Wednesday, 15 April 2026

NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AWASILI BRAZIL KUKUZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

...

Naibu waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt Ngwaru Maghembe (Mb.) amewasili nchini Brazil kwa ziara ya kikazi.

Mhe. Naibu Waziri Dkt. Maghembe amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dr. John Stephen simbachawene katika Ofisi ya Ubalozi.

Mhe Naibu waziri alipata nafasi ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali na Watumishi wa Ubalozi na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa kuvutia uwekezaji kutoka Brazili.

Katika ziara hiyo Mhe.Dkt Ngwaru Maghembe (Mb.) ataongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Mashauriano ya kisiasa kati ya Tanzania na Brazil.

Mkutano huo unalenga kukuza uhusiano wa Kidiplomasia na Ushirikiano baina ya Tanzania na Brazili katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, Uwekezaji, Kilimo, Mifugo na Utalii
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger