Wednesday 2 January 2019

AUAWA KWA KUKATWA PANGA NA RAFIKI YAKE KISA KAMTANIA KWA KUMUITA 'ALBINO'

Mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya sekondari Naisinyai wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara Godfrey Otieno (16) amefariki dunia kwa kukatwa panga kichwani na rafiki yake baada ya kumtania kwa kumuita albino.

Watoto hao ambao ni marafiki na majirani walikuwa pamoja wakisubiria kushangilia mwaka mpya wa 2019 ambao uligeuka kuwa kilio.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Agostino Senga akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Januari 2, 2019 amesema tukio hilo limetokea Desemba 31, 2018 saa tatu usiku katika kitongoji cha Songambele kata ya Mirerani wilayani Simanjiro.

Amemtaja anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni George Damas (15) mwanafunzi aliyemaliza shule ya msingi hivi karibuni na kufaulu, alikuwa akisubiri kupangiwa shule ya sekondari.

Ametaja chanzo cha kifo hicho ni utani kwani Otieno alimtania mwenzake kwa kumwita albino ndipo akakasirika na kuchukua panga na kumkata kichwani.

"Baada ya Otieno kukatwa na panga alikimbizwa kwenye kituo cha afya Mirerani lakini alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu," amesema kamanda Senga.

Amesema wanamshikilia Damas huku wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.

Na Joseph Lyimo, Mwananchi 
Share:

RAIS MAGUFULI ASHIKA NAFASI YA PILI ORODHA YA VIONGOZI BORA AFRIKA

Rais John Magufuli ameshika nafasi ya pili kati ya marais watano bora Afrika kwa mwaka 2018 kutokana na kazi aliyoifanya ndani ya miaka mitatu ya utawala wake, jarida la mtandaoni la Africa54 limebainisha.

Jarida hilo lilifanya utafiti wake kwa kuuliza wasomaji wake nani ni Rais bora kwa mwaka wa 2018, kiongozi ambaye hafanani na viongozi wengine wa Afrika; ufanisi wake katika kazi, msimamo, ujasiri na uongozi na matokeo makubwa.

Africa54 limebainisha kwamba, Rais Magufuli amefanya maajabu katika muda wa miaka mitatu ambao amekaa madarakani kuliko kiongozi mwingine. Ameweza kutoa elimu bure, amefufua shirika la ndege na kununua ndege saba, ameanza kujenga reli ya kisasa (SGR) na ameongeza upatikanaji wa huduma za afya. Pia anafahamika kwa kupiga vita rushwa na ufisadi.

Nafasi ya kwanza kwa mujibu wa utafiti huo imechukuliwa na Rais wa Botswana, Ian Khama. Jarida hilo limeandika Rais Khama ni kiongozi mtulivu ambaye ameleta mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi ikiwamo kuboresha miundombinu, upatikanaji wa huduma za jamii na upatikanaji wa ajira nchini kwake.

Limesema licha ya kuwa kiongozi huyo amestaafu Aprili mwaka huu, bado Waafrika wengi wanamuona kama kiongozi bora ambaye hana mfano barani Afrika.

Nafasi ya tatu imekwenda kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ambaye aliingia madarakani Aprili mwaka huu inaonyesha kuwa alipendwa ghafla na wananchi wengi nchini humo.

Africa54 limesema kiongozi huyo amefanikiwa kuibadilisha Ethiopia kuwa nchi ya kidemokrasia zaidi na jamii iliyo huru.

Ghulib-Fakim wa Mauritius anachukua nafasi ya nne miongoni mwa marais bora wa Afrika. Jarida hilo linabainisha licha ya kuondolewa madarakani kwa kashfa ya kadi ya malipo, alisimamia haki na maendeleo ya watu katika nchi yake.

Nafasi ya tano inakwenda kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda. Limesema licha ya kiongozi huyo kuminya demokrasia, Waafrika wengi wanampenda kwa sababu amefanikiwa kulibadilisha Taifa lake kuwa kitovu cha uchumi Afrika Mashariki.
Share:

ORODHA YA SIMU AMBAZO HAZIKAMATI TENA WHATSAPP, NA ZINAZOKARIBIA KUFUNGIWA


Wamiliki wa simu zinazotumia programu endeshi ya simu aina ya Series 40 wamekuwa hawawezi tena kutumia mtandao wa WhatsApp kwenye simu zao.

Hiyo imetokana na uamuzi wa kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao wa kijamii wa WhatsApp wa kuacha kutengeneza app yake kwa njia ambayo inaweza kutumiwa katika simu hizo.

Wengi zaidi wataathirika katika kipindi cha mwaka ujao, 1 Februari, 2020 ambapo simu nyingi zikiwemo baadhi ya iPhone zitapoteza uwezo wa kutumia WhatsApp.

Hata kabla ya wakati huo kufika, Facebook wameonya kwamba "kwa sababu hatutakuwa tukitengeneza na kuboresha app yetu tukizizingatia, huenda baadhi ya uwezo wake ukaathirika wakati wowote."

Zitakazoathirika mwaka ujao ni za Android zinazotumia Android 2.3.7 na miundo ya awali, pamoja na iPhone zinazotumia iPhone iOS 7 kwenda nyuma. Kwa sasa, mfumo wa Android umefikia 9.0. [Unaweza kuangalia mfumo unaotumiwa na simu yako kwenye 'Settings', kisha sehemu ya 'Software/Software Info]

Wanaotumia Android 2.3.7 kwenda nyuma hawawezi kufungua akaunti mpya za WhatsApp.

Ndipo uweze kutumia mtandao huo kwa sasa unahitajika kuwa unatumia Android 2.3.3 kwenda juu na Windows Phone 8.1 kwenda juu.

Kwa sasa, walioathirika zaidi ni wanaotumia baadhi ya simu za Nokia zinazotumia mfumo endeshi wa Series 40 ambao wakati mwingine huitwa S40 OS. Miongoni mwa simu maarufu zilizoathirika ni Nokia 6300.

Simu ya mwisho kutengenezwa ambayo ilikuwa inatumia S40 ilikuwa Nokia 515 ambayo ilizinduliwa mwaka 2013.

Ingawa baadhi ya simu hizi ni za bei nafuu na hutumiwa na watu wa kipato cha wastani au cha chini, kuna wanaotumia simu aina ya pia simu za Vertu Signature S ambazo zilikuwa ghali sana na ambazo hutumia programu hiyo endeshi pia.

Wakati wa kuanza kuuzwa kwa simu hizo zilikuwa zinauzwa takriban £8000 (Tshs23m; Kshs1m), ingawa hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita na huenda wengi wao wamenunua simu nyingine au wana uwezo wa kununua simu nyingine kwa urahisi.

Simu zilizoathirika kwa sasa

  • Nokia 206 Single SIM na dual SIM
  • Nokia 208
  • Nokia 301 Single SIM na dual SIM Chat Edition
  • Nokia 515 zinazouzwa zikiwa na WhatsApp
  • Nokia Asha 201
  • Nokia Asha 205 Chat Edition
  • Nokia Asha 210
  • Nokia Asha 230 Single SIM na dual SIM
  • Nokia Asha 300, 302, 303, 305, 306, 308, 309, 310, 311
  • Nokia Asha 500, 501, 502, 503
  • Nokia C3-00
  • Nokia C3-01
  • Nokia X2-00
  • Nokia X2-01
  • Nokia X3-02
  • Nokia X3-02.5
Simu ambazo haziwezi kutumia WhatsApp na tarehe ya kuacha kutumia
  • Nokia Symbian S60 baada ya Juni 30, 2017
  • BlackBerry OS na BlackBerry 10 baada ya Desemba 31, 2017
  • Windows Phone 8.0 na miundo ya awali Desemba 31, 2017
  • Nokia S40 baada ya Desemba 31, 2018
  • Android 2.3.7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020
  • iPhone iOS 7 na miundo ya awali baada ya Februari 1, 2020

Simu nyingine zisizotumia WhatsApp

Kufikia Juni mwaka 2017, huduma ya WhatsApp pia ilikuwa imeacha kutumika tena katika aina kadha za simu za zamani zikiwemo zile zilizotumia mfumo wa Windows Phone 7.1, Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6.

Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo ilisema wakati huo kwamba inataka kuangazia kustawisha "huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi."


Kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha simu za BlackBerry OS, BlackBerry 10, Nokia S40 na Nokia Symbian S60 kuwa miongoni mwa simu ambazo zingekatiwa huduma mwishoni mwa mwaka 2016 lakini ikabadilisha uamuzi wake na kuongeza muda hadi Juni 30, 2017.

Simu zilizotumia Android 2.1 na Android 2.2, na simu aina ya iPhone 3GS/iOS 6 hata hivyo zilifungiwa mwishoni mwa 2016.

Hatua hiyo ilikuwa imetangazwa na Facebook mapema mwezi Februari mwaka 2016.

Kampuni hiyo ilijitetea na kusema kwamba haikusudii kuwatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

"Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo," kampuni hiyo ilisema.WhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani

Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawawezi kutumia WhatsApp:

  • Android 2.1 na Android 2.2
  • Windows Phone 7
  • iPhone 3GS/iOS 6
  • BlackBerry OS and BlackBerry 10
  • Nokia S40
  • Nokia Symbian S60



Wanaotumia simu zilizofungiwa wameshauriwa kununua simu za kisasa zaidi.

Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.Simu ya Blackberry

Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.

Chanzo- BBC
Share:

MANARA AKERWA NA BABA YAKE AMTUMIA UJUMBE MZITO


Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amefunguka kuwa kitendo cha Baba yake mzazi, Sunday Manara ambaye aliichezea klabu ya Yanga zamani kuonekana bado akishirikiana na timu hiyo kinamuumiza.


Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo amesema kuwa hakupenda baba yake achezee klabu hiyo ya mahasimu wake wa jadi lakini hawezi kurithi ushabiki wa timu hiyo.

"Daaah, huyu ni baba yangu mzazi na nampenda sana ila hata sijui kwanini, alicheza hili timu na nnajua hivi sasa Yanga wanajitahidi kumtumia ili kunififisha mimi , lakini hawataweza, yeye ni Gongowazi mimi ni Simba. Duniani watu hurithi mali, hawarithi ushabiki wa timu", ameandika Manara.

Manara ameendelea kusema kuwa, "Baba yangu muda ni huu, achana na hiyo mitimu ya ajabu ajabu, hiyo timu unayoshabikia ni ya watu wa zamani enzi za kina Unju bin Unuki, njoo Simba kuna Chama na kina Kagere, halafu yupo MO na mwanao, baba, baba tafadhali mimi mwanao nisikilize".

Hivi karibuni Baba mzazi wa msemaji huyo, mzee Sunday Manara alizungumza na wanahabari na kutoa shukurani kwa kocha wao Mwinyi Zahera ambaye ameonesha kuibeba klabu hiyo katika kipindi ambacho timu inakabiriwa na ukata wa fedha.

Share:

FID Q AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE

Msanii wa muziki Bongo, Fid Q amefunga ndoa na mpenzi wake jana. Hatua hiyo ikuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu Fid Q alipomvisha pete ya uchumba mpenzi wake huyo.
Share:

WAKULIMA WA KOROSHO WAMBANA DC MASASI, WATAKA WALIPWE PESA ZAO


Mkuu wa Wilaya ya Masasi Selemani Mzee amelazimika kufanya kikao cha dharula na baadhi ya wakulima wa Vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS, baada ya baadhi ya wakulima kufika ofisini kwake wakilalamikia kuhusu ulipwaji wa fedha zao za korosho.

Kwa mujibu wa madai ya wakulima hao ni kwamba zoezi la uhakiki wa mashamba ambao lilitangazwa na serikali limekuwa likilegalega huku baadhi yao wakishindwa kulipwa fedha zao licha ya kuuza korosho yao kwa serikali.

Akizungumza kwenye mkutano huo na baadhi ya wakulima na viongozi wengine vyama hivyo vya msingi, Mkuu wa Wilaya amekiri kusuasua kwa zoezi hilo na kudai atalifanyia kazi.

"Nawaomba muwe wavumilivu kwa kuwa kila mkulima ambaye ni mkulima halali, lazima atalipwa fedha zake," amesema Mzee.

"Kuhusu suala la ukaguzi wa mashamba, hili nitakaa na wahusika kujua tatizo liko wapi, lakini ni lazima serikali iwalipe wakulima kupitia taratibu zake ambazo zinalenga kuhakikisha anayelipwa ni mkulima halali," ameongeza Mzee.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Wilaya, mmoja wa wakulima hao ambaye ameuza korosho zake kwenye Chama cha Msingi Tuaminiane (AMCOS), Saidi Khatau, alisema ni miongoni mwa wakulima wanaotakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mashamba yao. Alisema wanashangaa kuona ahadi ya serikali ya kukagua mashamba yao haitekelezwi licha ya kuuza korosho.

Share:

MWANAMKE ATAFUNWA KALIO NA SIMBA AKIMPELEKA MTOTO HOSPITALI

Mkazi wa Kijiji cha Kata ya Ngwala, wilayani Songwe, Susan James, amenusurika kufa baada ya kuvamiwa na simba na kutafunwa kalio lake la kushoto wakati akimpeleka mtoto wake hospitali.

Diwani wa kata hiyo, Donald Maganga, alithibitisha mwanamke huyo kunusurika kifo baada ya kuvamiwa na simba huyo.


Alisema baada ya simba huyo kumjeruhi mwanamke huyo, aliondoka na kuwaacha mama huyo na mtoto wake na kwamba ni kitendo cha kumshukuru Mungu kwa kuwa mnyama huyo anapomvamia mtu anakula kila kitu na kubakiza kichwa na viganja vya mikono.


Alisema, wananchi kwa kushirikiana walimchukua mama huyo na kumpeleka zahanati ya kijiji ambako alipatiwa matibabu na baadaye walimpeleka hospitali teule ya Mwambani, iliyopo makao makuu ya wilaya kilometa 120 kutoka kwenye kata hiyo.


Alisema mbali na tukio hilo, pia kulikuwapo na tukio la mke na mume wakiwa na mtoto wao kuvamiwa na simba ambaye alimtafuna mtoto wao na wao kunusurika.


Alisema kupitia tukio hilo, anatoa rai kwa wananchi hasa wageni wanaoingia kwenye maeneo hayo kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo kuwa makini na wanyama waliopo mbugani.


Aliwaomba watu wa maliasili kuwa waangalifu kwa kuwanusuru wananchi wanaoishi karibu na mbuga hiyo kuwaepusha na majanga ya kuvamiwa na wanyama.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwambani, Dk. Kusenge Benangode, alithibitisha kumpokea mwanamke huyo ambaye amepatiwa matibabu na hali yake ikiendelea vizuri.
Share:

MBARONI KWA KUMUUA MAMA YAKE KWA KISU DODOMA

Jeshi la Polisi linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Moleti Wilaya ya Kongwa, mkoani hapo, Peter Mgomba (26), kwa madai ya kumuua mama yake mzazi kwa kumchoma kisu tumboni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, jiijini hapo juzi.

Kamanda Muroto alisema tukio hilo lilitokea Desemba 29, katika Kijiji cha Moleti, Tarafa Mlali, Wilaya ya Kongwa.

Alisema tukio la mauaji linadaiwa kufanyika wakati Mgomba alipomchoma kisu tumboni mama yake mzazi, Anita Mgomba (61) na kusababisha kifo.

Alisema chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, lakini wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Hata hivyo, Kamanda Muroto alisema mtuhumiwa anasadikiwa kuwa ni mgonjwa wa tatizo la akili na baada ya kufanya tukio alitoroka, lakini jeshi hilo lilimtafuta na kumtia nguvuni.


Alisema siku ya tukio, Anita alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini, lakini akiwa kwenye matibabu Desemba 30, alifariki dunia.
Share:

Tuesday 1 January 2019

SABABU KWANINI JANUARI NDIYO MWEZI WA KWANZA WA MWAKA


Kila mwaka tarahe kama hii watu kutoka kote duniani hukaribisha mwaka mpya kwa fataki, kupiga filimbi, pambaja na vinywaji.

Lakini kabla ya kuanza sherehe hizo je hujafikiria ni kwa nini tarehe mosi Januari ndio inayoadhimisha kuanza kwa mwaka mpya?

Kila kitu kinatokana na mila na tamasha za Roma, na kalenda iliozinduliwa na Julius Caesar miaka 2000 iliopita.

Lakini pia huwezi kumwacha nje papa aliyejulikana kwa jina Gregorio wa kumi na tatu.

Hebu tuone ni kwa nini?

Kwa Waroma wa zamani .Januari ilikuwa muhimu kwa sababu ulikuwa mwezi uliotakaswa kwa mungu Janus (hivyobasi ukaitwa Ianuarius, ikimaanisha Januari kwa kilatino.}"Inahusishwa na kuangalia mbele na nyuma," anaelezea Diana Spencer, profesa katika Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza.

"Kwa hiyo ikiwa kuna muda katika mwaka ambao unapaswa kuamua, huu ndiyo wakati tunapoanza tena." Ni mantiki kuwa hivi ".

Pia unafanana na muda kama ule wa Ulaya ambapo siku zinaanza kuwa ndefu baada ya msimu wa baridi.

"Waroma walihusishwa nao sana kwa sababu hutokea baada ya siku fupi, wakati ambapo dunia ina giza ,baridi na hakuna kitu kinachomea, kulingana na Professa Spencer.

''Ni Muda wa kupumua na kutafakari''.

Baada ya Waroma kuwa na mamlaka zaidi, walianza kusamabaza kalenda yao katika ufalme wao mkubwa.Kulingana na itikadi za Roma, Janus ni mungu wa nyuso mbili, mwanzo na mwisho .

Lakini katika miaka ya kati , baada ya kuanguka kwa ufalme wa Roma , Ukristo uliakuwa umejiimarisha hivyobasi tarehe mosi januari ilionekana kuwa tarehe ya Kipagani.

Mataifa mengi yaliotawaliwa na Ukristo walitaka mwaka mpya kuadhimishwa tarehe 25, ambayo inaadhimisha tarehe ambayo malaika Jibreel alijitokeza kwa bikra Mariam mtakatifu.

''Ijapoikjuwa siku ya krisimasi ni siku ya kuyzaliwa kwa Yesu, tarehe muhimu ni wakati malaika huyo alipomwambia Mariam kwamba atajifungua mwana'', Spence aliambia BBC.

Huo ndio wakati ambapo hadithi ya Yesu ilianza , hivyobasi ilikuwa na maana kuu kutaka mwaka mpya kuanza siku hiyo.HPapa Gregorio wa 13 alishinikiza mwanzo wa mwaka kuwa mwezi Janurai badala ya mwezi Machi.

hatahivyo Uingereza ambayo ilipinga amri ya papa na kuchukua dini ya Wapinzani wa papa waliendelea kusherehekea Machi 25 hadi mwaka 1752.

Mwaka huo sheria ya bunge la Uingereza ilioana ile ya mataifa menbgine ya Ulaya.

Leo, mataifa mengi huongozwa na kalenda hiyo ya Gregorian, na ndio sababu fataki hupigwa kote duniani ifikiapo tarehe mosi mwezi januari kila mwaka.

Katika karne ya kumiIn the sixteenth century, Pope Gregory XIII introduced the Gregorian calendar, and January 1 was restored as a new year in Catholic countries.
Chanzo - BBC
Share:

DAWA INAYOZUIA UKIMWI KUSAMBAZWA BILA MALIPO 2019 CHILE

Matumizi ya PrEP lazima yaambatane na utumizi wa mipira ya kondomu.

Miji kama London, San Francisco na New York inasajili visa vichache vya maambukizi ya virusi vya HIV na wataalam wanadai kwamba hii inatokana na kupatikana kwa dawa kwa jina PrEP.

Iwapo itatumika kila siku PrEP ina uwezo wa kupunguza asilimia 90 ya uwezekano wa mtu kuambukizwa ukimwi kupitia ngono ama asilimia 70 kwa kutumia sindano ambayo ina viini au kutumiwa na watu kadhaa kulingana kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Marekani CDC.

Kampuni ya kuuza dawa ya Gilead ilianza kuuza dawa hizo mwaka 2012 chini ya chapa cha Truvada.

Na, miaka mitatu baadaye, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilianza kupendekeza matumizi yake ili kuzuia Ukimwi miongoni mwa vikundi vilivyo katika hatari kubwa ya maambukizi , kama vile mashoga, wanaume wa kijinsia na washirika wao wa kike, makahaba na wanandoa ambao mmoja wao ameambukizwa ukimwi.

Lakini wakati matokeo yake yameonekana tayari katika nchi zilizoendelea, bei ya juu ya matibabu haya yameifanya kutowafikia wale waliopo katika maeneo ya maambukizi.PrEP ina emtricitabine na tenofovir, dawa mbili ambazo hutumiwa katika kupambana na virusi

Kwa mfano, Chile ni moja ya nchi 10 ulimwenguni ambapo matukio mapya ya wagonjwa wa VVU yaliongezeka kwa zaidi ya asilimia 50 kati ya 2010 na 2017, kulingana na Mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu VVU / UKIMWI (UNAIDS).

Na huko PrEP inauzwa kati ya US $ 575 na US $ 645 kwa mwezi, kulingana na vyombo vya habari katika nchi hiyo.

Katika robo ya kwanza ya 2019, hata hivyo, serikali itasambaza bila malipo kama sehemu ya mpango wa kitaifa wa kupambana na UKIMWI, tangu maambukizi mapya yaongezeke mara mbili kati ya 2010 na 2017, kulingana na Taasisi ya Afya ya Umma ya Chile (ISP) ).

Lakini inafanya kazi vipi?

Madhara

PrEP ina emtricitabine na tenofovir, dawa mbili ambazo hutumiwa katika kupambana na virusi kwa sababu hupunguza kiwango cha virusi katika damu na kuzuia kuongezeka.

Haifanyi kazi kama chanjo, kwani haizalishi antibodies, lakini ulaji wake wa kila siku ni muhimu ili emtricitabine na tenofovir ziwepo katika damu wakati wa maambukizi na kuzuia VVU kuanzishwa katika mwili, CDC inaelezea .

Hata hivyo, PrEP haitumiwi na kila mtu. Kabla ya kuanza kuitumia, ni lazima ihakikishwe kwamba mgonjwa tayari ameambukizwa na virusi.

Pia ni muhimu kuthibitisha hali nzuri ya figo na ini, kwa sababu kidonge kinaweza kusababisha matatizo katika viungo hivi.
Wataalam wanashauri kupunguza matumizi yake kwa wale ambao wana hatari ya kuambukizwa VVU, kwa sababu matibabu yanaweza kusababisha madhara kama vile kichefuchefu, tumbo, kupumua au maumivu ya kichwa na, katika hali mbaya zaidi, kukusanya asidi ya lactic katika damu.

Aidha, wale wanaosumbuliwa na hepatitis B wanapaswa kuwa makini sana, kwa sababu kama wanaanza kutumia Truvada na kisha kuacha matibabu, kuna uwezekano mkubwa kuwa na hepatitis mbaya.
Chanzo - BBC
Share:

SALAH,MANE NA AUBAMEYANG KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA - CAF


Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, Sadio Mane na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Merick Aubameyang ndiyo wachezaji watatu wa mwisho wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Orodha hiyo ni marudio ya wachezaji watatu waliotajwa kuwania tuzo ya msimu uliopita, ambapo itatolewa kwa kuzingatia kiwango cha mchezaji husika katika mwaka 2018.

Pierre-Merick Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon, amefanikiwa kuwepo katika listi ya mwisho ya wachezaji watatu wa tuzo hizo kwa mara ya tano mfululizo sasa tangu mwaka 2014 na kuifikia rekodi ya mkongwe wa Ivory Coast, Yaya Toure na wa Ghana, Michael Essien.

Mohamed Salah ambaye aliweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kushinda tuzo hiyo tangu ilipoasisiwa mwaka 1992. Ametajwa katika listi ya wachezaji watatu wa mwisho kwa miaka miwili mfululizo huku akishinda kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

Kwa upande wa Sadio Mane, ametajwa katika listi ya wachezaji watatu wa mwisho wa tuzo hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku akiwa hajashinda tuzo hiyo mpaka sasa.

Kilele cha tuzo hizo kinatarajiwa kufanyika Januari 8, 2019 mjini Dakar, Senegal.
Share:

CCM YAITAKA AFRIKA IKATAE KUBURUZWA NA WAKOLONI WAPYA

Morogoro Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro kimesema vyama vya siasa katika mataifa yalioendelea havifanyi mikutano ya hadhara wala maandamano bila vibali mara baada ya chaguzi kuu kumalizika lakini inashashangaza mikutano hiyo ikishinikizwa ifanyike Barani Afrika. Kimeeleza maendeleo yaliopatikana Marekani na ulaya yangekawia mno iwapo wananchi wake wangepuuzia kazi za uzalishaji mali,kujiendeleza kielimu na kundekeza siasa kama inavyotakiwa ifanyike katika nchi za ulimwengu wa tatu . Msimamo huo ulitolewa jana na katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka,kwa nyakati tofauti akiwa ameambatana na secretarieti ya CCM mkoa wa…

Source

Share:

CCM YAITAKA AFRIKA IKATAE KUBURUZWA NA WAKOLONI WAPYA.

  Morogoro Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro kimesema vyama vya siasa katika mataifa yalioendelea havifanyi mikutano ya hadhara wala maandamano bila vibali mara baada ya chaguzi kuu kumalizika lakini inashashangaza mikutano hiyo ikishinikizwa ifanyike Barani Afrika. Kimeeleza maendeleo yaliopatikana Marekani na ulaya yangekawia mno iwapo wananchi wake wangepuuzia kazi za uzalishaji mali,kujiendeleza kielimu na kundekeza siasa kama inavyotakiwa ifanyike katika nchi za ulimwengu wa tatu . Msimamo huo ulitolewa jana na katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka,kwa nyakati tofauti akiwa ameambatana na secretarieti ya CCM mkoa…

Source

Share:

MWANAMKE AUAWA KISHA KUFUNGIWA NDANI YA BANDA LA NG'OMBE


Mkazi wa Kijiji cha Luhega, Wilaya ya Tanganyika, Milembe Manoni (22), amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani, kisha mwili wake kufungiwa ndani banda ng’ombe.


Akizungumzia tukio hilo jana, kaka wa marehemu, Nestory Malongo alisema lilitokea juzi usiku nyumbani kwa marehemu.

Alisema taarifa ya kuuawa kwa Milembe aliipata saa tatu asubuhi na wasamalia wema,

Baada ya kupata taarifa hizo, alikwenda eneo la tukio na kukuta watu wengi wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba.

Alisema baada ya kuona mwili hiyo, waliona majeraha sehemu za kifuani ambayo inaonyesha alichowa na kisu.

Alisema polisi walifika eneo hilo, kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuufanyia uchunguzi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi .

Mama wa marehemu, Tuma Matine alisema alipigiwa simu na mkwe wake na kusisitiza kitendo hicho ni cha kikatili mno.

Alisema katika nyumba hiyo, binti yake alikuwa akiishi na mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga mifugo ya ng’ombe.

“Nasikitika baada ya tukio hili huyu mfanyakazi hajaonekana nyumbani…inawezekana wazi ndiye aliyehusika na kifo hiki,”alisema.

Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa mifugo wa Mkoa wa Katavi, Mussa Kabushi alisema kumekuwapo na mauaji ya mara kwa mara ya kuuawa kwa wafugaji.

Alisema mauaji hayo, yamekuwa yakisababishwa kutokana na tabia ya wafugaji kukaa kwenye maeneo ya kujitenga na kutokuwa na ulinzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.
Na Walter Mguluchuma – Katavi
Share:

MWALIMU ALIYEFUNGIA KABATINI MTOTO WA HOUSEGIRL ATEMBEZEWA KICHAPO

JESHI la Polisi limelazimika kumtia tena mbaroni Anitha Kimaro, ambaye anadaiwa kumfungia kabatini mtoto wa miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake na kuanza kumtembezea kichapo huku wakipinga hatua ya polisi kumpa dhamana.

Anitha ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Chadulu mjini Dodoma, anatuhumiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani (jina linahifadhiwa), kwa kumpiga na kumjeruhi, huku akimfungia ndani ya kabati mtoto wake wa miezi sita Mtaa wa Makongoro, Kata ya Kiwanja cha Ndege.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema waliamua kumkamata tena Anitha kutokana na usalama wake uraiani kuwa mdogo.

Alisema awali walimkamata mtuhumiwa huyo, lakini ilibidi wamwachie kwa dhamana ambayo ni haki yake ya msingi.

“Tulimwachia kwa dhamana, lakini jana (juzi) tulilazimika kumkamata tena kutokana na usalama wake kuwa mdogo baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake,” alisema.

Na Ramadhan Hassan  - Mtanzania
Share:

MSANII WA FILAMU AFARIKI DUNIA

Share:

BINTI ASIMULIA ALIVYOISHI MWANAE ALIVYOISHI KABATINI...


Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto kudai kwamba madai ya mtoto wa miezi mitano kufungiwa kabatini sio ya kweli, mama mzazi wa kichanga hicho amesimulia jinsi alivyotumia mbinu kuokoa maisha ya mwanaye kabatini.

Katika tukio hilo ambalo linafanana na lile la mwaka 2014 la Mariamu Said wa Morogoro kumficha mtoto wa marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne, mama wa mtoto huyo amedai kuwa alikuwa akitakiwa kufanya hivyo na mwajiri wake ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi jijini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi jana, mzazi huyo mwenye umri wa miaka 15 alisimulia jinsi alivyolazimika kuvunja sehemu ya nyuma ya kabati ili mwanaye aweze kupata hewa bila mwajiri wake kujua.

Binti huyo na mwanaye ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Dodoma alisema alivunja mbao katika kabati hilo ili mwanaye apate hewa, wakati mwingine alikuwa akitumia upenyo huo kumnyonyesha kwa siri anapokuwa mwenyewe nyumbani hasa mchana.

“Hakujua kama nilivunja mbao nyepesi nyuma ya kabati lake lakini angejua sijui ingekuwaje maana asingekubali kilichofanyika,” alisema.

Binti huyo alidai kuwa ameishi kwa mwajiri wake zaidi ya mwaka mmoja na nusu baada ya kumchukua kutoka Kijiji cha Kigwe, Bahi. 

“Ila tangu aliponichukua hakuwahi kunilipa mshahara, alikuwa akinipa chakula tu,” alidai. “Mwanzoni aliniambia atakuwa akinilipa Sh30,000 kwa mwezi lakini sijawahi kupewa hata mia. Nilipata ujauzito nikiwa kwake na aliyenipa ni (anamtaja jina), ila tangu nimejifungua huyu mama amekuwa akinipiga.


“Asiponipiga yeye basi nitapigwa na mtoto wake wa kiume. Huyu mtoto wangu sijawahi kumnyonyesha mchana. Alikuwa akimuweka kwenye kabati lake la nguo lakini ikifika saa nane usiku ndipo ananipa nimnyonyeshe halafu asubuhi anamchukua tena.”

Polisi wakana kabati

Wakati mzazi huyo akisema hayo, Kamanda Muroto alisema wanamshikilia mwalimu huyo lakini amekanusha kukifungia kichanga hicho kabatini.


Na Habel Chidawali na Rachel Chibwete mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger