Saturday, 16 February 2019

WILAYA YA MUFINDI YAANZA KUPIGA KURA KUWABAINI WABAKAJI NA WALAWITI

Na.Amiri kilagalila
Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeanza kupiga kura ya maoni ya siri katika vijiji vyote vya tarafa tano za wilaya hiyo ili kuwabaini waharifu wa matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo yanaonekana kukithiri katika wilaya hiyo na kuifanya wilaya hiyo kuwa ya kwanza kati ya wilaya tatu za mkoa huo kwa ukatili huo.


Kaimu katibu tawala wa wilaya ya mufindi Joseph Mchina amesema kuwa kura ya siri ya maoni imeanza tangu januri katika vijiji na mitaa na baadae litafanyika katika taasisi za elimu zikiwemo shule za sekondari , msingi na vyuo ili kuwabaini watu wanaohusika na matukio hayo.


Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mafinga mh Charles makoga amesema kuwa sababu za matukio ya kikatili ya ubakaji na ulawiti katika mkoa wa iringa zinachagizwa na imani za kishirikina mambo ambayo yanatokana na ukosefu wa elimu.


Badhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu wamesema utaratibu wa serikali kupiga kura ya maoni ya siri uende sambamba na uandaaji wa takwimu sahihi kwa kuwa bado kunataarifa zilizipo hazina uhalisia na matukio.
Share:

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA APOKEA GARI,AKEMEA POLISI KUSINDIKIZA BANGI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amekemea matumizi yasiyofaa ya magari ya Jeshi la Polisi ikiwamo kubeba au kutumika kusindikiza magari yaliyopakia bangi na mirungi.

Ametoa kauli hiyo jana Ijumaa Februari 15, 2019 jijini Arusha wakati akipokea gari la Polisi lililokarabatiwa na taasisi ya Fredkin Conservation Fund kwa gharama ya Sh15 milioni.

"Mkuu wa Polisi wa wilaya sitaki kusikia hii tabia ya magari yetu kuhusika kwenye vitendo viovu, akabidhiwe dereva aliyehitimu vyema na mwenye maadili," alisema Lugola.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameishukuru taasisi hiyo kwa kuchangia shughuli za ulinzi na kuwa tayari wamejitokeza wadau watakaokarabati magari yote mabovu ya polisi wilayani humo.
Share:

Friday, 15 February 2019

MWANAMKE AFARIKI KWA KUBAKWA NA KULAWITIWA MANYARA

Kundi la watu wasiofahamika wamembaka na kumlawiti hadi kufa mwanamke mmoja (35)  jina limehifadhiwa mkazi wa kijiji cha Kimana kata ya Pori kwa pori wilaya ya Kiteto mkoa wa Manyara kisha mwili kutelekezwa kichakani.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara , Agustino Senga , amesema tukio hilo limetokea Februari 12,2019 ambapo  mbinu waliyoitumikia watu hao ni kumpeleka marehemu kichakani na kumbaka na kumlawiti katika harakati za kumziba mdomo asipige kelele ilisababisha kukosa pumzi na kufariki dunia.  Ameongeza kuwa kiini cha tukio hilo ni tama za kimwili.  Kamanda  Senga amesema kutokana…

Source

Share:

WANANCHI WAPIGA KURA ZA SIRI KUBAINI WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WATOTO BUSEGA

Na Stella Kalinga, Simiyu Wananchi wa Kata ya Lamadi Wilayani Busega mkoani Simiyu wamepiga kura za siri kwa lengo la kubaini watuhumiwa wa mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni wilayani humo. Wakizungumza katika zoezi hilo lililofanyika Februari 14, 2019  katika Kitongoji cha Kisesa Kijiji cha Lamadi wananchi hao wamesema kuwa  wamelipokea vizuri zoezi hilo na kubainisha kuwa kura hizo zitasaidia Vyombo vya Dola katika kufanya uchunguzi na kuwabaini wauaji wa watoto wilayani humo. “Zoezi hili nimelipokea vizuri na nina imani litatusaidia kuwapata wauaji wa watoto wetu na naishukuru Serikali kuona…

Source

Share:

Airbus kusitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380

Shirika la Airbus limetangaza kwamba ifikapo mwaka 2021 litasitisha uzalishaji wa ndege zake aina ya A380 superjumbo kutokana na kukosekana kwa soko.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na shirika hilo ifikapo mwaka 2021 oda zilizokuwepo za ndege aina ya A380 zitakabidhiwa kwa wanunuzi na uzalishaji wa ndege hizo utasimamishwa.

Katika taarifa hiyo mkurugenzi mkuu wa Airbus Tom Enders alisema, wanatoa tangazo hilo huku wao na wanahisa wengine wa A380 wakiwa na uchungu.

Mteja mkuu wa ndege hizo aina A380 shirika la ndege la Emirates limepunguza kiasi cha manunuzi ya ndege hizo kutoka ndege 162 hadi 123 imefahamishwa katika taarifa hiyo.

Emirates imeingia mkataba mpya wa kununua ndege 70 aina ya A330-900s na a350-900s mbadala wa A380. Mkataba huo mpya una thamani ya dola bilioni 21.4.

Ndege hizo za Airbus A380 zenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 800 ziliazalishwa kutoa ushindani kwa ndege aina ya Boeing 747 za shirika la uzalishaji ndege la Marekani.


Share:

Serikali Yakabidhi Eneo La Mradi Wa Umeme Wa Maji Mto Rufiji Kwa Mkandarasi Tayari Kwa Kazi Kuanza

SERIKALI imekabidhi rasmi eneo la mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP),  kwa mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy  Electric zote kutoka nchini Misri.

Hatua hiyo sasa inaashiria kuanza kwa kazi ya ujenzi wa mradi huo wa umeme ambao utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye dridi ya Taifa na kuifanya Tanzania kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alikabidhi mradi huo jana katika eneo la Hifadhi Matambwe lililopo mpakani mwa mikoa ya Pwani na Morogoro, akisema faida nyingine ya mradi huo utakapokamilika bei ya umeme itashuka kwa kiwango kikubwa na utasaidia nchini kutekeleza rasilimali muhimu za Taifa.

Alisema mradi huo utajenga bwawa kubwa, lenye mita za ujazo bilioni 34 na kituo cha kufua umeme, kitakachokuwa na mashine tisa za kuzalisha umeme zenye uwezo wa megawati 2,115.

Aidha, alisema pindi mradi huo ukikamilika, utasaidia kushusha gharama za umeme kutokana na uzalishaji wa umeme huo wa kutumia maji kuwa nafuu, tofauti na nishati nyingine kama mafuta, gesi, upepo na jua.

Aliwataka wakandarasi hao, kukamilisha mradi huo kwa muda waliokubaliana, huku akiwapongeza wataalamu kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuchangia utekelezaji wa mradi huo kwa hatua za awali. 

Aliwataka wakandarasi watakaotekeleza ujenzi huo, kujenga kwa ufanisi mkubwa na kwa viwango vinavyotakiwa na muda uliopangwa na utakaondoa shaka kwa wale wasioutakia mema mradi huo.

Dk Kalemani alimpongeza Rais John Magufuli kwa jinsi ambavyo amechukua ujasiri wa kuamua kutekeleza ndoto za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye mwaka 1958 alikuwa na mpango wa kujenga bwawa hilo, lakini ikashindikana kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo za kifedha. 

Hivyo aliwataka wakandarasi wa kampuni hizo na timu ya wataalamu wa Tanesco, kutoondoka eneo la mradi baada ya kukabidhiwa eneo, kwa kuwa hadi sasa kila kitu kipo kuanzia nyumba za kuishi, umeme na maji. Aliwataka wajenge wakati wote wa mvua na jua.

“Hatutaki kugeuka nyuma kuanzia sasa, Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco ushiriki kikamilifu ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati uliopangwa,” alisema Dk Kalemani. 

Aliongeza, “Mimi na Naibu Waziri na hata Rais tutakuwa bega kwa bega usiku na mchana kuona mradi unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa viwango na ubora wa kimataifa wa mabwawa ya kufua umeme.”

Alisema kukamilika kwa mradi huo, kutaleta tija katika kujenga uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda. Alisema mahitaji ya umeme nchini kwa sasa ni makubwa kwani nchi inatekeleza Sera ya Uchumi wa Viwanda, hivyo huduma za umeme wa uhakika inahitajika zaidi. 

Dk Kalemani alisema ujenzi wa mradi huo, unajumuisha ujenzi wa bwawa kuu lenye uwezo wa kutunza maji takribani mita za ujazo bilioni 34, kituo cha kufua umeme kitakachokuwa na mashine tisa za kuzalisha umeme zenye uwezo wa megawati 235 kila moja, hivyo kufanya uwezo kuzalisha umeme wa mradi megawati 2,115.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka alisema mradi huo wa kihistoria, uliosainiwa kati ya Tanesco na Kampuni ya Ubia Arab Contractors (Osman A. Osman Co na Elsewedy Electric), utakuwa na mkataba wa miezi 42. 

Msimamizi Mkuu wa kampuni mbili zilizopewa kandarasi hiyo, Makamu wa Rais wa kampuni hizo kutoka Serikali ya Misri, Wael Handy alisema mradi huo si wa Watanzania pekee, bali ni faida kwa wananchi wa Afrika yote.

Alisema mradi huo umeshirikisha timu mbalimbali za wataalamu wa sekta mbalimbali na katika kutekeleza mradi huo, Serikali ya Misri haitawaangusha na itahakikisha unatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.


Share:

Hiki Ndicho Wanacho Kiwaza Wanaume Wengi Kuhusu Kuingia Katika Mahusiano /ndoa Na Single Mothers

Wewe  ni  Single  Mother ?  Upo  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  na  mwanaume ? Au  unataka  kuingia  katika  mahusiano ya  kimapenzi/uchumba/ndoa  na  mwanaume  ambae  si  baba  wa  mtoto  wako?

Basi  kabla  ya  kufanya  hivyo,unatakiwa  kujua  kitu  gani  wanacho  kiwaza  wanaume  wanao  ingia  katika  mahusiano  na  single  mothers.

Pia  unatakiwa  kuyafahamu  mambo  wanayo  yawaza wanaume  wengi  kabla  ya  kuingia katika  ndoa  na  single  mothers.

Mahusiano  mengi ya  single  mothers  yanashindwa kufika  mbali  kwa  sababu  single  mothers  wengi  huwa  wanaingia  katika  mahusiano  na  wanaume  bila  kuyafanyia   analysis  mambo  haya  muhimu  kabisa  kwa  kila  single  mother kuyafahamu.

AFRICANDADAZ ime kusanya maoni  kutoka  kwa  wanaume  mbalimbali kuhusu  uzoefu  wao  na  mtazamo  wao  kuhusu  kuingia  katika  mahusiano  ya kimapenzi  au ndoa  na  single  mothers.  

Maoni  haya  yamechukuliwa  kutoka  kwa  wanaume  mbalimbali  wa  hapa    Tanzania  na  waliopo  nje  ya  Tanzania.  Baadhi  ya  mambo  yanayo semwa  na  wanaume  hawa  kuhusu  kuingia  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  au  ndoa na  single  mothers  yanatisha  na  kuogopesha   sana. 

 Ni  vyema  kila  single  mother ambae  anafikiria  kuingia  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  au  kuingia  katika  ndoa  na  mwanaume  ambae  si  baba  wa  mtoto  wake  ayafahamu  mambo  haya.

Kusoma  zaidi  makala  haya tembelea Kwa kubofya hapo chini :



Share:

Mwigulu Nchemba Aruhusiwa Kutoka Hospitali

Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) Dk Mwigulu Nchemba aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Dk Mwiguli alipata ajali Februari 13, 2019 katika eneo la Migori mkoani Iringa akitokea mkoani humo kwenda mkoani Singida baada ya gari lake kugonga punda waliokuwa wanakatisha barabara.

Katika ajali hiyo Dk Mwigulu, aliumia maeneo ya kifua, nyonga na kwenye mguu lakini dereva wake ambaye ni mtu pekee aliyekuwa naye kwenye gari hilo hakuumia mahali popote.
 Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dk Alphonce Chandika amesema waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani ameruhusiwa hospitalini hapo baada ya afya yake kuimarika.

“Mheshimiwa Mwigulu anaendelea vizuri na sasa tumemruhusu kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika,” amesema Dk Chandika.

 Katika ukurasa wake wa Istagram, Mwigulu Nchemba ameandika ujumbe wa kumshukuru Mungu, Rais Magufuli na viongozi wengine na wananchi kwa maombi yao,


Share:

TANESCO WAPEWA SIKU TATU KUANDAA MKAKATI WA KUMALIZA TATIZO LA UMEME SONGWE

Shirika la Umeme nchini, TANESCO Mkoa wa Songwe limepewa siku tatu kuandaa mkakati utakaoelezea namna ya kumaliza matatizo ya umeme ikiwemo katizo la mara kwa mara la umeme na tatizo la kiwango kidogo cha umeme.  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus  Mwangela  ametoa agizo hilo mapema leo asubuhi alipofika ofisi za TANESCO Songwe kufuatia kukatika mara kwa mara kwa umeme na pia kila siku ya Jumamosi ambapo alimtaka Meneja wa shirika hilo kueleza mkakati wa kumaliza tatizo hilo.  “Nimekuja hapa kwakuwa naona sasa tunageuka makubaliano ya kukata…

Source

Share:

WILAYA YA MUFINDI IMEANZA KUPIGA KURA KUWABAINI WABAKAJI NA WALAWITI

Na.Amiri kilagalila Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imeanza kupiga kura ya maoni ya siri katika vijiji vyote vya tarafa tano za wilaya hiyo ili kuwabaini waharifu wa matukio ya ubakaji na ulawiti ambayo yanaonekana kukithiri katika wilaya hiyo na kuifanya wilaya hiyo kuwa ya kwanza kati ya wilaya tatu za mkoa huo kwa ukatili huo. Kaimu katibu tawala wa wilaya ya mufindi Joseph Mchina amesema kuwa kura ya siri ya maoni imeanza tangu januri katika vijiji na mitaa na baadae litafanyika katika taasisi za elimu zikiwemo shule za…

Source

Share:

KOCHA MKUU WA YANGA ZAHERA AFUNGUKA KABLA YA KUIVAA SIMBA KESHO


Kuelekea mchezo wa watani wa jadi kesho, kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameweka wazi kuwa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Simba, waliingia wakiwa na matatizo ikiwemo kutokuwa na maandalizi mazuri.

Zahera ameyasema hayo leo katika mkutano wake na wanahabari, ambapo amesema jambo hilo kwa sasa halipo kwani wapo vizuri na mchezo wa kesho utakuwa mzuri kushinda ule wa kwanza ambao muda mwingi walitumia kujilinda kuliko kushambulia.

''Watu waje uwanjani kwa wingi mchezo utakuwa mzuri sana maana tunaongoza ligi na tumejiandaa vizuri yale matatizo hayapo tena'', amesema Zahera.

Kwa upande mwingine Zahera amesema kitendo cha mpaka sasa timu yake kuongoza ligi kumeijengea hali ya kujiamini kwani mwanzo waliona wanaweza kumaliza hata nafasi ya 5 au 6 lakini sasa wapo kwenye nafasi nzuri.

Mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni ambapo Yanga iliyocheza mechi 23 mpaka sasa ikiwa inaongoza ligi na pointi 58 wakati Simba ambayo ipo nafasi ya 3 ina pointi 36 katika mechi 15.
Chanzo- EATV
Share:

Ujenzi Wa Reli Ya Kimataifa Dar Es Salaamhadi Morogoro Washika Kasi, Wafikia Asilimia 42

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa dhati kukamilisha mradi mkubwa wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo tayari kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 2 kimetolewa mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi eneo la Soga, umbali wa kilometa 53, na kujionea maendeleo makubwa ya ujenzi wa reli hiyo.

Ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wake na kumpongeza mkandarasi anaye jenga reli hiyo, Kampuni ya Yapi Merkezi, kwa kutekeleza ujenzi huo kwa viwango vya hali ya juu ambapo ameelezwa kuwa, treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro inatarajia kuanza safari zake Mwezi Novemba mwaka huu kama kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

"Ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake kubwa na kuamua kwa dhati kutekeleza mradi huu mkubwa na miradi mingine, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, ambayo kukamilika kwake kutachochea uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Kijaji

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, tutakuwa na viwanda kila mahali, tumeanza ujenzi wa mradi wa umeme wa megawat 2,115, viwanda vitazalisha bidhaa ambazo zitahitaji miundombinu ya usafirishaji, reli hii itatumika na tunatarajia ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa ni nchi yenye kipato cha kati"  aliongeza Dkt. Kijaji

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha  kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo umekamilika kwa asilimia 42.

"Mradi wetu unaenda vizuri na kwa wakati, zoezi la ujenzi na utandikaji reli tumeanza katika Jijini la Dar es Salaam umeanza na unaendelea vizuri ambapo ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 55 na utandikaji wa reli katika Jiji hili utafikia kilometa 10 mwishoni mwa mwezi Februari" alifafanua Mhandisi Masanja.

na nguvu kubwa imeelekezwa katika ujenzi wa tuta na madaraja, zezi ambalo limefikia asilimia 55 hivi sasa" alifafanua Mhandisi Masanja

Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Mwanza, na baadae kuunganisha mtandao wake na nchi jirani za Kongo, Uganda, Burundi na Rwanda, unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 7.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezungumza na wakazi wa eneo la Guluka Kwalala, Gongo la Mboto, waliokuwa wakiendelea na taratibu zao za kulipwa fidia ambapo amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaletea maendeleo.

Baadhi ya wakazi hao, pamoja na kuiomba Wizara ya Ardhi na Makazi iwasaidie kupata viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao baada ya kulipwa fidia kupisha ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa, wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia ustawi na maendeleo ya nchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.

Mwisho


Share:

KAULI YA MWIGULU NCHEMBA BAADA YA KURUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


Mbunge wa Jimbo la Iramba, Mwigulu Nchemba ameruhusiwa kutoka hospitali hii leo kufuatia ajali ya gari aliyoipata Jumatano, Februari 13,2019 mkoani Iringa.

Mbunge huyo alikuwa akisafiri kutoka Iringa kuelekea Dodoma, wakati gari lake lilipopata ajali hiyo katika eneo la Migori moani Iringa, ambapo alikimbizwa katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma.

Katika ukurasa wake wa Istagram, Mwigulu Nchemba ameandika ujumbe wa kumshukuru Mungu, Rais Magufuli na viongozi wengine na wananchi kwa maombi yao,

"Nashukuru Mungu nimeruhusiwa kutoka Hospitali, Shukran kwa mhe Rais na wasaidizi wake wote kwakuwa karibu nami,wabunge,viongozi wa Chama na Serikali, madaktari kwa matibabu ya haraka, wananchi wote kwa maombi yenu na salamu za kunitakia heri. Zaidi namshukuru Mungu kwa namna alivyonitetea mimi pamoja na dreva wangu, hakika kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa." 
(@mwigulunchemba) 
Share:

Korean Government Scholarship Program, Scholarship Benefit & Application procedures

Korean Government Scholarship Program
Purpose
To provide international students with opportunities to conduct advanced studies in undergraduate & graduate programs at higher educational institutions in the Republic of Korea in order to promote international exchanges in education and mutual friendship between countries.

Available Options in Universities
Undergraduate course: 4-year courses at designated universities
※ Transferring between universities is not allowed. (e.g. Starting studies at the junior year is not allowed.)
Graduate course: Master’s or Ph.D. courses at general graduate schools of Korean universities

Total Candidates to be Selected
170 persons (undergraduate course), 700 persons (graduate course)

Korea Language Training
Grantees are required to take Korean language training courses for 1 year at a language institution located on-campus of the domestic universities. (Those who have attained a Korean language fluency score higher than level 5 in TOPIK are exempt from this requirement.)

 

MORE DETAILS AVAILABLE HERE

APPLY FOR THIS SCHOLARSHIP

The post Korean Government Scholarship Program, Scholarship Benefit & Application procedures appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Korea Scholarships academic year 2019-2021: Qualifications and Procedure for the Scholarship Award

Korea Scholarships academic year 2019-2021: Qualifications and Procedure for the Scholarship Award

Qualifications
Both an applicant and his/her parents must be citizens of their country of origin.
※ Applicants should not hold Korean citizenship.- Applicants should have adequate health, both mentally and physically, to stay in a foreign country for a long time.
– Should be under 25 years of age at the date of entrance. (Undergraduate)
– Should be under 40 years of age at the date of entrance. (Graduate)
– Have finished or be scheduled to finish formal education of all elementary, middle, high school courses by the date of arrival. (Undergraduate)

– Possess a grade point average (G.P.A.) above 80% from the last educational institution attended.
– Hold a Bachelor’s degree or a Master’s degree by the date of arrival. (Graduate)
※ Applicants who have previously acheived in any undergraduate program, master’s program, or doctoral program in Korea cannot apply for this program.

However, a former or current KGSP scholar who hold the overall grade of 90% or above can reapply to this program once either through the embassy or university track.

Procedure for the Scholarship Award
NIIED invites the Korean Embassy in the invited country or a domestic university to recommend potential candidates.
Applicants should submit all documents related to their scholarship application to the Korean Embassy in their country of residence to or the domestic university concerned.
The Korean Embassy or the domestic university sends proper candidates to NIIED with the required documents.
NIIED evaluates potential candidates and notifies the Korean Embassy of the final selected KGSP grantees.

The post Korea Scholarships academic year 2019-2021: Qualifications and Procedure for the Scholarship Award appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MBUNGE ATISHIWA KUAWA KWA KUNYOFOLEWA NYETI ZAKE NA WASIOJULIKANA

Mbunge wa Kimilili nchini Kenya Didmus Barasa amemwandikia Spika wa Bunge Justin Muturi akitaka aongezewe walinzi kwa sababu anadai maisha yake yapo hatarini.

Akihutubia wanahabari Alhamisi katika majengo ya Bunge, jijini Nairobi Bw Barasa alisema amekuwa akipokea simu na jumbe za kutisha kutoka kwa watu wasiojulikana wakitaka kumuua.

 “Katika barua hizo wamekuwa wakiniambia kwamba… 'Tunataka kichwa chako kidogo na viungo vingine vya mwili wako, nyamaza na ukome kutangatanga’,” alisema. 

Mbunge huyo wa chama cha Jubilee alisema majuzi watu hao walijaribu kumteka nyara mwanawe wa kiume ambaye ni mwanafunzi katika Shule ya Msingi ya Consolata, Nairobi.

 “Nilipata simu kutoka kwa mwalimu wa mtoto wangu akiniambia mwanaume fulani alikuja shuleni humo akidai ametumwa kumchukua mwanangu amrejeshe nyumbani. 

Mwalimu aliposisitiza kunipigia simu kwanza, jamaa huyo akatoweka,” Barasa aliongeza kusema.

 Kulingana naye, watu fulani wamekuwa wakivizia boma lake huko Kimilili na karibuni walipatikana wakitaka kuliangusha ili kuingia katika boma hilo kwa nguvu. 

“Niliwahi kuripoti polisi kisa ambapo nilishambuliwa na watu wenye bunduki lakini nikaponea. Mtu mmoja alikamatwa na kesi hiyo bado inachunguzwana na maafisa wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI), Langata,” alisema. 

Akiandamana na Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Laikipia Bi Catherine Waruguru, Barasa alidai kuwa mwanasiasa mmoja, ambaye hakumtaja, amekuwa akimtishia maisha.

 Mbunge huyo alitoa wito kwa DCI katika eneo bunge la Kimilili na Nairobi kuharakisha uchunguzi kuhusu tisho kwa maisha yake.
Share:

KONDOM ZAADIMIKA MJI WA MAFINGA

Na.Amiri kilagalila Maambukizi ya virusi vya ukimwi mjini mafinga mkoani iringa yanahofiwa kuongezeka kwa kasi kutokana na kuadimika kwa bidhaa ya kujikinga na maabukizi. kondom za kike na za kiume zimeonekana kupungua mjini hapo huku zilizopo zikielezwa kupanda bei na kuuzwa kwa bei ya ghali kunzia shilingi elfu 1000 mpaka elfu 3000 hali inayopelekea badhi ya watumiaji kushindwa kumudu gharama na kuwa hatarini zaidi na kukumbwa na maambukizi ya VVU. “Utakuta ukienda duka hili hakuna kondom je mh.mwenyekiti tunawasaidiaje wanaouza hizi kondom kuzipata kwa uraisi na ongezeko ili zije kwa…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger