INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Klose ameifungia Ujerumani bao la pili wakati ikitoa kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Brazil katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Klose alifunga mabao matano katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002 na 2006, akatupia manne huko Afrika Kusini mwaka 2010 na mpaka sasa huko Brazil tayari amefunga mabao mawili moja dhidi ya timu yake na Ghana wakati la pili dhidi ya Brazil leo.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amempiku mshambuliaji wa Brazil, Ronaldo Luís Nazário de Lima aliyekuwa na mabao 15.
Wachezaji wengine waliowahi kufunga mabao zaidi ya 11 kwenye michuano hiyo ni: Gerd Muller wa Ujerumani 14, Just Fontaine wa Ufaransa 13, Pele wa Brazil 12, Jurgen Klinsmann wa Ujerumani 11 na Sandor Kocsis wa Hungary 11.
Miroslav Josef Klose akishangilia baada ya kutupia bao la pili kwa Ujerumani usiku huu na kuvunja rekodi ya kupachika mabao.
MSHAMBULIAJI wa Ujerumani na timu ya Lazio ya Italia, Miroslav Josef
Klose, ameweka historia usiku huu baada ya kutupia bao lake la 16 na
kuwa mfungaji wa mabao mengi katika michuano ya Kombe la Dunia iliyoanza
mwaka 1930 ambayo kwa sasa inaendelea nchini Brazil.Klose ameifungia Ujerumani bao la pili wakati ikitoa kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Brazil katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.