Tuesday, 13 May 2014

MAJUNGU TUPA KULE..!HUU NDIO UKWELI KUHUSU MAHUSIANO YA BOND NA WASTARA...!


ANATOKA KIMAPENZI NA WASTARA?
Nakukubali sana kaka Bond lakini napenda kukuuliza kwamba kuna madai kuwa unatoka kimapenzi na Wastara Juma (mwigizaji). 
 BOND: Siyo kweli. Mimi ni meneja wa Wastara. Pia ni mwongozaji wake wa filamu kwa hiyo tuna mikataba mingi ya kufanya kazi muda mrefu sana. UHUSIANO NA AUNTY LULU
Kiukweli kama una uhusiano na Aunty Lulu (Semagongo) mwache tu kwa sababu hutamuweza, skendo zake zinatisha lakini mimi nakushauri  usimuache hivihivi, mshauri vizuri, awe mwelewa kwani anatakiwa kuwa na msimamo mzuri. Msomaji, 0764158569.
BOND: Asante, Aunty Lulu nilishaachana naye muda mrefu lakini huwa naendelea kumshauri vitu vingi kwa hiyo yeye ndiye anayeamua kuchukua ushauri au kuacha. OA SASA
Kuwa na uhusiano ni sawa kwani umri unakata mbuga, kwa maoni yangu uoe sasa. Msomaji, 0785606175.
BOND: Asante nitalifanyia kazi hilo, namuomba Mungu anijalie.
USHAURI
Mimi napenda kuigiza na kipaji ninacho lakini bado mchanga kisanaa ila natamani kutimiza ndoto yangu nifanyeje? Naomba nisaidie. James Salamba, 0768558834.
BOND: Ongea vizuri na wazazi wako kwa sababu siku hizi kuna shule nyingi zinazofundisha sanaa ujiunge nazo au uende kwenye vikundi vya sanaa, naamini utatimiza ndoto yako.
FILAMU NGAPI? ANA MCHUMBA?
Mpaka sasa una filamu ngapi na je, una mchumba? Msomaji, Mwanza, 0765757273.
BOND: Nina filamu saba mpaka sasa na nina mchumba.
 UTULIVU
Nakukubali sana kaka ila naomba utulie. Mariam Said, Gairo, 0656977555.
BOND: Asante sana na mimi siku zote nimetulia huwa sihangaiki.
ALISHAKUWA TEJA?
Nasikia ulishawahi kuwa teja, ni kweli? Frank, Mwanza, 0752157695.
BOND: Sijawahi na ninamuomba Mungu aninusuru.
AUNTY LULU TENA Kwa ushauri wangu achana na umsahau kabisa huyo Aunty Lulu. Specioza, Mwanza, 076507479.
BOND: Asante ila kwa pamoja ninaomba tumuombee Aunty Lulu abadilike pia tuendelee kumshauri.
ILIKUWAJE?
Ilikuwaje mpaka ukaachana na Aunty Lulu maana mlikuwa mnapendana sana? Salumu Kabunda, Iringa, 0763236597.
BOND: Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, naona mwisho wetu ulikuwa wa hapahapa duniani.
WALIMWAGANA KITAMBO
Vipi kaka bado mnaendelea na uhusiano wa kimapenzi na Lulu Semagongo au mmeshamwagana? Zamrata Makame, Dar, 0688909490.
BOND: Tulishamwagana siku nyingi.

 NAOMBA AWE MCHUMBA WANGU
Bond namkubali kwenye mambo yake na kwa vile hajaoa naomba achukue namba yangu, nahitaji awe mume wangu. Ashura, Mtwara, 0712231020.
BOND: Nashukuru na nimefurahi kwa kunikubali ila nina mchumba tayari, nakuombea kwa Mungu akupatie mume mwema.
Share:

SOMA:-Ratiba ya ziara ya awamu ya Kwanza ya "UKAWA’’ -TANZANIA BARA" Tarehe 14 hadi 27 MEI 2014.


Katibu mkuu wa CHADEMA ,Dr. WILBROAD SLAA akizungumza na wanahabari mapema jana (May 12,2014) juu ya ziara yao ya nchi nzima.


Umoja wa Katiba ya Watanzania UKAWA jana(May 12,2014) umejitokeza na kutangaza rasmi ratiba yao ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu juu ya katiba mpya na mchakato huo ulipofikia sasa.
Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya makao makuu ya Chama cha Wananchi CUF ,katibu mkuu wa CHADEMA ,Dr. WILBROD SLAA amesema kuwa UKAWA sasa imeanza rasmi kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kila kona ya Tanzania kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwaeleza ukweli kuhusu mchakato wa katiba.

Katibu mkuu wa NCCR mageuzi MOSENA NYAMBABE akizungumza ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa UKAWA ambao watazunguka nchi nzima ,pamoja na mambo mengine kuelezea mchakato wa Katiba Mpya.

Dr. SLAA anasema kuwa kwa wale ambao wanasema kuwa UKAWA ni nguvu ya soda wanapotea, kwani muungano huo haujaja kwa bahati mbaya kwani wamejipanga kuhakikisha kuwa inawaeleza Watanzania ukweli juu ya katiba na jinsi chama cha mapinduzai CCM wanavyoupotosha umma juu ya mchakato huo.
Aidha Dr. SLAA amesema kuwa  kauli ambazo zilitolewa na viongozi wa juu wa chama cha mapinduzi CCM kuwa Tanzania haiitaji sana katiba mpya ni kauli za mtu ambaye hajafika darasani na ni kuwapotosha watanzania na kauli hizo zinatakiwa kupigwa vita sana kwani zinaupotosha umma.

JULIUS MTATIRO akizungumza katika mkutano huo.

Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mkutano huo wa UKAWA na wanahabari jana May 12,2014.

UKAWA wametangaza kufanya maandamano na mikutano kona zote za Tanzania kwa kuigawa Tanzania kwa kanda tatu ambazo ni KANDA YA KATI,KANDA YA KASKAZINI na KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI,ambapo viongozi kutoka vyama vitatu wakiwemo makatibu wakuu wote wataongoza mikutano hiyo ambayo itaanza rasmi tarehe 14 ,May ,2014.


"UKAWA INAANZA TANZANIA BARA" RATIBA YA ZIARA YA AWAMU YA KWANZA YA UKAWA, TAREHE 14 -  27 MEI 2014. 
TIMU “A”- KANDA YA KAT.
1. Mhe. Mosena Nyambabe (NCCR) – Katibu Mkuu.
2. Mhe. Ashura Mustapha (CUF)  –  Mjumbe wa Baraza Kuu. 
3. John Heche (CHADEMA)  –  Mwenyekiti wa Vijana Taifa.
  
TAREHE ENEO LA MKUTANO.
Tarehe 14/05/2014 MOROGORO MJINI.
Tarehe  16/05/2014 SHINYANGA MJINI.
Tarehe  17/05/2014 BARIADI MJINI.
Tarehe  18/05/2014 NZEGA MJINI.
Tarehe  19/05/2014 TABORA MJINI.
Tarehe  20/05/2014 URAMBO.
Tarehe  22/05/2014 NGURUKA.
Tarehe  23/05/2014 KIGOMA MJINI.
Tarehe  24/05/2014 MNANILA.
Tarehe  25/05/2014 KASULU MJINI.
Tarehe  26/05/2014 KASULU VIJIJINI.
Tarehe  27/05/2014 KIBONDO MJINI.
TIMU “B” –  KANDA YA KASKAZINI.
1. Dr Willibroad Slaa(CHADEMA)  –  Katibu Mkuu.
 2. Mhe. Mustapha Wandwi (CUF)  –  Mjumbe wa Baraza Kuu.
 3. Ahmed Msabaha (NCCR)  –  Mjumbe wa Halmashauri Kuu.
TAREHE ENEO LA MKUTANO.
Tarehe  14/05/2014 MOSHI MJINI.
Tarehe  15/05/2014 BABATI MJINI.
Tarehe  16/05/2014 ARUSHA MJINI.
Tarehe  18/05/2014 MUSOMA MJINI.
Tarehe  19/05/2014 TARIME MJINI.
Tarehe  20/05/2014 BUNDA MJINI.
Tarehe  21/05/2014 BIHARAMULO MJINI.
Tarehe  22/05/2014 BUKOBA MJINI.
Tarehe  23/05/2014 KARAGWE MJINI.
Tarehe  24/05/2014 NGARA MJINI.
Tarehe  25/05/2014 KATORO.
Tarehe  26/05/2014 GEITA MJINI.
TIMU “C” –  NYANDA ZA JUU KUSINI.
1. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba(CUF)  –  Mwenyekiti.
 2. Mhe. Said Issa (CHADEMA)  –  Makamu Mwenyekiti Taifa.
 3. Martin Juju Danda(NCCR)  –  Mjumbe wa Halmashauri Kuu. 
TAREHE ENEO LA MKUTANO.
Tarehe  15/05/2014 IRINGA MJINI.
Tarehe  16/05/2014 MAFINGA.
Tarehe  17/05/2014 MAKAMBAKO MJINI.
Tarehe  18/05/2014 NJOMBE MJINI.
Tarehe  19/05/2014 SONGEA MJINI.
Tarehe  20/05/2014 MBINGA MJINI.
Tarehe  22/05/2014 MBEYA MJINI.
Tarehe  23/05/2014 MOMBA.
Tarehe  24/05/2014 SUMBAWANGA MJINI.
Tarehe  25/05/2014 NAMANYERE.
Tarehe  26/05/2014 KATAVI MPANDA - MULELE (MAJIMOTO).
Tarehe  27/05/2014 MPANDA MJINI.


Aidha UKAWA umewataka wananchi wa maeneo yote yaliyotajwa mjiandae na awamu ya kwanza ya ziara hii. Awamu ya  pili itaendelea mwezi Juni na ziara za wabunge walioko bungeni mtatangaziwa.
Share:

SERIKALI YATANGAZA NAFASI MPYA ZA KAZI MAY 09 2014

SEKRETARIETI YA AJIRA INATANGAZA NAFASI ZA KAZI KWA NAFASI ZIFUATAZO MWISHO WA KUAPPLY NI 23rd MAY 2014.

BONYEZA HAPO CHINI KUCHEKI NAFASI HIZO ZA KAZI.

DOWNLOAD HAPA

Share:

Balaa la Snura awapo Sita kwa Sita yatishia kuvunja kitanda.

Balaa la Snura awapo Sita kwa Sita yatishia kuvunja kitanda.Staa  wa  kike  anayetikisa  kwenye  tasnia  ya  filamu  na  muziki, Snura  Mushi  a.k.a  Majanga  anadaiwa  kuwa  ni  mmoja  wa  mastaa  wa  kike  wenye  ujuzi  mkubwa  kimahaba  kiasi  cha  kuwapagawisha mno  wanaume  anaokuwa  nao  katika  mahusiano…..

Chanzo  chetu  cha habari  ambacho  kiko  karibu  na  staa  huyo  kilieleza  kuwa  Snura  huwa  na  tabia  ya  kupandisha  mzuka  wa  jukwaani  awapo  kwenye  sita  kwa  sita  na  wakati  mwingine  huweza  hata  kuvunja  kitanda  endapo  akiamua  kufanya  hivyo…..

 
“Unajua  Snura  anaasili  ya  kizaramo, Amefundwa  kila  aina  ya  mafunzo  ya  kuwa  na  mwanaume.Mimi  ni  rafiki  yangu  kwa  kipindi  kirefu, yaani  tokea  niwe  karibu  naye  wanaume  aliowahi  kuwa  nao  wamemsifu  kuwa  anaweza  mambo  tena  si  kitoto”, Kilieleza  chanzo  hicho
Inadaiwa  kwamba  asilimia  kubwa  ya  mastaa  wa  kike  huwa  hawapendi  kujishughulisha  wawapo  faragha  kutokana  na  ustaa  wao,lakini  taarifa  za  Snura  zimekuwa  tofauti….
Mwandishi  wetu  alimtafuta  Snura  ambaye  baada  ya  kumuuliza  aliangua  kicheko:
“Sasa  utamu  wa  ngoma  si  ni  lazima  uicheze? Huwezi  kujua  hivi  hivi.Hayo  mambo  ni  mazito  sana  naona  kwangu  ni  ngumu  kuyazungumzia  kwa  sababu  najiandaa  kuolewa. Ila  kwa  mwanamke  hasa  wa  taipu  yangu  ni  lazima  ujue  kumpetipeti  mume.
 
“Hilo  halinipi  shida  sana  sababu  nimekamilika  kila  idara.Mbele  ya  watu  kibao  shughuli  inakuwa  pevu  jukwaani  sembuse  chumbani  wawili  tu?”  Alisema  staa  huyo  anayefunika  Tanzania  na  ngoma  yake  ya  Nimevurugwa
Share:

Monday, 12 May 2014

BOKO HARAM WAONYESHA WASICHANA WALIOTEKWA

Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
CHANZO BBC SWAHILI
Share:

MAUAJI YA KUTISHA!! BODABODA ACHINJWA-KISARAWE II KIGAMBONI


Bi. Sakina, ambaye ni mama mzazi wa John Thobias akiweka shada la maua kwa uchungu.
Katekista Millinga akiweka msalaba.
Jeneza likiwa ndani ya kaburi.
Mwili wa marehemu ukipelekwa makaburi ya Magogoni-Kigamboni.
 Hizi ni pikipiki za vijana wa bodaboda zikiwa zimepaki jirani na msibani.
  Bodaboda wakijipanga toka nyumbani mpaka makaburini kwa ajili ya kuubeba mwili wa marehemu.
Bodaboda huyu alizuiwa kwa muda ili kwenda kuzika mwili wa mwenzao.
Bw. Joseph mjomba wa marehemu akiwa karibu na jeneza.
 John enzi za uhai wake.
Familia ya marehemu John ikiwa pamoja baada ya mazishi.
  Hiki ndicho kibanda kilichoandaliwa kwa ajili ya kufanyia tambiko ya mila kwa mwili wa John kabla ya kuagwa na kuzikwa.
MJI wa Kigamboni umegubikwa na majonzi mazito na vilio kutawala kila kona kufuatia kijana aliyefahamika kwa jina la John Thobias Joseph (19), dereva wa bodaboda maeneo ya Magogoni Kigamboni, kuchinjwa kisha pikipiki yake kuchukuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Inasemekana John, alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akimtaka akamchuke na kumpeleka Kisarawe II, baada ya maongezi, John alionekana kumfahamu mteja huyo na kumuahidi kumfuata.
Inasemekana John alikuwa amembeba mama yake mdogo wakitokea hospitali, ambapo alimshusha mama na kumfuata mteja huyo.
Akisimulia bodaboda mwenziye alisema “John huwa na taratibu za kufika kijiweni asubuhi (mtaa wa Tungi kwa Matenga ambapo anapaki) lakini siku ya tukio haikuwa hivyo, jambo lililowashangaza wenzake na mmoja wao akaamua kumpigia simu lakini iliita pasipo kupokelewa.
“Baada ya kumtafuta kwa muda bila mafanikio ndipo tukapata taarifa za kuwapo kijana mmoja aliyekutwa amekufa nje ya mji, ndipo tukaamua kwenda eneo la tukio na kumkuta ni John’’ alisema kijana huyo.

Aidha Katekista Millinga, akizungumza katika misa ya kuaga mwili wa marehemu huyo alisema, “Pengine wauaji wako hapahapa tulipo, sidhani kama wauaji wanatoka mbali, lakini maandiko yanasema, anayeuwa kwa upanga naye atauwawa kwa upanga."
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutaka familia na wanabodaboda wote kuwa wavumilivu wakati uchunguzi ukiendelea.
Aidha, amewataka vijana wa bodaboda kuwa makini na abiria wanaowakodi,wasivutike na pesa nyingi wanazoahidiwa.
John, ambaye alikuwa ni kijana mdogo sana kiumri na hata umbo, alikutwa na mauti siku ya Alhamisi tarehe 8/05/2014 majira ya saa 8 mchana eneo la Kisarawe II, nje kidogo na Kigamboni.
Marehemu alizikwa tarehe 10/05/2014 katika  makaburi ya Magogoni-Kigamboni, Dar.
Share:

UKAWA WAPIGWA MARUFUKU BUNGE LA BAJETI.


   
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema ni marufuku kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya shughuli zake ndani ya Bunge la Bajeti.

  

Alisema hayo juzi bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kutangaza baraza kivuli la mawaziri na kusema hicho ndiko kikosi cha ukawa ndani ya Bunge.
 
Spika Makinda alimtaka Mbowe kuhakikisha Ukawa inafanya kazi zake nje ya Bunge na si ndani ya Bunge kwani wanapokuwa ndani ya Bunge wanakuwa ni kambi ya upinzani bungeni na si vinginevyo.
“Ukawa ndani ya Bunge haipo, mnakumbuka shuka kumekucha, baraza lenu ni International Standard na miaka ya nyuma nilishawahi kuwashauri kitu kama hicho lakini mkakidharau na kuona hakina maana, nawapongeza sana, lakini mmekumbuka shuka kumekucha,” alisema.
Pia Spika Makinda alilitaka baraza hilo kivuli kutoa ushirikiano na wabunge wengine ili kufanya kazi ya kuendeleza watu.
“Watanzania hawajui nani anatoka wapi ila wanachotaka ni maendeleo yatakayosaidia kuboresha hali zao za maisha, wanataka kuona barabara nzuri na hata mazao yao yananunuliwa,” alisema.
Uteuzi huo ulihusisha vyama vya Chadema, CUF na NCCR Mageuzi ambapo baraza hilo kivuli lina mawaziri 29 ambapo watashika nafasi za uongozi katika kipindi kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
Share:

SUAREZ BINGWA WA MABAO LIGI YA ENGLAND 2013/2014

LICHA ya Liverpool kukosa ubingwa, lakini nyota wao Luis Suarez ametwaa kiatu cha mfungaji bora kwa kumaliza na mabao yake 31 akifuatiwa na Daniel Sturidge naye pia wa Liver mwenye mabao 21.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger