Monday, 30 June 2014

MSAJILI WA VYAMA VINGI AKATAA MABADILIKO YA CHADEMA



mutunga_f8c6f.jpg
Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Share:

MECHI KATI YA BRAZIL VS COLOMBIA: BRAZIL YAIFUNGA COLOMBIA MARA 15 KATIKA MECHI 25

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Nyota wa Brazil, Neymar akishangilia mojawapo ya mabao aliyoifungia timu yake katika fainali zinazoendelea

MECHI ya robo fainali baina ya Brazil na Colombia ni ya kwanza kabisa kwa timu hizo mbili za Amerika Kusini kupambana
kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Dunia, lakini ni ya 26 kuzikutanisha timu hizo katika historia yao.
Ukitazama rekodi vitabuni, unaweza kusema kwamba Colombia ni vibonde wa Brazil, kwani katika mechi 25 walizocheza tangu mwaka 1945 mpaka sasa, Brazil imeshinda jumla ya 15, kutoka sare mara nane na kufungwa mechi mbili tu.
Kwa ujumla wake, Brazil imefunga mabao 55-11, ikiwa ni rekodi kubwa mno ya mabao.
Timu hizo zimepambana mara 10 katika mashindano ya awali ya Kombe la Dunia ambapo katika mechi hizo Brazil imeshinda mara tano na kutoka sare mara tano pia.
Aidha, katika mashindano ya Ubingwa wa Amerika Kusini maarufu kama Copa America (zamani yakijulikana kama South American Championship), timu hizo zimepambana mara tisa na Brazil imeshinda mara saba, kutoka sare moja na kupoteza moja.
Zilipopambana katika mashindano ya 7 ya Kombe la Dhahabu (Gold Cup) kule Miami, Marekani mwaka 2003, Brazil ilishinda kwa mabao 2-0.
Share:

CCM YAWABEMBELEZA CUF KUREJEA BUNGE LA KATIBA-MWEZI WA NANE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,Vuai Ali Vuai
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ali Vuai, amesema ikiwa wajumbe wa Bunge la Maalum la Katiba kutoka Chama cha Wananchi (CUF) hawatorejea bungeni, wataikosesha Zanzibar fursa za kiuchumi.
Share:

MASAA MACHACHE KABLA YA MECHI YA ALGERIA NA GERMANY-KOCHA AKERWA NA SWALI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                     
Kocha Vahid Halilhodzic amesema swala kufunga au la ni la kibinfasi
Kocha wa timu ya taifa ya Algeria ambayo inashiriki kombe la dunia nchini Brazil, Vahid Halilhodzic amekataa kufichua idadi ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi yake na Ujerumani baadaye Jumatatu
Share:

DR SALIM AFICHUA SIRI YA JT NA TUME YA WARIOBA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                                                      “Ni vizuri viongozi wakaandaliwa, isiwe mtu anaibuka tu anagawa hela halafu anashinda. Anatakiwa mtu atakayeweza kushughulikia matatizo ya Watanzania. Watanzania ni wapole na wavumilivu lakini wanazungumza. Hivyo anahitajika kiongozi atakayesikiliza mahitaji yao na kutoa suluhisho, si kutoa ahadi za uongo,” Dk Salim Ahmed Salim
KWA UFUPI
Abainisha ilikuwa ikimpa taarifa kwa kila hatua iliyokuwa ikifikia, asema alishangaa kumsikia akiikosoa katika Bunge la Katiba
Dk Salim: Sina mpango na urais 2015
Share:

HAWA NDIO WASHINDI WA TUZO ZA BET 2014,BEYONCE ACHUKUA 3

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Pharrell Williams na Missy Elliot wakifungua shoo ya utoaji tuzo za BET usiku wa kuamkia leo jijini Los Angeles.
Share:

AVEVA ACHAGULIWA KUWA RAIS MPYA SIMBA SC

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Amin Bakhresa akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Simba SC.
Share:

Sunday, 29 June 2014

TANGAZO LA ORODHA YA MAJINA YA KUITWA KAZINI 27 JUNI 2014,KWA WAOMBAJI WALIOFANYA USAILI TAR.05 HADI 06 JUNE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY1
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na. EA.7/96/01/G/30 27 Juni, 2014 KUITWA KAZINI 

