Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kuorodhesha shule kumi za sekondari zilizofanya vizuri zaidi. Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde ameeleza kuwa shule binafsi ndizo zilizoongoza kwa kufanya vizuri zaidi katika matokeo hayo. Amezitaja shule kumi zilizopata ufaulu wa juu zaidi Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys (Pwani), Marian Girls (Pwani), Ahmes (Pwani), Canossa (Dar es Salaam), Bright Future Girls (Dar es Salaam), Maua Seminary (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa). Aidha, Dkt. Msonde amemtaja Hope Mwaibanje…
Thursday, 24 January 2019
HIZI HAPA SHULE 10 BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018,MWANAFUNZI BORA...TUMAINI LUTHERAN IMEFUTIWA MATOKEO
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.
Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma katibu mkuu wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).
Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi.
Wakati huo huo (Necta) imefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.
Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.
Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.
Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.
MWAKITINYA AWANYOOSHEA KIDOLE WAPINZANI AMFAGILIA JPM
NA DANSON KAIJAGE, DODOMA MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) Mussa Mwakitinya maarufu kwa jina la Mwana wa Mungu amewashambulia wabunge wa upinzani na kueleza kuwa wana nia mbaya na amani ya taifa. Mwakitinya ambaye kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani na kuzungumza na vyombo vya habari amesema kuwa wanasiasa hao ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. Mnec huyo alisema kuwa wanasiasa hao wamekuwa wakifanya siasa za kulitia doa taifa kwa…
MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU KUHUSU OLIVER MUTUKUDZI
Kama umeshawahi kuiona filamu ya Neria, basi bila shaka utakuwa unaujua wimbo wa Neria ambao umeimbwa kwa sauti nzuri nzito, ambayo hautachoka kusikia masikioni mwako, huku vinanda vyake vikiusuuza moyo wako na utamu wake masikioni mwako.
Oliver Mutukudzi aliimba wimbo huo akiwa na lengo la kumliwaza dada yake Neria aliyefiwa na mumewe na kukumbana na manyanyaso ya wakwe zake.
Mutukudzi alizaliwa September 22, 1952 nchini Zimbabwe katika eneo la Highfield, ambako ni Uswahilini haswa ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo Harare.
Kutokana na sauti yake nzuri na ya kuvutia anapoimba aliyojaliwa na Mungu. Oliver aliingia kwenye muziki na kuwavutia wengi tangu miaka ya 77, umauti umemfika akiwa na albam 59 alizozifanya, na kujiwekea heshima kubwa duniani.
Haya ni mambo muhimu ambayo unapaswa kuyajua kuhusu Oliver Mutukudzi.
1. Ni baba wa watoto watano, watoto wake wawili ni wanamuziki wakubwa nchini Zimbabwe, lakini kwa bahati mbaya mmoja, Sma Mutukudzi alifariki dunia mwaka 2014 kwa ajali ya gari.
2. Ana albam 59 mpaka anakutwa na umauti Januri 23, 2019.
3. Ameshajizolea tuzo zaidi ya 20 za kitaifa na Kimataifa
4. ameshawahi kuwa katika ukurasa wa mbele wa Gazeti kubwa la Marekani la Time, na kuwa msanii pekee kutoka Zimbabwe kufanya hivyo.
5. Alikuwa muigizaji wa filamu, ikiwemo filamu ya Neria ambayo ilizidi kumpa umaarufu Afrika na duniani.
6. Mwaka 2011, jarida la Forbes lilimtaja kuwa miongoni mwa watu maarufu 40 wa Afrika wenye nguvu, akiwemo muandishi wa vitabu Chinua Achebe na msanii wa muziki Akon.
7. Mutukudzi amefariki tarehe moja na rafiki yake kipenzi, msanii wa muziki wa Afrika Kusini, Hugh Masekela, ambaye alifariki Januari 23, 2018.
8. Ameshawahi kufanya kazi na msanii wetu wa hapa nyumbani Lady Jaydee, na hata kumleta kuja kufanya naye show katika moja ya kumbi Jijini Dar es salaam.
9. Ameshawahi kupewa degree ya heshima kutokana na kuwa philanthropist
10. Amefanya kazi na bendi kubwa nchini Afrika Kusini ambayo inahusisha wanaume watupu, ya Ladysmith Black Mambazo, ambao kwa pamoja waliurudia wimbo wa Neria na kutoa nyinginezo
Kifo cha Oliver Mutukudzi kimeacha pengo kubwa katika nchi ya Zimbabwe, kwani Mutukudzi hakujulikana kama msanii tu, bali alikuwa na heshima kubwa aliopewa wana Zimbabwe, kutokana na matendo yake na roho yake ya upendo ya kusaidia watu.
Taharuki : MLINZI AJIUA KWA SHUKA KWENYE CHUMBA CHA SINDANO..WAGONJWA WATIMUA MBIO
Mlinzi wa zahanati ya kijiji cha Katani kata ya Nkandasi wilayani Nkasi mkoani Rukwa Laudifasi Sokoni (60) amejinyonga katika chumba cha kuchomea sindano wagonjwa cha zahanati hiyo kwa kutumia shuka lake.
Tukio hilo lilibainika asubuhi ya Januari 23,2019 muda mfupi baada ya wahudumu kufika kazini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kutoa huduma.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa kijiji hicho,Jofrey kisato alisema baada ya wahudumu wa zahanati hiyo kufika kazini na kuanza kuandaa mazingira ya kutoa huduma ndipo walipogundua tukio hilo hali iliyosababisha watoe taarifa kwenye uongozi wa kijiji nao ukatoa taarifa kituo cha polisi.
Alisema marehemu alikuwa ni mlinzi wa zahanati ya kijiji na kuwa alikuwa akiishi peke yake kwa muda mrefu kutokana na mkewe kufariki dunia na mpaka sasa hawajui chanzo cha yeye kuamua kujinyonga.
"Inaonekana alidhamiria kujinyonga kwani alikwenda eneo lake la lindo na shuka, ambalo alitumia kujinyonga, na usiku wa kuamkia siku hiyo aliamua kujitundika kwa kutumia shuka hilo na wahudumu wa zahanati hiyo waligundua mwili wake ukining'inia wakati wakiandaa mazingira ya kutoa huduma hali iliyosababisha baadhi ya wagonjwa kuingiwa hofu na kutimua mbio bila kupata huduma" ,alisema mwenyekiti wa kijiji hicho.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote.
Alisema baada ya polisi kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa chanzo cha marehemu kufikia maamuzi hayo ni kutokana na kukabiliwa na maisha magumu pamoja na upweke.
Kamanda Kyando alisema tangu mke wa marehemu kufariki dunia mlinzi huyo alibaki akionekana kuwa na msongo wa mawazo pamoja na hali ngumu ya maisha inayomkabili ndiyo sababu zilizopelekea kujinyonga.
Alisema pamoja na kuwepo kwa sababu hizo za awali lakini polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo hasa cha Sokoni kufikia maamuzi ya kujinyonga.
Na Walter Mguluchuma - Malunde1 blog
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
Picha : AGAPE, EfG, MIIKO WAUNGANA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWENYE MASOKO MBEYA NA SHINYANGA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola wakionesha mkataba wa ushirikiano wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko ya Mikoa ya Shinyanga na Mbeya baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya EfG, Penina Leveta (kulia), akiwa na viongozi wa mashirika yaliyofanya mkataba wa ushirikiano. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga.
Mtathmini Miradi wa EfG, Samora Julius, akitoa mada katika semina ya maofisa wa mashirika hayo iliyofanyika hivi karibuni.
Maofisa wa mashirika hayo wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mwezeshaji katika semina hiyo, Pentaleon Shoki akitoa mada.
Usikivu katika semina hiyo.
Mwonekano wa chumba wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika moja ya kumbi zilizopo Baraza ka Maaskofu Kurasini jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina hiyo na kusaini mkataba wa ushirikiano.
Na Dotto Mwaibale
***
Mashirika matatu yasiyo ya kiserikali yametiliana saini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kupinga ukati wa kijinsia kwenye masoko`katika mikoa ya Mbeya na Shinyanga.
Mkataba huo ulihusisha shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, Shirika la Miiko la mkoani Mbeya na Shirika la Equality for Growth (EfG) la jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufunga semina ya siku tatu iliyowashirikisha maofisa kutoka katika mashirika hayo jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita alisema wameona waungane ili kuongeza nguvu ya kampeni ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika masoko ndani ya mikoa hiyo.
"Sisi shirika letu kwa hapa Dar es Salaam tulianza na mradi wa mpe riziki si matusi ambao ulilenga kuwalinda wanawake wafanyabiashara sokoni dhidi ya ukatili. Katika kupunguza ukatili dhidi ya wanawake katika masoko mradi huo umeweza kubadilisha mtazamo na tabia dhidi ya ukatili kwa wamawake, kuwahakikishia waathirika wa ukatili wanapata hakizao", alisema Magigita.
Alisema utafiti uliofanywa na EfG mwaka 2015 katika masoko 6 kuhusu ukatili wa kijinsia na uelewa wa sheria katika Wilaya za Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ulionesha kuwepo na ukatili dhidi ya Wanawake katika masoko ambapo asilimia 95.97 ya waliohojiwa katika masoko yote walisema kulikuwa na ukatili dhidi ya wanawake kwenye masoko yao.
Alisema zaidi ya wafanyabiashara 6500 waliweza kufikiwa na kampeni za kupinga ukatili, kampeni za kuongeza uelewa juu ya ukatili dhidi ya wanawake, sheria na haki za binadamu.
Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola alisema sasa wanakwenda kufanya kampeni kubwa ya kupinga ukaliti wa kijinsia katika Soko Kuu, Nguzonane, Kambarage, Ngokolo, Ndembezi na Majengo Mapya.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga alisema kampeni hiyo wataifanya katika masoko yote ya jijini humo.
TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JAN 24, 2019
Kiungo Mhispania Denis Suarez, 25, atasalia klabuni Barcelona baada ya mipango ya kuhamia Arsenal mwezi huu kushindikana. (ESPN)
Liverpool inaminyana na Bayern Munich katika mbio za usajili wa winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18. (Bild - in German)
Winga wa Chelsea na Nigeria Victor Moses, 28, anatarajiwa kwenda kwa mkopo klabu ya Fenerbahce mwishoni mwa msimu. (Goal)
Paris St-Germain wanatarajiwa kuwapiku Chelsea katika usajili wa kiungo wa Zenit St Petersburg raia wa Argentina Leandro Paredes, 24. (Telegraph)Victor Moses
Mipango ya Arsenal ya kumuuza kiungo wao Aaron Ramsey, 28, kwenda Juventus inaonekana kuungwa mkono na kocha wa timu yake ya taifa ya Wales,Ryan Giggs, ambaye amedai kuwa mchezaji huyo atazidi kuboreka kwa kucheza kwenye timu kubwa kama Juventus. (Sky Sports)
Watford wana imani kuwa Kiungo wao Abdoulaye Doucoure, 26, atasalia klabuni hapo walau mpaka mwisho wa msimu huu, japo kumeshatangazwa dau la pauni milioni 50 na Paris St-Germain ambao wanataka kumsajili. (Evening Standard)Marcelo na Ronaldo
Beki wa Real Madrid defender Marcelo, 30, anataka kuungana na Cristiano Ronaldo katika klabu ya Juventus, na tayari ameshamweleza kocha wake juu ya dhamira yake hiyo: "Kama (Juventus) wateleta ofa ya kuninunua, itabidi tu mniruhusu niende". (Marca via Tuttosport)
Newcastle wanajiandaa kusajili wachezaji wawili kwa mkopo kabla ya wiki hii kuisha. Tayari wameshawasilisha ofa kwa beki raia wa Italia anayechezea Monaco Antonio Barreca, 23, na winga wa Ureno anayekipiga na klabu ya Atletico Madrid Gelson Martins, 23. (Telegraph)
ALIYEKATWA MIGUU BAADA YA KUFANYIA TOHARA NA NGARIBA APATA MATUMAINI
Matumaini mapya ya mtoto Chistopher Masaka (11) ambaye alikatwa miguu yote mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufanyiwa tohara mwaka 2017 yameanza kurejea.
Christopher, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Mtitaa, alikatwa miguu yote kutokana na ushauri wa madaktari wa hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Akizungumzia mkasa huo baba mzazi wa mtoto huyo, Elias Masaka wa Kijiji cha Mtitaa, Bahi alisema Christopher alizaliwa akiwa mzima kabisa.
Mara baada ya kutahiriwa na ngariba, kijana huyo alianza kuugua miguu akisema alikuwa akihisi kama kuwa vitu vilivyokuwa vikitembelea kwenye nyayo zake.
Baba huyo alisema kadri muda ulivyosonga, tatizo hilo liliendelea na kufikia hatua ya kuanza kutoa majimaji.
Alisema hata aliporejeshwa kutoka jandoni haikuwezekana tena kupelekwa shule kwani wakati huo alikuwa hawezi kutembea umbali mrefu.
Mzazi huyo alisema hakuwahi kukutana na tatizo kama hilo katika ukoo wao wala katika kijiji chao lakini akasema wanajiuliza ni kwa nini chanzo cha tatizo hilo kianzie wakati wa tohara.
Na Habel Chidawali, Mwananchi
MKAZI WA ARUSHA AKABIDHIWA GARI ALILOSHINDA KATIKA PROMOSHENI YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA'
Mshindi wa gari la tatu kupitia promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane Baa, George Isaya mkazi wa Arusha, akifurahi baada ya kukabidhiwa gari lake. Kushoto ni Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, Meneja Masoko na Biashara wa TBL Edith Bebwa (kulia) na Afisa Mawasiliano wa TBL Amanda Walter.
Meneja ukuzaji Masoko wa TBL na ABInBev Afrika Mashariki Edith Bebwa (katikati) akimkabidhi ufunguo wa gari mkazi wa Arusha, George Issaya mshindi wa gari la promosheni iliyomalizika ya TBL Kumenoga Tukutane Baa.
**
Mkazi wa Arusha, George Isaya (29) ambaye wiki iliyopita aliibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID, katika droo ya promosheni ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’leo amekabidhiwa gari katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, alisema gari hilo ndio la mwisho katika promosheni hii iliyodumu kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo pia imewezesha wateja wengine Julitha Kilawe wa Dar es Salaam na Frank Nathan wa Iringa kujishindia magari.
“Kwa niaba ya kampuni ya TBL, nawapongeza wateja wetu wote ambao wameshiriki katika promosheni hii na wale ambao wamefanikiwa kujishindia zawadi kubwa za magari na zawadi nyinginezo ambazo zilikuwa zinatolewa kupitia kununua bia za chapa za bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.”
Akiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa gari lake, George Isaya alisema siku zote tangu apigiwe simu na kupewa habari za kushinda gari alikuwa haamini kama kama ni za kweli, leo baada ya kukabidhiwa gari lake ndio ameamini.
“Ninayo furaha kubwa kuona ndoto yangu ya muda mrefu ya kumiliki gari imetimia kupitia kunywa bia aina ya Kilimanjaro, gari hili litanisaidia kunirahisishia usafiri katika kutekeleza majukumu yangu mbalimbali, nashukuru kampuni ya TBL kwa kubuni promosheni zenye kuleta manufaa kwa wateja wake” alisema George Isaya.
Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, aliwashukuru wateja wote wa TBL kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.
WATU WATANO WAFARIKI, WAWILI KWA JIKO,WENGINE RISASI NA KUCHINJWA KAGERA
Watu watano mkoani Kagera wamefariki dunia katika matukio tofauti wakiwamo wanandoa wawili huku mwingine akiuawa kwa kuchinjwa shingo na sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kuchomwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi alisema jana kuwa wanandoa Mkundwa Selestine (51) na mkewe Letisia Katawa (48) walikutwa wamefariki katika Kijiji cha Ngararambe Kata ya Nyakahura wilayani Biharamulo vifo vyao vikihusishwa na kukosa hewa ndani ya nyumba baada ya kuacha jiko la mkaa likiwaka.
Katika tukio jingine la Januari 19, lililotokea katika Kitongoji cha Nyakanyasi, Tarafa ya Kaisho Wilayani, Peter Ezekiel ( 27 ) alikutwa ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili chumbani kwake.
Kamanda Malimi alisema mbali ya Ezekiel kuchinjwa shingo, alikatwa kichwani na kuondolewa sehemu zake za siri na kisha mwili wake kupelekwa katika chumba kingine na kuchomwa moto na watu wasiojulikana. Alisema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa.
Kamanda huyo alisema tukio jingine lilitokea Januari 21 katika Kitongoji cha Kyenguge Kata ya Katereteo, Bukoba. Katika tukio hilo, Rwegasira Godwine (29 ) alikutwa sebuleni nyumbani kwake akiwa amepigwa na kitu kizito kichwani na mwili wake kuchoma moto.
Alisema kabla ya tukio hilo ulitokea ugomvi kati ya marehemu na vijana wawili ambao ni aliwataja vijana wawili waliokuwa marafiki zake ambao alisema walihitilafiana kwa kutembea na mwanamke ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na marehemu.
Kamanda huyo akielezea tukio jingine la mauaji lililotokea katika Kitongoji cha Kibamba, Kijiji cha Nyabugombe wilayani Biharamulo ambako Philbert Kinyana (37) mfugaji na mfanyabiashara wa nyama, mkazi wa Ngara mjini alipigwa risasi na watu wasiojulikana.
Na Shaaban Ndyamukama, Mwananchi
URAIS WA TUNDU LISSU WAMVURUGA MBUNGE CCM
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amefunguka juu ya kauli ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuwa akipewa nafasi ya kugombea Urais yuko tayari kukiwakilisha chama chake na kudai suala hilo lilikuwa ni ndoto yake.
Musukuma amedai kauli ya Tundu Lissu inaonesha alikuwa akitamani kuwania nafasi ya Urais kwa muda mrefu ndiyo maana amekuwa haonekani mara kwa mara kwenye jimbo lake bali anafanya siasa za kitaifa.
Musukuma amesema, "ukiona mtu aliyenusurika kufa halafu ameamka tu anawaza Urais maana yake alikuwa na ndoto ya kuwa rais wa Tanzania ndiyo maana alipotoka tu kwenye matibabu akasema anataka kuwa Rais wa nchi."
"Tumuombe Mungu kwa kuwa tu amelitanguliza suala la mapenzi ya jinsia moja hata huko kwenye chama chake naamini kuna watu hawataki ushoga kama tumekaa miaka yote bila kupitisha ushoga kwanini tupitishe ushoga kwenye Urais wa Tundu Lissu", ameongeza Musukuma.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa sasa yuko nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu kufuatiwa kushambuliwa kwa risasi mwishoni mwa mwaka 2017 na hivi karibuni baada ya kupata nafuu alitangaza nia ya kuwania Urais endapo ataaminiwa na chama chake.
BASI LA FIKOSHI LAPINDUKA NA KUUA WATU WANNE, KUJERUHI 42
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 42 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya FIKOSHI linalofanya safari zake kati ya Kigoma na Mwanza kupoteza mwelekeo na kupinduka katika eneo la Uvinza mkoani Kigoma usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva wa basi hilo, na kusababisha kupinduka.
“Ajali imetokea maeneo ya Uvinza, kuna sehemu inaitwa Mnarani, ni barabara ya Vumbi, ilipofika maeno hayo ambayo ina kona kona nyingi, kwa mujibu wa mashuhuda wamesema dereva alikuwa kwenye mwendo kasi, alipofika maeno hayo, gari ikapinduka na kusababisha vifo vyo watu wanne wanaume watatu na mwanamke mmoja, na majeruhi 42.
"Majeruhi tumewachukua kuwapeleka hospitali ya Maweni ya Mkoa ambako wanaendelea kupata matibabu”, amesema Kamanda Otieno.
HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 24,2019.
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 24, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.
Wednesday, 23 January 2019
HALMASHAURI YA MJI NJOMBE YAIPIGA MSASA MANISPAA YA SUMBAWANGA SIRI YA USAFI WA MAZINGIRA
Halmashauri ya Mji Njombe imepokea ugeni wa Madiwani wakiambatana na Wataalamu kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga lengo ikiwa ni kujifunza na kuongeza maarifa kuhusiana na maswala ya mapato na usafi wa Mazingira. Hayo yalibainika wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wageni hao iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, ambapo ugeni huo ulikiri wazi kuwa wamevutiwa kufika Halmashauri ya Mji Njombe kujifunza kutokana na sifa ambazo Halmashauri imekuwa ikijizolea kila mara katika eneo la usafi wa Mazingira pamoja na ukusanyaji mapato. “Halmashauri ya Mji Sumbawanga kwa mwaka wa fedha…
MBUNGE MAVUNDE ATIMIZA AHADI YAKE KWA MTOTO CHRISTOPHER MASAKA,AIOMBA JAMII KUSAIDIA WENYE MAHITAJI
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony P. Mavunde ameiomba jamii kuwasaidia watu wenye mahitaji ili kuwawezesha kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Mavunde ameyasema hayo leo katika Shule ya Fountain Gate Academy wakati akimkabidhi mtoto Christopher Masaka kwa Uongozi wa shule hiyo na kusajiliwa rasmi kama Mwanafunzi wa shule hiyo. Mtoto Christopher Masaka alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa viungo uliopelekea kukatwa miguu yake yote miwili katika Hospital ya Benjamin Mkapa ambapo Hospital ya Benjamin Mkapa ilitoa msaada wa kiti mwendo “wheelchair” kwa mtoto…
WANANCHI WAMHITAJI LAMBALAMBA WATISHIA KUGOMA MAENDELEO WASIPOSIKILIZWA
Na Amiri kilagalila Wananchi wa kijiji cha Ikondo kata ya Ikondo kilichopo Lupembe wilaya ya Njombe wametishia kugoma kushiriki katika shughuli za maendeleo mbele ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri endapo hawatapewa ruhusa ya kuwaleta waganga wa kienyeji maarufu Kama LAMBALAMBA ili waweze kusafisha kijiji chao ambacho kinatajwa kutawaliwa na washirikina wengi. Wamesema wamelazimika kuazimia kususia kujitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuwa usalama wa maisha yao umetoweka kijijini hapo kwa kuwa kumekuwa na kesi nyingi za wanawake kuingiliwa kingono kimazingara huku wengine wakijikuta wamelala wakiamkia…
SIMBA SC WAICHAPA AFC LEOPARD 2 - 1
Simba SC imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Afc Leopard na kufuzu kucheza nusu fainali