Monday, 4 February 2019

MWIZI APEWA ADHABU YA KULA BAKULI LA PILIPILI

 Baadhi ya wakazi Mombasa nchini Kenya sasa wameanza kuitumia pilipili kama kifaa cha kuadhibia watu wanaokutwa na makosa kwa mfano wizi.

Katika video ambayo sasa inasambaa kwa kasi mtandaoni na kufuatiliwa na watu mbalimbali, jamaa anayedaiwa kuiba jozi ya viatu alilazimishwa kula pilipili.

Haijafahamika ni viatu vya aina gani alivyoiba kabla ya kupewa adhabu hiyo.

 Waliomkamata katika tendo hilo walimlazimisha kukiri kuiba kabla ya kumpa pilipili hiyo kuila na kumtaka aseme hatowahi kurudia tena. 

 "Mimi ni mwizi na mimi huiba viatu, nilitumwa na Felix anayefanya kazi feri. Baadhi ya viatu ninavyoiba sisi huviuza feri na Changamwe," alisema mwizi huyo chini ya ulinzi mkali.

 Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa adhabu ya aiana hii kutumika na itakumbukwa katika kisa kingine cha wizi, jamaa alitakiwa kuchagua kati ya kupigwa kitutu na kula pilipili.

 La kushangaza ni kuwa, jamaa huyo alichagua kula bakuli la pilipili huku waliokuwa wamemkamata wakiangalia. 

BOFYA HAPA KUONA VIDEO YA JAMAA AKILA PILIPILI
This shoe thief will never steal again after being forced to eat pilipili 😂😂😂


1:38
15.8K views

Share:

SAKATA LA TRILLION 1.5 BADO PASUA KICHWA,WAPINZANI KUHAMISHIA MAJIMBONI

Wabunge wa kambi ya upinzani wamesema watalihamishia sakata la utata wa Sh.1.5 Trilioni majimboni kwao baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhitimisha kuwa fedha hizo hazikuibiwa au kupotea. Uamuzi huo wa wapinzani umetolewa na Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF). Bobali amesema kuwa ingawa kamati imehitimisha hivyo, wao wataendelea kuwasha moto akidai kuwa fedha hizo zilitumika bila idhini ya Bunge. “Pale tunapohoji ni nani aliyeruhusu fedha hizo zikatumika bila idhini ya Bunge, na ni fedha nyingi. Sasa mjadala ndio kwanza unaanza na ni lazima moto uwake…

Source

Share:

WAGANGA WA JADI WAKIMBIA NJOMBE

Na Amiri kilagalila Baadhi ya waganga wa jadi wasiokuwa na nia Njema wameanza kutoroka mkoani Njombe na kukimbilia mikoa ya jirani kutokana na msako mkali wa jeshi la polisi unaoendelea mkoani humo ili kuwabaini wanaojihusisha na ramli chonganishi zinazosababisha mauaji ya watoto. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa Njombe RENATHA MZINGA amesema kuwa jeshi la polisi halitaweza kuwaacha wale wote waliokuwa na nia ovu na kuwatafuta popote pale walipo. “Tunao waganga 6 tunaowashikilia mpaka sasa kwa mahojiano na tulivyoanza na kamata kamata wale ambao wana…

Source

Share:

Picha : TVMC YAFADHILI VIJANA KUSOMA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI,YAKABIDHI VIFAA MUHIMU

Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) linalotoa huduma za kijamii kwa upande wa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza limewafadhili vijana watano wa kike kuendelea na masomo katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga.

Vijana hao ambao wameshindwa kuendelea na masomo katika mfumo rasmi baada ya kuhitimu masomo ya darasa la saba mwaka 2018 wanatoka katika kata ya Chamaguha katika Manispaa ya Shinyanga.

Shirika la TVMC limewalipia ada na kuwapatia mahitaji yote muhimu yanayotakiwa chuoni vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3.4 lengo likiwa ni kupambana na mimba na ndoa za utotoni.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa vya wanafunzi hao kisha kuwakabidhi wahusika leo Jumatatu Februari 4,2019, Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Bi. Octavina Kiwone alisema TVMC imefanya jambo jema ili kuwasaidia vijana kujiendeleza kielimu hali itakayowafanya wajikwamue kimaisha.

“Tunawashukuru TVMC kwa kuwa wadau muhimu katika manispaa yetu,mmekuwa pamoja na watoto hawa tangu mwaka 2016 kwa kuwapatia huduma mbalimbali ikiwemo kuwapa sare za shule na kuwalipia bima za afya,tunaimani vijana watatumi fursa hii kusoma kwa bidii na kutokubali kurubuniwa”,alieleza Kiwone.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Ngangala ufadhili huo wa masomo kwa vijana wanaotoka katika mazingira magumu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuzuia mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa na TVMC kwa ufadhili wa shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani.

“Vijana hawa wameshindwa kuendelea na masomo katika mfumo rasmi,hivyo tumeona ni vyema kuwaendeleza kielimu kwani elimu hii itawasaidia kuendeleza maisha yao,na hawa watano tuliowapeleka chuoni watakuwa mfano kwa wengine na tunatarajia kuongeza wengine kadri tutakavyopata nafasi”,alisema Ngangala.

“Vijana hawa watapata mafunzo mbalimbali kwenye chuo cha FDC Buhangija kwa muda wa mwaka mmoja,tumewalipia ada shilingi 500,000/= kila mmoja na kuwapatia mahitaji yote muhimu chuoni kama vile magodoro,vyandarua,vyombo,shuka na vifaa vya kujifunzia”,alieleza.

Aidha aliishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana na shirika hilo katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wao,vijana hao walilishukuru shirika hilo kuwa kuwashika mkono na kuahidi kuzingatia masomo yao chuoni.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Bi. Octavina Kiwone akizungumza wakati Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) likikabidhi vifaa kwa vijana watano ambao wamefadhiliwa na shirika hilo kujiunga na masomo katika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Bi. Octavina Kiwone akiwasisitiza vijana kuzingatia masomo yao huku akiwataka wazazi na walezi kutowatenga watoto wao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC), Mussa Ngangala akizungumza wakati akikabidhi magodoro na vifaa mbalimbali kwa vijana watano ambao wanajiunga katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC), Mussa Ngangala (kulia) akimuonesha vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto/vijana watano wanaojiunga katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Bi. Octavina Kiwone.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC), Mussa Ngangala akionesha kifaa cha kujifunzia katika chuo cha FDC
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Bi. Octavina Kiwone akipokea godoro kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC), Mussa Ngangala kwa ajili ya vijana wanaofadhiliwa na shirika hilo.
Vijana wakibeba vifaa vyao na kuviweka kwenye gari kwa ajili ya safari kuelekea katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

PAPA AANZA ZIARA RASMI FALME ZA KIARABU

Ziara hiyo ya kiongozi wa kanisa Katoliki duniani ni ya kwanza kuwahi kufanywa na kiongozi wa kanisa hilo kwenye rasi ya Uarabuni.

 Lengo ni kufungua ukurasa mpya katika uhusiano baina ya wakristo na Waislamu.

Mrithi wa mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan alimpokea Papa Francis kwenye uwanja wa ndege akiwa na tabasamu huku akiongozana na mawaziri wake. 

Imam mkuu wa msikiti maarufu wa Al-Azhar wa nchini Misri, Ahmed el Tayeba pia alikuwapo uwanja wa ndege kumlaki Baba Mtakatifu.

 Leo hii Papa Francis na imam el Tayeb watahutubia kwenye mkutano utakaohudhuriwa na wawakilishi wa dini zote. 

Hapo kesho Papa Francis ataongoza misa itakayokuwa ya kwanza kuongozwa na baba mtakatifu kwenye rasi ya Uarabuni. Waumini wapatao 135,000 wanatarajiwa kuhudhuria misa hiyo ya hadharani.

Chanzo:Dw
Share:

AMUUA MKEWE KISHA NAYE KUJIUA KISA UGOMVI WAKE NA MAMA MKWE


 Wakazi wa kijiji cha Ober, Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya wameshangazwa na tukio la mwanaume aitwaye Paul Ochieng', (21) kujiua mara baada ya kumpiga mpenzi wake Beryl Atieno na kumtoa uhai.

 Inadaiwa Paul Ochieng' aligombana na mpenzi wake Beryl Atieno, 18, Ijumaa, Februari 1,2019 kabla ya kujitoa uhai.

Kwa mujibu wa majirani walioshuhudia tukio hilo, ndoa ya Ochieng na binti huyo ilipingwa sana na mama mkwe aliyetaka binti yake kurejea katika boma lao ili kuendelea na masomo, Citizen Digital iliripoti Jumapili, Februari 3,2019.

 Akithibitisha kisa hicho, Chifu wa eneo hilo Chief Mark Ongoro alisema marehemu hao walikuwa katika uhusiano uliokuwa umedumu karibia miezi kumi. 

 Ongoro alisema Atieno alikuwa amerejea katika nyumba yao kuchukua virago vyake wakati Ochieng' alipopandwa na hasira na kufanya unyama huo. 

Baada ya kugundua mchumba wake alikuwa amerejea nyumbani, majirani wanasema Ochieng' alikwenda sokoni na kununua sumu na kamba na kurejea nyumbani na kuanza kumpiga mke wake hadi kumuua. 

 Ochieng' alikunywa sumu na kujitia kitanzi shingoni kabla ya majirani kuingilia kati na kumpeleka hospitalini alikokata roho akipokea matibabu.

 Miili ya wawili hao ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Homa Bay huku polisi wakianzisha uchunguzi wao kuhusu kisa hicho. 

Via Tuko
Share:

HARMONIZE AMJIBU MAKONDA "NILIYEJIPOST NA MIMOSHI YA SIGARA NA HAWA WACHEZAJI WA SIMBA NANI WAKUSOKOMEZWA NDANI TUKITUA BONGO?

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amejibu tuhuma iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwamba huwenda akawa anatumia bangi baada ya kuonekana akivuta sigara yenye moshi mzito katika moja ya video ambayo aliiweka mitandaoni.

Mkuu huyo aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wasanii katika mkutano wa kusikiliza changamoto za wasanii na kuzitatua ambapo alizungumzia suala la nidhamu kwa wasanii hao.

Baada ya kauli hiyo, Harmonize ambaye yupo nchini Afrika Kusini amejibu tuhuma hizo kwa njia ya matani huku akilihusisha na suala la Simba kufungwa goli 5 na Al Alhy ya Misri.

Harmonize alipost video ambayo inamuonyesha mtu akilia na kuandika;“Wakati mwingine tuacheni utani tuweni serious …!!! hivi mie niliejipost na mimoshi ya Sigara tena Sigara Embasy Hiyo Bange yenyewe naisikia kwenye Bomba…!!! na hawa wachezaji wa@simbasctanzania Nani wakusokomezwa ndani tukitua Bongo…???? 🤣🤣🤣 hebu angalieni wanavotesa watu wasiokuwa na hatia 😭 
 
Minazani tungeanza na @hajismanara Kwanza akamatwe achunguzwe….!!! 🤣🤣🤣🙏🙏"

Share:

ASKOFU MAJEBERE : WAHUSIKA MAUAJI YA WATOTO NI WANASIASA WATEJA WAKUBWA WA WAGANGA WA JADI

Moja ya mwili wa mtoto ambaye alikuwa ameuawa mkoani Njombe mapema wiki iliyopita
**
Wakati watoto saba wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wakiripotiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani Njombe, Askofu wa Kanisa la Ufunuo Tanzania Mkoa wa Geita, Heryyabwana Majebere, amesema mauaji hayo yamezuka hivi sasa ikiwa ni kuelekea kwenye mdogo wa serikali za mitaa.

Kwa mujibu wa Askofu Heryyabwana Majebere, huenda wahusika wakubwa wa mauaji ya watoto ni viongozi wa serikali na vyama vya siasa ambao ndiyo wateja wakubwa wa waganga wa jadi.

Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalumu ya kuwaombea watoto hao wasio na hatia, Askofu Majebere amesema amepokea kwa masikitiko mauaji ya watoto yanayoendelea Mkoani Njombe huku akibainisha kuwa watoto wana haki ya msingi ya kulindwa.

kuhusu mauaji hayo kuhusishwa na imani za kishirikina, Askofu Majebere amesema serikali inapaswa kuchukua hatua kali kwa waganga watakaobainika kujihusisha na ramli.
Share:

AMUUA MKEWE KWA KUMNYONGA AKIMTUHUMU KUCHEPUKA NA WANAUME WANAOMPA POMBE KAHAMA


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Maselle Mheziwa (40) mkazi wa Kagongwa wilayani Kahama ameuawa kwa kunyongwa shingo na mmewe aitwaye Omary Juma (46),mkazi wa Kagongwa kutokana na ugomvi wa wivu wa kimapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao,tukio hilo limetokea Februari 2,2019 majira ya saa mbili asubuhi katika kata Kagongwa, tarafa ya Isaghehe, wilaya ya Kahama.

 "Chanzo ni ugomvi uliokuwepo kati ya marehemu na mumewe akimtuhumu mkewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine kwa sababu ananunuliwa pombe na wanaume bila kibali kutoka kwa mmewe",amesema Kamanda Abwao.

"Mbinu iliyotumika ni kumnyonga shingo na kumweka njiani ili asijulikane. Mtuhumiwa amekamatwa kwa hatua zaidi za kisheria",ameongeza.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.


Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install


https://bit.ly/2Qb7qyF



NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Usikubali Kupitwa na Habari Moto Moto : Pakua App ya Malunde1 blog Tukupe Uhondo Wote..Bonyeza Hapa

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.



Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Share:

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE AJIUA DAR

Mtoto wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Msewe jijini Dar es Salaam, Daniel Mussa (10), anadaiwa kukutwa amejinyonga chumbani kwake nyumbani kwao Kimara Kona jijini.

Tukio hilo lililotokea Januari 30,2019 limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro, aliyedai uchunguzi wake bado unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

"Kuna mambo matatu hapo; kajinyonga, kafa au kauawa? Sisi bado tunachunguza ili kujua ukweli," Kamanda Muliro alisema.

Alisema hakuna mtu wanayemshikilia kutokana na tukio hilo, lakini wanafanya uchunguzi kwa watu wa karibu na mtoto huyo wakiwamo wazazi na ndugu zake.

"Sisi (Jeshi la Polisi) tunapochunguza, ninyi (waandishi wa habari) husema tunawashikilia, tunahoji watu wa karibu baba, baba mdogo na wengine ili kupata ukweli wa tukio," alisema.

Chanzo- Nipashe
Share:

Video : NANDY - HAZIPO

Hii hapa video ya wimbo wa Nandy- Hazipo

Advertisement
Share:

WAZIRI WA ELIMU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI SITA WA CHUO CHA PATANDI

Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi watumishi sita wa chuo cha elimu maalum Patandi mkoani Arusha kwa tuhuma za kushindwa kusimamia majukumu yao na pia matumizi mabaya ya zaidi ya bilioni 2.3 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho.

Waziri Ndalichako amechukua hatua hiyo baada ya kutembelea chuo hicho kukagua mradi wa majengo ya chuo hicho ambao licha taarifa kuonyesha kuwa umechelewa kukamilika bila sababu za msingi pia thamani ya fedha zinazotajwa inapingana na hali halisi na pia ubora wake,na amemuagiza Katibu mkuu kupeleka watendaji wengine wakati uchunguzi ukiendelea na ikithibitika sherika itachukua mkondo wake.

Watumishi waliosimamishwa ni mhasibu mkuu, Rose Kijaka; makamu mkuu wa chuo, Isack Myovela; mwenyekiti wa kamati ya mapokezi, Peter Mosha; boharia wa chuo, Charles Njarabi; na Henry Matei aliyehamishiwa Chuo cha Ualimu Monduli ambaye ameagiza arudishwe kujibu tuhuma zinazowakabili.

Kuhusu mkuu wa chuo hicho, Janes Liana amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, kumuondolea madaraka na kuendelea na utumishi kutokana na maradhi yanayomsumbua kwa muda mrefu.
Share:

TUNDU LISSU AMJIBU BALOZI WA TANZANIA UJERUMANI

Siku chache baada ya Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi kutoa taarifa ya kumjibu Tundu Lissu kutokana na madai aliyoyatoa alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Deutsche Welle nchini humo, mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema) ameibuka na kumkosoa balozi huyo.

Katika maelezo yake, Dk Possi alimtaka Lissu kurudi Tanzania ili kutoa ushirikiano wa uchunguzi unaofanywa na Polisi.

Hata hivyo, Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mchana wa Septemba 7, 2017 jijini Dodoma amesema uchunguzi huo hauhitaji yeye wala dereva wake kuwapo.

“Sheria ya kusaidiana katika masuala ya jinai iliyotungwa na Bunge la Tanzania, imeweka utaratibu wa namna ya kupata ushahidi au mtuhumiwa aliyeko nje ya Tanzania,” amesema Lissu kupitia ujumbe aliotutuma Mwananchi.

“Kwa mujibu wa sheria hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Tanzania anatakiwa kuomba msaada wa nchi aliko shahidi au mtuhumiwa huyo ili kupatikana ushahidi au mtuhumiwa anayehitajika kwa uchunguzi wa kijinai,” ameongeza. 

Lissu amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania hajawahi kuomba msaada wa Serikali ya Kenya, kwa kipindi chote cha miezi minne alichokuwa Hospitali ya Nairobi wala kwa Serikali ya Ubelgiji tangu alipokwenda Januari 6, 2018 kwa matibabu zaidi.

“Kauli hii, ambayo imerudiwa rudiwa sana na Serikali, ina maana kwamba kama mimi na dereva wangu tungeuawa siku ya shambulio hilo, basi kusingekuwa na uchunguzi wowote?” alihoji.

Amesema yeye na dereva wake siyo mashahidi pekee wa tukio hilo, bali kuna ushahidi na mashahidi wengine ambao wangeweza kuhojiwa na wapelelezi lakini hawajahojiwa na wala taarifa yoyote ya uchunguzi kutolewa.

“Jeshi la Polisi halijawahoji majirani zangu nyumbani kwa Waziri wa Nishati Medard Kalemani, Mbunge wa Ulanga Magharibi, Haji Mponda na Katibu Mkuu. Hawa nilikuwa naishi nao kwenye jengo moja.

“Jeshi la Polisi halijawahi kueleza nani aliyeondoa CCTV iliyokuwapo kwenye jengo la makazi yangu baada ya shambulio; kwa nini iliondolewa; mahali ilikopelekwa, na ni kitu gani kinaonyeshwa kwenye CCTV hiyo,” amesema Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Lissu amesema: “Jeshi la Polisi halijawahi kueleza hata aina ya silaha au risasi zilizotumika kunishambulia, taarifa ambazo hazihitaji uwapo wangu, bali uchunguzi wa kitaalamu wa silaha.”

Katika maelezo yake, Lissu amesema: “Kwa hiyo, katika mazingira haya, kauli ya Balozi Possi kwamba uchunguzi wa shambulio dhidi yangu unasubiri mimi na dereva wangu turudi Tanzania, ni kauli ya kukwepa kuwajibika kwa vyombo vya upelelezi vya Serikali ya Tanzania.”
Chanzo- Mwananchi
Share:

SERIKALI KUFUMUA SHERIA YA UVUVI

Na.Amiri kilagalila Serikali imeamua kuifumua Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 ili kuondoa vikwazo vya kibiashara na uwekezaji katika sekta ya uvuvi. Pia kwenda na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya awamu ya tano inayolenga kujenga Tanzania ya viwanda, kuwatetea na kuwalinda wanyonge. Akizungumza katika uzinduzi wa ukusanyaji maoni ya wadau kuhusu rasimu ya Sheria ya Uvuvi na Sheria ya Ukuzaji viumbe kwenye maji jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, alitaja sababu nyingine zilizosababisha kuwapo mabadiliko hayo.…

Source

Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 4,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 4, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Sunday, 3 February 2019

CCM TABATA YAOMBA WANACHAMA WASICHAFUANE

Na Heri Shaban Chama cha Mapinduzi CCM Mtaa wa Kimanga darajani imewataka wana CCM wasichafune katika kipindi hiki cha kuelekea chaguzi za Serikali za Mitaa badala yake wanachama wa chama hicho wametakiwa wajenge chama na Jumuiya zake. Hayo yalisemwa na Katibu Mwenezi wa CCM Kimanga Deogratius Mkude wakati wa hafla ya mkutano mkuu wa CCM Kimanga darajani. Mkude alisema wakati CCM ikielekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa sasa sio mda wa kuchafuana ni mda wa kujenga chama pamoja na jumuiya za Vijana, Wazazi na jumuiya ya Wanawake UWT…

Source

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger