BARAZA LA MITIHANI LA
TANZANIA
|
Baadhi
ya wadau wamekuwa wakitaka kujua utaratibu uliotumika kukokotoa pointi za
madaraja katika matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2014. Hii
imetokana na kuona kuwa kuna baadhi ya masomo hayakujumuishwa katika kupata
idadi ya pointi kwa watahiniwa wa Tanzania Bara na wale wa Zanzibar.
Baraza
la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha wadau wote kuwa ukokotoaji wa
pointi za madaraja kwa watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Sita huzingatia
masomo ya Tahasusi (Subject Combinations) aliyoyasoma mtahiniwa kama
ilivyobainishwa katika Kanuni za Mitihani (The Examinations Regulations) Toleo
la mwaka 2013 kifungu cha 23(1) kinachosomeka:
“The Advanced Certificate of Secondary
Education shall be awarded in four Divisions to both schools and private
candidates who have conformed to entry requirements and have fulfilled the
conditions of the awards. Calculations of points shall be done based on Subject
Combinations approved by the Ministry of Education”,
Masomo
ya Tahasusi (Subject Combinations) yanayotumika kukokotoa alama za
madaraja yamebainishwa katika Waraka
Namba 1 wa mwaka 2006 wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi na Waraka Kumb. Namba P33/8/53/Vol.I/44 wa mwaka 2012 wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali, Zanzibar.
Baadhi
ya Tahasusi zinazotumika Zanzibar zinatofautiana na zilizopo Tanzania Bara,
ambapo kwa Zanzibar zipo baadhi ya Tahasusi zenye kuhusisha masomo ya hiari.
Masomo ya hiari ambayo husomwa na baadhi ya watahiniwa ni pamoja na General Studies (GS), Islamic
Knowledge, Basic Applied Mathematics (BAM), Divinity, Computer Studies na
Arabic Language. Hata hivyo, Baraza la Mitihani hufanya tathmini na kutunuku
ufaulu kwa masomo yote ya hiari ya mtahiniwa katika cheti chake ili kimsaidie
katika udahili wa ngazi mbalimbali za mafunzo kulingana na matakwa ya sifa za
mafunzo husika.
Taarifa
za kina kuhusu utaratibu wa kutunuku matokeo ya Kidato cha Sita zipo katika
kitabu cha Mwongozo wa Matumizi ya
Viwango vya Ufaulu na Utaratibu wa Kutunuku Matokeo ya Kidato cha Nne na cha
Sita kilichotolewa mwaka 2014.
Aidha, kitabu hicho kilikabidhiwa kwa
Wakuu wa Shule zote za sekondari Tanzania Bara na Zanzibar. Pia kitabu hicho
kinapatikana kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania (www.necta.go.tz).
Baraza
la Mitihani la Tanzania linawaomba wadau wasipotoshwe na taarifa ambazo
zinasambazwa katika baadhi ya vyombo vya
habari na mitandao ya kijamii ambazo zina lengo la kupotosha Umma.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO
ASANTE KWA KUTEMBELEA MASWAYETU BLOG BE BLESSED
0 comments:
Post a Comment