JESHI LA KUJENGA TAIFA LINAWATANGAZIA VIJANA WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KUWA WANATAKIWA KURIPOTI KWENYE MAKAMBI WALIYOPANGIWA KUANZIA TAREHE 04 SEPTEMBA 2014 NA MAFUNZO YATAANZA RASMI TAREHE 11 SEPTEMBA 2014.
AIDHA JKT LINAKANUSHA UVUMI UNAOSAMBAZWA KWA KUTUMIA UJUMBE MFUPI KWA NJIA YA SIMU "SMS" NA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUWA MAFUNZO HAYO HAYATAKUWEPO. TAARIFA HII SI YA KWELI BALI NI UZUSHI NA UPOTOSHAJI.
INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
VIJANA WANAOTAKIWA KURIPOTI NI KAMA IFUATAVYO:-
1. WALIMU WOTE NGAZI YA CHETI (GATCE) 2014. (WALIOMALIZA MWAKA 2014)
2. WALIMU ELFU TATU NGAZI YA DIPLOMA (DSEE). (WALIOMALIZA MWAKA 2014)
3. VIJANA KIDATO CHA SITA AMBAO HAWAJAANDIKA BARUA ZA KUOMBA KUAIRISHA KAMA ILIVYOTOLEWA MAELEKEZO AWALI.
MAJINA YA VIJANA NA VIKOSI WALIVYOPANGIWA YANAONEKANA KATIKA TOVUTI YA JKT ww.jkt.go.tz .
N.B VIJANA WENYE ULEMAVU UNAOONEKANA WALIPOTI KATIKA KAMBI YA RUVU. MARA WATAKAPORIPOTI RUVU WATAFANYIWA UCHUNGUZI NA JOPO LA MADAKTARI ILI KUBAINI ULEMAVU WAO ILI WAWEZE KUPEWA MAFUNZO KULINGANA NA ULEMAVU WALIONAO.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
AKSANTE KWA KUTEMBELEA MASWAYETU BLOG
0 comments:
Post a Comment