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 05 hadi 06 Juni, 2014  kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika tangazo hili.   Aidha, wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vipya vya kazi katika muda ambao umeainishwa katika barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.  Kwa Waombaji Kazi walioitwa katika Wizara ya Maliasili na Utalii wote kwa pamoja wanatakiwa kuripoti Chuo Cha Taifa cha Utalii Tandika, Wilayani Temeke tarehe 14/07/2014 Saa 2:00 Asubuhi Bila kukosa.
Barua za kuwapangia vituo vya kazi kwa walioitwa katika Taasisi ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba mara nafasi za kazi zitakapotangazwa tena. 
ANGALIA MAJINA HAYO...HAPA CHINI
Share:

MAJINA MAPYA YA VIONGOZI CUF TAIFA BAADA YA UCHAGUZI MKUU

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
1.MWENYEKITI PROFESA IBRAHIM LIPUMBA
2.KATIBU MKUUU......MAALIM SEIF

3. Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mhe. Magdalena Sakaya.

4. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
Share:

MWENYEKITI WA CCM KATA YA BUSAMBALA BUTIAMA afariki dunia-baada YA MAJAMBAZI KUMUUA


Watu  wanadhaniwa  kuwa ni majambazi wamemuua kinyama kwa kupiga  risasi moja ya kichwani mwenyekiti  wa chama cha mapinduzi  kata ya Busambala wilayani Butiama mkoani Mara Bw Willison Opio mwenye umri wa miaka 6o huku kichwa chake kikisambaratishwa  kabisa na risasi hiyo.
Share:

HOTUBA YA MH.MIZENGO PINDA-WAZIRI MKUU WAKATIA AKIFUNGA SHUGHULI ZA BUNGE JANA DODOMA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
PG4A9702
UTANGULIZI

a)    Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika,
1.    Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015.

2.    Napenda kutumia nafasi hii ya awali kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ya kutukuka ambayo wameifanya kwa nidhamu na ufanisi mkubwa, hususan wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Serikali na Mafungu ya Wizara za Kisekta. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi kwa kazi yao nzuri ya kuchambua Bajeti ya Serikali na Sheria zinazoambatana na masuala ya Bajeti. Changamoto zilikuwa nyingi,   lakini   kwa   pamoja   tumekubaliana   na   kuafikiana. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kwenda kushirikiana na Wananchi katika utekelezaji wa Bajeti hii ili kuwaletea maendeleo.

Mheshimiwa Spika,
3.    Katika kipindi hiki tukiwa hapa Bungeni, yapo matukio ya kusikitisha yaliyotokea ambapo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walipoteza Wapendwa wao. Aidha, yapo matukio ya Kitaifa yaliyosababisha kupoteza maisha ya Ndugu, Jamaa na Marafiki. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote waliofikwa na misiba na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wote waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki.

Mheshimiwa Spika,
4.    Kipekee niwape pole ndugu, jamaa na marafiki waliopotelewa na ndugu zao na wote waliopata majeraha wakati kulipotokea Mlipuko wa Bomu pale Darajani, Zanzibar. Tukio hili la kusikitisha halipendezi kwa Nchi yetu. Niwaombe Wananchi wote kwa umoja wetu tushirikiane kuwa Walinzi katika maeneo yetu na kuwezesha kuwatambua mapema wale wote wenye nia mbaya ya kuharibu amani na utulivu katika Taifa letu.

Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
2_0603b.jpg
Share:

TANGAZO KWA FORM IV WOTE MLIOKOSA NAFASI ZA KWENDA KIDATO CHA TANO 2014 ,SASA UTASOMESHWA BURE KABISA SOMA HAPA

INNOCENT-THE BLOGGER
Share:

Saturday, 28 June 2014

NAFASI MPYA ZA KAZI-KUJITOLEA KWA MUDA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Share:

MATOKEO BRAZIL NA CHILE:BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI KWA MATUTA,HONGERA CHILE

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY


WENYEJI Brazil wameitoa Chile kwa penalti 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mjini Uwanja wa Belo Horizonte, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
Share:

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI - JUNI 29

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

MWANAMKE ASALIMISHA SHANGA ZA MAJINI KANISANI SOMA HAPA

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mwanamke anayefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli akikabidhi shanga kwa Mchungaji Kiongozi, (Frank Endrew) wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani Arusha.Katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli hivi karibuni aliamua kukabidhi kanisani shanga za majini kwa kile alichodai kuwa, zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger