza tatizo hilo kwa kujenga maadili kwa watoto. Takwimu zinaonyesha kuwa wanafunzi 170 wa sekondari katika Mkoa wa Geita kwa mwaka 2017 waliacha shule kwa kupata ujauzito huku 90 wa shule za msingi wakishindwa kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito.


Pia, mkoa huo una tatizo kubwa la utoro kwa wanafunzi, takwimu zinaonyesha kati ya wanafunzi 13,139 walioanza kidato cha kwanza mwaka 2014, ni wanafunzi 7,912 tu ambao ni sawa na asilimia 60 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017.
Share:

KIONGOZI WA TFF AFARIKI DUNIA

Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza kifo cha aliyekuwa mtunza vifaa msaidizi wa timu ya taifa 'Taifa Stars', Kessy Rajab kilichotokea jana Desemba 23.








Taarifa ya TFF iliyotolewa na Rais wake, Wallace Karia imesema, "Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania TFF Wallace Karia amepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa kifo cha aliyekuwa mtunza vifaa msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Kessy Rajab".

"Kwa niaba ya TFF, Rais Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Kessy, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wenzake, " imeongeza taarifa hiyo.

Msiba upo nyumbani kwake, Kurasini karibu na Uhamiaji wakati taratibu nyingine za mazishi zikiendelea.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, zinaeleza kuwa chanzo cha kifo hicho ni mshtuko alioupata katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, kati ya Simba na Nkana Red Devils uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Rajab Kessy alikuwa ni shabiki mkubwa wa Simba na alihudhuria katika mchezo huo wa jana ambao alipata mshtuko mara baada ya Simba kufungwa bao la kwanza. Alikimbizwa hospitali ya Temeke ambako ndiko alipoteza maisha.

Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Chanzo: Eatv
Share:

WHITE STAR YAIBUKA KIDEDEA MICHUANO YA MWISHO WA MWAKA NGARA.

NGARA. Kahinde Kamugisha Michuano ya kumaliza mwaka 2018 ya mpira wa miguu katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge wilaya ya Ngara mkoani Kagera,jana imefikia tamati kwa kuchezwa fainali kati ya Mursagamba Fc na Rulenge white star Katika mchezo wa michuano hiyo Rulenge white star wameibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuwa bingwa wa michezo kwa mwaka 2018 huku ikichukua zawadi ya kombe, seti ya jezi na mipira miwili. Mshindi wa pili Mursagamba Fc amepata zawadi ya seti ya jezi na mpira moja huku mshindi wa tatu Kibogora Fc…

Source

Share:

JINSI WANAWAKE WENYE SHEPU WANAVYOHANGAISHA WANAUME MITAANI


Habari dada, kwa jina naitwa Warda nina miaka 26. Nina mume wangu wa ndoa tangu mwaka jana 2017. Tulishaishi mwaka mmoja bila ndoa ambayo ni mwaka 2016. 

Naomba ushauri wako, mume wangu anapenda sana wanawake wanene wenye mishepu. Mimi siyo mnene wala mwembamba ni wa kawaida tu na mume wangu nampenda sana na yeye pia ananipenda.

Lakini tatizo kubwa ni kuchepuka kila nikikaa naye namuuliza kinachomfanya achepuke ni nini ananijibu ni mahaba. Lakini mimi kila kitu namfanyia anachotaka lakini bado anachepuka. 

Ana umri wa miaka 27. Je, umri wake labda ndio unamfanya hivyo au ni nini. Maana nimechoka kumvumilia, je, nifanyeje?

Mpenzi msomaji, bila shaka umemsikia dada huyu anavyolalamika juu ya nyendo za mumewe. Kwamba mumewe anavutwa zaidi na mishepu ya wanawake kila wapitapo au awaonapo popote. 

Hili ni tatizo kubwa. Bibie amefikia hatua akaona bora apaze sauti kwa sababu anahisi kabisa kwamba mume wake havutiki tena naye bali mawazo au mapenzi kayahamishia huko mitaani anakowakodolea macho wanawake wenye mishepu.

Bibie kajieleza vema hapo juu, kwamba yeye siyo mnene ni umbo la kawaida tu. Hata hivyo, mwanaume huyo alimpenda jinsi alivyo, lakini sasa anashangaa mumewe kaipata wapi tabia ya kupenda wanawake wanene wenye mishepu na makalio mvuto.

Mpenzi msomaji, mimi nimetafakari kilio cha bibie nikaona picha iliyosheheni matukio kibao. Labda hapa nitaje machache, mengine msomaji wangu utamalizia.

Katika maisha ya ndoa, zipo changamoto mbalimbali. Pia zipo siri nyingi zilizojificha ambazo hujitokeza baadaye baada ya watu kuoana. Ni katika maeneo machache sana wawili huweka wazi tabia zao kabla ya kuoana. Mengine hufichwa yakajitokeza baadaye.

Inawezekana kabisa, tabia hii ya kupenda wanawake wenye mishepu kijana huyu alikuwa nayo lakini akalazimika kumuoa huyo anayelalamika kutokana na sababu mbalimbali. Labda alimpa mimba kabla, au ilikuwa ni shinikisha la wazazi na kadhalika.

Au, inawezekana kabisa kijana huyu hakuwa na hiyo tabia hapo awali, ila baada ya kuoa na kuchanganyika na vijana wenzake, akajikuta anaiga tabia ambazo wala hakuwahi kufikiria kuwa nazo. Akaona wenzake wanafurahia wanawake wenye mishepu na yeye akavutwa kupenda. 

Kingine inawezekana baadhi ya marafiki zake wameoa wanawake wenye mishepu na hivyo kumjaza sifa walizonazo wanawake wa aina hiyo, matokeo yake anamuona hata yule wa nyumbani aliyemchagua mwenyewe, kumbe hafai. Hiyo ni laana ya kuiga vya wengine ambavyo kwako ni madhara.

Angalia sasa kijana ambaye alikuwa anaishi vizuri na mkewe kaanza kubadilika na hata wanapokuwa matembezini pamoja bwana akiona mwanamke mwenye shepu hata kama yuko na mumewe, atageuza shingo kumtizama.

Jambo hilo limemkwaza sana bibie hata kuamua kulitoa moyoni aweze kupewa ushauri. Amefikia hatua kumuuliza mumewe kwamba kwanini anatamani vya nje wakati yeye yupo. Na akamuuliza ni nini anachokikosa kwake hata kuamua kukodolea macho vya nje?

Mpenzi msomaji, nimedokeza awali hapo juu kwamba ziko siri zilizojificha. Inawezekana kabisa mume huyu baada ya kuoa amekuja kugundua kuwa yapo mapungufu fulani kwa mkewe.

Lakini hata kama yapo mapungufu, wangeweza kabisa kuyarekebisha, maisha yakasonga mbele. 

Kingine kinachoweza kuwa moja ya sababu ya jamaa kuvutiwa na shepu ya nje, inawezekana anatoka nje ya ndoa. Na pengine kwa utashi wake mwenyewe au kwa kushawishiwa na marafiki zake, amepata mchepuko mwenye mishepu kiasi cha kumchanganya.

Ndio maana baada ya kuulizwa na mkewe kwanini anahangaika na wanawake wa nje akamjibu kuwa ni mahaba. Hapa tayari ndoa iliyokuwa na matumaini imeshaingia dosari.

Wanatiana moyo kwamba wanapendana lakini katika uhalisia ule upendo wa mwanzo umeshagawanyika na kinachotawala sasa ni mashaka na hofu hasa kwa bibie ambaye anashangaa nini kimemsibu mumewe.

Mwanaume yeye ameshaweka wazi tabia yake kwamba anapenda michepuko. Na mwanamke anadai anajitahidi kumzuia mume wake asivutwe na tamaa za nje lakini anashindwa ndio maana ameamua kuvunja ukimya.

Kiukweli, na hii nimeisema mara nyingi kwamba, shetani yuko kazini akiharibu na kubomoa ndoa za watu. Jamaa kavamiwa na pepo linalotamani wanawake wa nje ingawa wa kwake mzuri yuko ndani. 

Ili ujue shetani kamnasa mwanaume huyo, ngoja mkewe aamue kufungasha virago ndipo atakapozinduka na kujiona mjinga kwa kutamani mishepu ya mitaani isiyo na faida, iliyojaa hasara. Maisha Ndivyo Yalivyo.

Tabia za aina hii ni hatari kwani mwanamke naye aweza kuchepuka. Na huo ukawa mwanzo wa kukaribisha maradhi mabaya yanayoua na kuchipua watoto yatima. 

Je, una ushauri wowote kwa familia hii? Au unalo suala la kifamilia/ndoa/mahusiano linalokutatiza? Wasiliana nami kwa ujumbe mfupi kupitia simu ya ofisi namba 0715268581 (usipige), au barua pepe; fwingia@gmail.com au flora.wingia@guardian.co.tz

Share:

SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA KUANZISHA SAFARI ZA MOJA KWA MOJA ZAMBIA,ZIMBABWE NA CHINA Via THAILAND


Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) liko mbioni kuanzisha safari za moja kwa moja katika nchi ya Zambia, Zimbabwe pamoja na China kupitia Thailand huku ikiongeza vituo vitano vya ndani ya nchi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho leo Jumapili Desemba 23,2018 katika mapokezi ya ndege mpya ya Airbus A220-300 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Dk Chamuriho amesema huo ni utekelezaji wa awamu ya pili ya upanuzi wa mtandao wa ATCL ikiwa ni baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza.

Amesema vituo vya ndani vitakavyoongezwa ni Mpanda, Pemba, Iringa, Kahama, Musoma na kurudisha safari za Songea na Mtwara.

“Utekelezaji wa safari hizo za ndani utatokana na kukamilika kwa utekelezaji wa ujenzi wa viwanja hivyo juu ya ujenzi wa miundombinu unaofanyika pamoja na uwepo wa abiria wa kutosha ikiwamo mbinu za kibiashara,” amesema Dk Chamuriho

Amesema utekelezaji wa awamu ya tatu ukifuatiwa na mpango mkakati wa miaka mitano utaanza 2021-2022 ambao utahusisha safari za Ghana, Nigeria, Dubai, Uingereza na Muscat.

“Wakati tunaanza tulikuwa na marubani 16 na hadi sasa tunao 50, wengi wao ni wale tuliowatayarisha wenyewe kupitia mpango mafunzo ya awali nchini na kuwapeleka nje ya nchi kupitia makubaliano tuliyoweka na Shirika la Ndege la Ethiopia na Kampuni ya Bombadier,” amesema Dk Chamuriho

Kwa upande wa mafundi na wahandisi wa ndege wameongezeka kutoka 31 waliokuwepo Oktoba 2016 hadi 87 ambapo wahandisi wazawa ni 36, wageni sita na mafundi 45 huku nafasi zikiendelea kutolewa kupitia mpango maalumu kwa vijana wa Kitanzania.

Dk Chamuriho amesema uwezo wa ndege za ATCL katika kubeba abiria umeongezeka hadi kufikia 34,000 kwa mwezi kutoka abiria 5,600 huku umiliki wa soko la ndani ukiongezeka kutoka asilimia 2 Desemba 2016 hadi asilimia 31, Oktoba mwaka huu.

Amesema shirika limepiga hatua kwa kuruka kwa ndege na kutua kwa wakati kutoka asilimia 22, Oktoba 2016 hadi asilimia 80 mwaka huu.

“Tunalipa kodi serikalini, tunawekeza katika ukodishaji pesa, hizi zote ni faida ambazo zinapatikana katika uendeshaji wa shirika hili. Tunaendelea kutumia bidhaa zinazozalishwa na kuchakatwa ndani ya nchi,” amesema Dk Chamuriho.

Amesema ndege mbili za aina hii inayopokelewa leo zilitakiwa kupokelewa Mei na Juni mwaka huu lakini kutokana na changamoto za mafundi ndiyo maana moja inapokelewa leo na nyingine Januari mwakani.

"Mpaka hivi sasa tumekuwa na vituo 11 vya huduma ambapo kimoja kipo nje ya nchi na tumeboresha mifumo ya ukataji tiketi, huduma kwa wateja na kuimarisha mifumo ya uondokaji wa ndege," amesema Dk Chamuriho.
Share:

NAPE NNAUYE ATOKA MAFICHONI... 'SIMBA HII NI KIBOKO...THIS IS SIMBA

Share:

Sunday, 23 December 2018

Picha; SHIRIKA LA RAFIKI SDO LASHEHEREKEA SIKU YA FAMILIA 'RAFIKI FAMILY DAY' NA MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA

Share:

Angalia Picha 26 : RAIS MAGUFULI AKIPOKEA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220 - 300 UWANJA WA NDEGE DAR

Share:

SUMAYE KUJILIPUA KESHO,ANATARAJIA KUWEKA MAMBO HADHARANI

NA KAROLI VINSENT WAZIRI Mkuu Mstaafu,Fredrick Sumaye kesho Jumatatu  ya tarehe 24 Desemba 2018 anatarajia kuzungumzia mambo mazito kuhusu hali ya nchi ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na wengi. Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari inasema Waziri Mkuu huyo aliyedumu kwenye nafasi yake kwa kipindi kirefu cha miaka 10 ,inasema atazungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kanda ya Pwani ya Chadema zilizoko Magomeni Jijini Dar es Salaam. Taarifa hiyo ambayo haijasema nini ambacho atazungumzia Mwenyekiti huyo wa Kanda hiyo ya Pwani,ila kwa mujibu wa Mtoa Taarifa kutoka…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger